Eritrea panatisha, Bora Tanzania

Duh huko ni hataru sio pa kwenda
Nchini Eritrea hakuna mashine za ATM na kadi za simu ni bidhaa adimu
15 Oktoba 2019

Mafunzo ya jeshi ni lazima kwa vijana nchini Eritrea
Eritrea imekuwa ikielezwa kuwa moja kati ya nchi ambazo zinaelezwa kuwa watu wake wanakosa misingi muhimu ya uhuru wa dini na kisiasa.

Suala hili si la ajabu kutokana na kuwepo kwa utawala wa chama kimoja chini ya raisi Isaias Afwerki ambaye amekuwa madarakani tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ethiopia mwaka 1993.

Serikali ilipiga marufuku vyama vya upinzani na vyombo vya habari binafsi, pia iliwafunga wakosoaji wa serikali (baadhi ambao hawajasikika kwa miaka sasa) na kuwasajili jeshini vijana wadogo.

Hali hii iliwafanya mamia ya raia wa Eritrea kuikimbia nchi hiyo, Mwandishi wa BBC ameandika namna ambavyo serikali imekuwa ikiyadhibiti maisha ya watu.

1) Kadi za simu ni gharama

Mtandao wa simu unaomilikiwa na serikali, Eri Tel ndio pekee unaotoa huduma za mawasiliano. Huduma zinazotolewa ni mbaya, na unadhibitiwa vikali na serikali.

Ripoti ya Shirikisho la kimataifa kuhusu masuala ya mawasiliano inasema kupenya kwa huduma za mtandao wa intaneti nchini Eritrea ni juu ya asilimia 1.

Wananchi wanapaswa kujisajili serikalini ili kupata kadi ya simu.

Na hata ukupata kadi, huwezi kuitumia ili kupata mtandao wa intaneti kwa sababu hakuna data.

Watu hulazimika kupata mtandao wa kutumia WiFi, lakini mtandao uko chini sana. Kuingia kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter, watu hutumia mtandao wa VPN (virtual private network) ili kuzuia udhibiti wa serikali.

Kwa kuwa kuna ugumu mkubwa wa kupata kadi za simu, watu bado wanategemea simu za Umma za kulipia kabla ya mazungumzo.

2) Watu hutoa hela ndani ya benki pekee

Hela ya Eritrea
Serikali imeweka sheria kali kuhusu kiasi cha fedha kinachotolewa na wateja wa benki kutoka kwenye akaunti zao.

Hata kama wana mamilioni ya fedha katika akaunti zao, wanaruhusiwa kutoa kiasi cha dola za Marekani 330 kwa mwezi.

Wafanyabiashara hupendelea kuwa na fedha mkononi kwa kuwa mzunguko wa fedha ni mdogo.

Hakuna mashine za kutoa fedha (ATM) nchini Eritrea .Ikiwa kuna shughuli ya harusi siku za usoni, na wahusika wakihitaji fedha zaidi, huomba barua ya kibali kutoka serikalini kwenda benki , na kuruhusiwa kutoa zaidi ya kiasi kilichowekwa na serikali.

Raia wa Eritrea wametoa maoni tofauti kuhusu sababu za serikali kuweka vikwazo katika kutoa fedha. Baadhi wanasema nia ya serikali ni ''kujenga tabia za watu wenye kujiwekea akiba na kupambana na gharama za maisha'' wengine wakisema kuwa ''serikali haipendi shughuli za kibiashara. Hivyo kudhibiti mzunguko wa fedha''.

3) Kuna televisheni moja pekee nchini humo.

Watu wengi wanapenda kutazama chaneli za kigeni za televisheni
Eri-Tv ni televisheni pekee iliyo nchini ya serikali ya Eritrea. Ni chombo kinachoisemea serikali, lakini ukiwa na satelaiti unaweza kutazama televisheni nyingine za kimataifa.

Kamati ya kutetea waandishi wa habari (CPJ) inatazama kwa karibu suala la uhuru wa vyombo vya habari nchini Eritrea, ikiitaja kuwa nchi inayodhibiti zaidi uhuru wa vyombo vya habari'', nyuma ya Korea Kaskazini.

Hatahivyo, Waziri wa habari Yemane Meskel anasema kuwa asilimia 91% ya nyumba za watu zina mabeseni ya satelaiti.

4 ) Vijana wadogo wanataka kuondoka

''Kupata pasi ya kusafiria ni kama ndoto iliyokuwa kweli,'' anasema kijana mmoja.

Lakini anasema vijana hawapewi pasi za kusafiria mpaka baada ya kufuzu mafunzo ya jeshi.

Wengine huhatarisha maisha kwa kufanya safari wakivuka bahari ya Mediterrania ili kufika Ulaya, wengi hufa kutokana na njaa na kiu kwenye jangwa na baharini.
 
Niliwahi kufika Massawa mji wa bandari wa Eritrea katika harakati za kutafuta maisha. Wakati wa ujenzi wa barabara kutoka Massawa kwenda Asseb.
Miongoni mwa safari zilizonikatisha tamaa sana kutokana na hali mbaya niliyokutana nayo.

Hali yao ni duni sana hasa ikielezwa kwa sababu ya Vita kati yake na Ethiopia (miaka hiyo)
Mambo machache kuhusu Eritrea
1. Nchi ina mfumo wa Chama kimoja na Rais wake ni Isaias Afrwerki ambaye amekuwa rais tangu 1993.

2. Hakuna uchaguzi ambao umewahi kufanyika

3. Nchi ina rekodi mbaya kwenye Haki za Binadamu inaifuatia Korea Kaskazini kwa rekodi mbaya zaidi.

4. Inakadiriwa ina idadi ya watu takribani milioni tano.

5. Vyombo vyote vya habari vinamilikiwa na serikali.

6. Kuna vyuo vikuu viwili tu ambavyo ni Asmara University na Eritrea Institute of Technology.

7. Wana shirika la ndege linalomiliki ndege moja tu Boeing 767-366/ER

8. Kuna wanawake wazuri sana, wanafana sana na Waethiopia.

9. Mjini Massawa kuna vijana wengi wa Kitanzania ambao hufanya kazi kwenye kampuni za Kichina kwenye miradi ya ujenzi.
Nilibahatika kukutana na vijana zaidi ya 40 wa Kitanzania na Kenya.

10. Waeritrea ni wapole sana. Si mahali ambapo kuna fujo na uhuni sana.
Nimeishi na kufanya kazi na Wa Eritrea ni wapole lakini wanaipenda sana nchi yao, pia wana jisifia sana kuishinda Ethiopia kwenye vita yao, ni kama sisi na waganda. Watu wengi huwafananisha na Waethiopia na hawapendi hilo kabisa.
Wanajituma na ni wavumilivu pia .
 
Nchini Eritrea hakuna mashine za ATM na kadi za simu ni bidhaa adimu
15 Oktoba 2019

Mafunzo ya jeshi ni lazima kwa vijana nchini Eritrea
Eritrea imekuwa ikielezwa kuwa moja kati ya nchi ambazo zinaelezwa kuwa watu wake wanakosa misingi muhimu ya uhuru wa dini na kisiasa.

Suala hili si la ajabu kutokana na kuwepo kwa utawala wa chama kimoja chini ya raisi Isaias Afwerki ambaye amekuwa madarakani tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ethiopia mwaka 1993.

Serikali ilipiga marufuku vyama vya upinzani na vyombo vya habari binafsi, pia iliwafunga wakosoaji wa serikali (baadhi ambao hawajasikika kwa miaka sasa) na kuwasajili jeshini vijana wadogo.

Hali hii iliwafanya mamia ya raia wa Eritrea kuikimbia nchi hiyo, Mwandishi wa BBC ameandika namna ambavyo serikali imekuwa ikiyadhibiti maisha ya watu.

1) Kadi za simu ni gharama

Mtandao wa simu unaomilikiwa na serikali, Eri Tel ndio pekee unaotoa huduma za mawasiliano. Huduma zinazotolewa ni mbaya, na unadhibitiwa vikali na serikali.

Ripoti ya Shirikisho la kimataifa kuhusu masuala ya mawasiliano inasema kupenya kwa huduma za mtandao wa intaneti nchini Eritrea ni juu ya asilimia 1.

Wananchi wanapaswa kujisajili serikalini ili kupata kadi ya simu.

Na hata ukupata kadi, huwezi kuitumia ili kupata mtandao wa intaneti kwa sababu hakuna data.

Watu hulazimika kupata mtandao wa kutumia WiFi, lakini mtandao uko chini sana. Kuingia kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter, watu hutumia mtandao wa VPN (virtual private network) ili kuzuia udhibiti wa serikali.

Kwa kuwa kuna ugumu mkubwa wa kupata kadi za simu, watu bado wanategemea simu za Umma za kulipia kabla ya mazungumzo.

2) Watu hutoa hela ndani ya benki pekee

Hela ya Eritrea
Serikali imeweka sheria kali kuhusu kiasi cha fedha kinachotolewa na wateja wa benki kutoka kwenye akaunti zao.

Hata kama wana mamilioni ya fedha katika akaunti zao, wanaruhusiwa kutoa kiasi cha dola za Marekani 330 kwa mwezi.

Wafanyabiashara hupendelea kuwa na fedha mkononi kwa kuwa mzunguko wa fedha ni mdogo.

Hakuna mashine za kutoa fedha (ATM) nchini Eritrea .Ikiwa kuna shughuli ya harusi siku za usoni, na wahusika wakihitaji fedha zaidi, huomba barua ya kibali kutoka serikalini kwenda benki , na kuruhusiwa kutoa zaidi ya kiasi kilichowekwa na serikali.

Raia wa Eritrea wametoa maoni tofauti kuhusu sababu za serikali kuweka vikwazo katika kutoa fedha. Baadhi wanasema nia ya serikali ni ''kujenga tabia za watu wenye kujiwekea akiba na kupambana na gharama za maisha'' wengine wakisema kuwa ''serikali haipendi shughuli za kibiashara. Hivyo kudhibiti mzunguko wa fedha''.

3) Kuna televisheni moja pekee nchini humo.

Watu wengi wanapenda kutazama chaneli za kigeni za televisheni
Eri-Tv ni televisheni pekee iliyo nchini ya serikali ya Eritrea. Ni chombo kinachoisemea serikali, lakini ukiwa na satelaiti unaweza kutazama televisheni nyingine za kimataifa.

Kamati ya kutetea waandishi wa habari (CPJ) inatazama kwa karibu suala la uhuru wa vyombo vya habari nchini Eritrea, ikiitaja kuwa nchi inayodhibiti zaidi uhuru wa vyombo vya habari'', nyuma ya Korea Kaskazini.

Hatahivyo, Waziri wa habari Yemane Meskel anasema kuwa asilimia 91% ya nyumba za watu zina mabeseni ya satelaiti.

4 ) Vijana wadogo wanataka kuondoka

''Kupata pasi ya kusafiria ni kama ndoto iliyokuwa kweli,'' anasema kijana mmoja.

Lakini anasema vijana hawapewi pasi za kusafiria mpaka baada ya kufuzu mafunzo ya jeshi.

Wengine huhatarisha maisha kwa kufanya safari wakivuka bahari ya Mediterrania ili kufika Ulaya, wengi hufa kutokana na njaa na kiu kwenye jangwa na baharini.

HAHAAAAA BRITANNICA.COM

Nimeishi na kufanya kazi na Wa Eritrea ni wapole lakini wanaipenda sana nchi yao, pia wana jisifia sana kuishinda Ethiopia kwenye vita yao, ni kama sisi na waganda. Watu wengi huwafananisha na Waethiopia na hawapendi hilo kabisa.
Wanajituma na ni wavumilivu pia .
Ni kweli kabisa. Nadhani wanasiasa hasa rais wao ndio anawaangusha hawa watu na kuwanyima uhuru na maendeleo.
 
Dah hao jamaa kweli wamekamatika. ukisikia udikteta ndo huo sasa. ndomana huu wa hapa watu waliuita udikteta uchwara.
Lakini hapa tuna mbuyu ambao ndiyo unaanza sasa nyie sijui mnadhani ni mchicha huu
Ya heritrea kutukuta ni suala la mda tu
 
tatizo unaishi kwa kukariri,,usikariri kuwa kila asie CCM basi ni CHADEMA,,wengine hatupo kote kote,,,and YES,,,makamanda uchwara wapo pia
Kukariri???
Mimi na chagua pale au chama ninacho ona kina maslaha kwangu na taifa na nadhani na wewe pia unapaswa ufanye hivyo kama wewe sio mwanasiasa. Sishabikii chama Kama club ya mpira. Kabla ya Magufuli nilikua sitaki kusikia CCM, wakati huo CHADEMA kilikua na sera za kueleweka, Sasa 70% niko kwa Magu na hizo 30% sijaona bado chama kingine chenye sera za kueleweka.
Magufuli anafanya vizuri na pia anamakos anayofanya, lakini mazuri yakilinganishwa na makosa mazuri yana zidi. Ndio maana kuna kipindi wenzetu walioendelea huko ulaya walitaka kukata misaada, Sweden mmoja wapo lakini wao wakaona ni busara kwanza kumtuma waziri wao nadhani alikua waziri wa mambo ya nje. Huyo jamaa kaja kuonana na Magufuli na akawekewa kila kitu juu ya meza bada ya hapo katoka na kuonana viongizi wa upinzani na hapo akelezewa kila kitu. Alivyo rudi jamaa waka kaa kimya hadi leo... Ni kwa sababu gani unadhani wameamua kukaa kinya? Au huyo waziri alihingwa na Magu?
Tanzania tunahitaji upinzani, upinzani wenye sera nzito si kupinga tu kila kitu. Inabidi watoe sera kwamba wanaweza kufanya vizuri zaidi kuliko anavyo fanya na kwa njia ipi...
 
Kuondoka sio suluhisho. Yaani mafunzo yote hayo ya jeshi wanapewa bure bado wanakaa tu? NI sawa na ukiwa na njaa mtu anakupa chakula halafu unataka kwenda kwa jirani kula.

Wanahitaji kupigiwa ngoma ili watambue wanawezaje kuyatumia mafunzo yao ya jeshi?
Mkuu ukiona hivyo ujue watu wamebanwa haswa.
 
Hata Eritrea nao wataasema Tanzania panatisha maana mbunge anamiminiwa risasi zaid ya 30 na raia wanatekwa yaan mpaka bilionea anatekwaa
 
Back
Top Bottom