Escrow: Wale waliochukulia Stanbic hawafahamiki; watarudisha kweli?

Escrow: Wale waliochukulia Stanbic hawafahamiki; watarudisha kweli?

Kwa hisani ya Yeriko:

Kampuni hii inayomiliki hisa 50% kwenye kampuni ya PAP iliyonunua hisa zote za IPTL iliyoliingiza taifa kwenye hasara ya trilioni moja nukta nane hilo ni sehemu ya sababu ya watz kulazimika kuifahamu.
Simba trust imesajiliwa nchini Australia chini ya uwakilishi wa mwanasheria mmoja wa Australia mwenye uswahiba na Tanzania.

Taarifa toka Afrika ya Kusini zinasema Simba Trust imetumiwa na Rais Jacob Zuma kuibia madini nchini Kongo katika kipindi cha vita vya kuwafukuza M23 mashariki mwa nchi ya Kongo, Ndani ya ANC kumeibuka msuguano mkubwa watu wakihoji utajiri wa ghafla wa Rais Zuma tangu kipindi kifupi cha Vitata ya M23,

Taarifa zinasema wizi huo wa madini katika mgongo wa vita vya kimataifa ulizihusisha mamlaka za urais wa nchi tatu ambazo ni Zuma, Kabila na Kikwete, na katika kipindi hicho mpaka sasa, kampuni hiyo haijawahi kulipa kodi kwa biashara hiyo mahali popote katika nchi hizo hali inayotafsiriwa kuwa walifanya hivyo kwa "wizi".

Hapa kwetu tunaona jinsi kampuni hii inavyonufaika kwa wizi huu wa Escrow kwa mabilioni ya umma na nguvu kubwa ya wabunge wa chama tawala kutetea wizi huu. Katika taarifa ya PAC Katibu wa Rais Prosper Mbena ameshiriki kuchota mabilioni ya pesa hizi za umma,

Ikiwa Prospet Mbena amesaini barua kuruhusu pesa zitoke kwa niaba ya raisi huu ni uhusika wa rais yeye binafsi na si kama taasisi, kwani huyu Prosper ni msaidizi wake private.

Kama ingekuwa ni taasisi ya urais tulitegemea Sefue ndiyo asaini, unaweza sasa kutofautisha na kupata picha nia ya ya serikali kuchukua hatua dhidi ya uovu huu ni chafu yenye kulinda maslahi binafsi zaidi.

Tutumie mda wetu kwa maslahi mapana ya taifa letu kuitafuta Simba Trust na umiliki wake na biashara zake hii ni baada ya wale niliowataja wiki juzi kukanusha umiliki huo, ili tujue tunayepambana nae ni nani? isije kuwa ndie tuliyemtanguliza vitani..
 
Ngeleja kaonyesha mfano! Kwa kuwa yeye ya kwake alichukulia mkombozi bank! Hivi wale wasiofahamika na waliochukulia Stanbic Bank watarudisha kweli?
Kabla hawajarudisha Yesu atakuwa kesharudi
Ngoja waje

Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app


Sent from my SM-J200F using JamiiForums mobile app
 
Tutumie mda wetu kwa maslahi mapana ya taifa letu kuitafuta Simba Trust na umiliki wake na biashara zake hii ni baada ya wale niliowataja wiki juzi kukanusha umiliki huo, ili tujue tunayepambana nae ni nani? isije kuwa ndie tuliyemtanguliza vitani
Mkuu nashukuru kwa kunitoa tongo tongo!! Dah?
 
Tutawajua siku kesi ya Ruge itakapoanza kuunguruma ..................!!
 
Hizo haziwezi kurudi maana ndio zilimwingiza Sizonje madarakani!
Muongo mkubwa wewe zingekuwa ndio zimemwingiza madarakani ndio angesimamia zirudishwe au waliozitoa wafikishwe mahakamni hata akili kidogo tu mnashindwa kuzitumia,acha kufikiri kwa kutumia unyayo ,tumia bongo kaka.
 
Ruge na singasinga wataimba kama chiriku huko mahakamani na tusubiri,muda si mrefu wale waliobeba kwa lumbesa pale stanbic wataimbwa tu ,singasinga hapendengi kuchuchumalishwa bana
 
Asiyerudisha ni yule ambaye mwilini hana matundu yaliyowazi!
 
Ngeleja kaonyesha mfano! Kwa kuwa yeye ya kwake alichukulia mkombozi bank! Hivi wale wasiofahamika na waliochukulia Stanbic Bank watarudisha kweli?
Hao wanalindwa na katiba ya nchi na wengine walifadhili chama chetu uchaguzi 2015
 
Ngeleja kaonyesha mfano! Kwa kuwa yeye ya kwake alichukulia mkombozi bank! Hivi wale wasiofahamika na waliochukulia Stanbic Bank watarudisha kweli?

Hii sasa ni ile kuisoma namba kwa kumakinika. Nchi imejaa hofu kila kona kwa kumwogopa mtu mmoja. Huyu Sizonje anatisha kama UKIMWI!! Yaani hawa kina William Mganga Ngeleja walokuwa na nyodo, jeuri na mbwembwe za kila leo wanarudisha fueza ya Escrow bila kupenda kwa kumwogopa Magufuli, hatari sana mzazi!!!
Yaani Ngeleja na usukuma wake kamwogopa msukuma mwenzie kisa kupelekwa KEKO kunyea ndoo!!! Kazitema 40.4m/- za Escrow bila kupenda Bado tunamdai za MAKINIKIA maana huyu jamaa alipita kote huko kwenye migodi

Bado namsubiri Msukuma mwenzao Andrew Chenge ambaye huwa hababaiki na mtu! Je, safari hii atarejesha vile vijisenti vya RADA(2 Billioni), ESCROW( 1.6 Billion) na MAKINIKIA( Trillions+).
Picha inazidi kunoga. CCM watajuta kwanini huyu jamaa walimpendekeza kuwa mgombea a Urahisi ilhali alikuwa hana sifa za kuingia Ikulu? Ngoja sasa awashikishe adabu wakome na wakomae!!!
 
Haya mambo haya..... hadi mtu unatamani kipindi kile cha mabomu ya Mbagala na Goms ungekuwa na rimoti ukayaelekeza mabomu yale maeneo tofauti tofauti ya kudondokea. Basi tu Mungu siyo abdala.
 
kama fedha zimechukuliwa na SIMBA yanga awezi kufua dafu kuzichukua ahaaaa!!!
 
Muongo mkubwa wewe zingekuwa ndio zimemwingiza madarakani ndio angesimamia zirudishwe au waliozitoa wafikishwe mahakamni hata akili kidogo tu mnashindwa kuzitumia,acha kufikiri kwa kutumia unyayo ,tumia bongo kaka
Teh teh teh...!! Pole pole msije pigana
 
Haya mambo haya..... hadi mtu unatamani kipindi kile cha mabomu ya Mbagala na Goms ungekuwa na rimoti ukayaelekeza mabomu yale maeneo tofauti tofauti ya kudondokea. Basi tu Mungu siyo abdala
Mkuu kwa sentence hii, hata mi naunga mkono😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom