Eritrea panatisha, Bora Tanzania

Eritrea panatisha, Bora Tanzania

Hivi inakuwaje mtu mmoja anaweza kuwaburuza mamilioni atakavyo?.Ndio kusema Africa hamnaga wana mapinduzi wa kweli.

Mbona hata hapa jiwe anatuburuza apendavyo. Ni kama hapa tu, kinachofanyika mpaka kufikia huko vyombo vya dola hutumika na sana ni kwakupewa mishahara minono, na hawasumbiliwi wala kukaguliwa vyeti fake. Vyombo vya dola huweza kufanya lolote na hutekwa na maneno ya viongozi kwa kujifanya wazalendo, ghiliba hiyo huwaingia vyombo vya dola na hasa ukizingatia mishahara na marupurupu manono wanayopewa hugeuka vipofu wa unyama wote. Kisha huundwa kundi la watu wasiojulikana, hili hufanya ukatili wa kutisha huku vyombo vya dola vikifumbia macho mambo hayo, mfano hapa kwetu. Viongozi wa vyombo vya dola huhongwa vyeo na kuwa upande wa kiongozi kwa lolote mfano hapa kwetu. Chaguzi zote huwa kiini macho, na wanaotangazwa washindi ni wale wanaotakiwa na mtawala ili kumpitishia sheria zake za ukandamizaji, mfano huo pia uko hapa kwetu.

Bunge na mahakama nazo hujikuta katika hali hii ya kutii kila kitu kwani kundi la watu wasiojulikana hutumika kumnyamazisha yoyote anayekuwa kikwazo. Gia inayotumika kupandikiza unyama wote huu ni neno uzalendo. Yoyote asiyemtii mtawala huonwa ni msaliti. Wakati hayo yakiendelea zaidi ya nusu ya wananchi hulishwa propaganda na ghafla nchi nzima hujikita ikimsifia mtawala wa aina hiyo. Mifano ya mambo hayo iko wazi hata hapa nchini.
 
Nchini Eritrea hakuna mashine za ATM na kadi za simu ni bidhaa adimu
15 Oktoba 2019

Mafunzo ya jeshi ni lazima kwa vijana nchini Eritrea
Eritrea imekuwa ikielezwa kuwa moja kati ya nchi ambazo zinaelezwa kuwa watu wake wanakosa misingi muhimu ya uhuru wa dini na kisiasa.

Suala hili si la ajabu kutokana na kuwepo kwa utawala wa chama kimoja chini ya raisi Isaias Afwerki ambaye amekuwa madarakani tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ethiopia mwaka 1993.

Serikali ilipiga marufuku vyama vya upinzani na vyombo vya habari binafsi, pia iliwafunga wakosoaji wa serikali (baadhi ambao hawajasikika kwa miaka sasa) na kuwasajili jeshini vijana wadogo.

Hali hii iliwafanya mamia ya raia wa Eritrea kuikimbia nchi hiyo, Mwandishi wa BBC ameandika namna ambavyo serikali imekuwa ikiyadhibiti maisha ya watu.

1) Kadi za simu ni gharama

Mtandao wa simu unaomilikiwa na serikali, Eri Tel ndio pekee unaotoa huduma za mawasiliano. Huduma zinazotolewa ni mbaya, na unadhibitiwa vikali na serikali.

Ripoti ya Shirikisho la kimataifa kuhusu masuala ya mawasiliano inasema kupenya kwa huduma za mtandao wa intaneti nchini Eritrea ni juu ya asilimia 1.

Wananchi wanapaswa kujisajili serikalini ili kupata kadi ya simu.

Na hata ukupata kadi, huwezi kuitumia ili kupata mtandao wa intaneti kwa sababu hakuna data.

Watu hulazimika kupata mtandao wa kutumia WiFi, lakini mtandao uko chini sana. Kuingia kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter, watu hutumia mtandao wa VPN (virtual private network) ili kuzuia udhibiti wa serikali.

Kwa kuwa kuna ugumu mkubwa wa kupata kadi za simu, watu bado wanategemea simu za Umma za kulipia kabla ya mazungumzo.

2) Watu hutoa hela ndani ya benki pekee

Hela ya Eritrea
Serikali imeweka sheria kali kuhusu kiasi cha fedha kinachotolewa na wateja wa benki kutoka kwenye akaunti zao.

Hata kama wana mamilioni ya fedha katika akaunti zao, wanaruhusiwa kutoa kiasi cha dola za Marekani 330 kwa mwezi.

Wafanyabiashara hupendelea kuwa na fedha mkononi kwa kuwa mzunguko wa fedha ni mdogo.

Hakuna mashine za kutoa fedha (ATM) nchini Eritrea .Ikiwa kuna shughuli ya harusi siku za usoni, na wahusika wakihitaji fedha zaidi, huomba barua ya kibali kutoka serikalini kwenda benki , na kuruhusiwa kutoa zaidi ya kiasi kilichowekwa na serikali.

Raia wa Eritrea wametoa maoni tofauti kuhusu sababu za serikali kuweka vikwazo katika kutoa fedha. Baadhi wanasema nia ya serikali ni ''kujenga tabia za watu wenye kujiwekea akiba na kupambana na gharama za maisha'' wengine wakisema kuwa ''serikali haipendi shughuli za kibiashara. Hivyo kudhibiti mzunguko wa fedha''.

3) Kuna televisheni moja pekee nchini humo.

Watu wengi wanapenda kutazama chaneli za kigeni za televisheni
Eri-Tv ni televisheni pekee iliyo nchini ya serikali ya Eritrea. Ni chombo kinachoisemea serikali, lakini ukiwa na satelaiti unaweza kutazama televisheni nyingine za kimataifa.

Kamati ya kutetea waandishi wa habari (CPJ) inatazama kwa karibu suala la uhuru wa vyombo vya habari nchini Eritrea, ikiitaja kuwa nchi inayodhibiti zaidi uhuru wa vyombo vya habari'', nyuma ya Korea Kaskazini.

Hatahivyo, Waziri wa habari Yemane Meskel anasema kuwa asilimia 91% ya nyumba za watu zina mabeseni ya satelaiti.

4 ) Vijana wadogo wanataka kuondoka

''Kupata pasi ya kusafiria ni kama ndoto iliyokuwa kweli,'' anasema kijana mmoja.

Lakini anasema vijana hawapewi pasi za kusafiria mpaka baada ya kufuzu mafunzo ya jeshi.

Wengine huhatarisha maisha kwa kufanya safari wakivuka bahari ya Mediterrania ili kufika Ulaya, wengi hufa kutokana na njaa na kiu kwenye jangwa na baharini.
Kuna watu hawaipendi Tanzania yetu, bora wahamie huko.
 
Mkuu usiseme afadhali ya Tanzania wakati,Magufuli ndo anatamani tufike huko, wakati wa kikwete hali haikuwa Kama ilivyo leo.
Endapo Magufuli atang'ang'ania madarakani na sisi Tanzania tutakuwa kama Eritrea pia, kwanza mpango wake ni kuua sekta zote binafsi ,Tazama alivyoiua fast jet ili ATCL iinuke, amezima uhuru wa Habari hata humu JF yale mazito tunayoandika mods wanayafuta kwa hofu ya kukamatwa.
 
Niliwahi kufika Massawa mji wa bandari wa Eritrea katika harakati za kutafuta maisha. Wakati wa ujenzi wa barabara kutoka Massawa kwenda Asseb.
Miongoni mwa safari zilizonikatisha tamaa sana kutokana na hali mbaya niliyokutana nayo.

Hali yao ni duni sana hasa ikielezwa kwa sababu ya Vita kati yake na Ethiopia (miaka hiyo)
Mambo machache kuhusu Eritrea
1. Nchi ina mfumo wa Chama kimoja na Rais wake ni Isaias Afrwerki ambaye amekuwa rais tangu 1993.

2. Hakuna uchaguzi ambao umewahi kufanyika

3. Nchi ina rekodi mbaya kwenye Haki za Binadamu inaifuatia Korea Kaskazini kwa rekodi mbaya zaidi.

4. Inakadiriwa ina idadi ya watu takribani milioni tano.

5. Vyombo vyote vya habari vinamilikiwa na serikali.

6. Kuna vyuo vikuu viwili tu ambavyo ni Asmara University na Eritrea Institute of Technology.

7. Wana shirika la ndege linalomiliki ndege moja tu Boeing 767-366/ER

8. Kuna wanawake wazuri sana, wanafana sana na Waethiopia.

9. Mjini Massawa kuna vijana wengi wa Kitanzania ambao hufanya kazi kwenye kampuni za Kichina kwenye miradi ya ujenzi.
Nilibahatika kukutana na vijana zaidi ya 40 wa Kitanzania na Kenya.

10. Waeritrea ni wapole sana. Si mahali ambapo kuna fujo na uhuni sana.
 
Tumefikia kujilinganisha na Eritrea?!
Kweli tumerudi nyuma miaka 50.
Nakulilia Tanganyika yangu.
 
Nchini Eritrea hakuna mashine za ATM na kadi za simu ni bidhaa adimu 15 Oktoba 2019
Mafunzo ya jeshi ni lazima kwa vijana nchini Eritrea
Eritrea imekuwa ikielezwa kuwa moja kati ya nchi ambazo zinaelezwa kuwa watu wake wanakosa misingi muhimu ya uhuru wa dini na kisiasa.
Suala hili si la ajabu kutokana na kuwepo kwa utawala wa chama kimoja chini ya raisi Isaias Afwerki ambaye amekuwa madarakani tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ethiopia mwaka 1993.
Serikali ilipiga marufuku vyama vya upinzani na vyombo vya habari binafsi, pia iliwafunga wakosoaji wa serikali (baadhi ambao hawajasikika kwa miaka sasa) na kuwasajili jeshini vijana wadogo.
Hali hii iliwafanya mamia ya raia wa Eritrea kuikimbia nchi hiyo, Mwandishi wa BBC ameandika namna ambavyo serikali imekuwa ikiyadhibiti maisha ya watu.
1) Kadi za simu ni gharama
Mtandao wa simu unaomilikiwa na serikali, Eri Tel ndio pekee unaotoa huduma za mawasiliano. Huduma zinazotolewa ni mbaya, na unadhibitiwa vikali na serikali.
Ripoti ya Shirikisho la kimataifa kuhusu masuala ya mawasiliano inasema kupenya kwa huduma za mtandao wa intaneti nchini Eritrea ni juu ya asilimia 1.
Wananchi wanapaswa kujisajili serikalini ili kupata kadi ya simu.
Na hata ukupata kadi, huwezi kuitumia ili kupata mtandao wa intaneti kwa sababu hakuna data.
Watu hulazimika kupata mtandao wa kutumia WiFi, lakini mtandao uko chini sana. Kuingia kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter, watu hutumia mtandao wa VPN (virtual private network) ili kuzuia udhibiti wa serikali.
Kwa kuwa kuna ugumu mkubwa wa kupata kadi za simu, watu bado wanategemea simu za Umma za kulipia kabla ya mazungumzo.
2) Watu hutoa hela ndani ya benki pekee
Hela ya Eritrea
Serikali imeweka sheria kali kuhusu kiasi cha fedha kinachotolewa na wateja wa benki kutoka kwenye akaunti zao.
Hata kama wana mamilioni ya fedha katika akaunti zao, wanaruhusiwa kutoa kiasi cha dola za Marekani 330 kwa mwezi.
Wafanyabiashara hupendelea kuwa na fedha mkononi kwa kuwa mzunguko wa fedha ni mdogo.
Hakuna mashine za kutoa fedha (ATM) nchini Eritrea .Ikiwa kuna shughuli ya harusi siku za usoni, na wahusika wakihitaji fedha zaidi, huomba barua ya kibali kutoka serikalini kwenda benki , na kuruhusiwa kutoa zaidi ya kiasi kilichowekwa na serikali.
Raia wa Eritrea wametoa maoni tofauti kuhusu sababu za serikali kuweka vikwazo katika kutoa fedha. Baadhi wanasema nia ya serikali ni ''kujenga tabia za watu wenye kujiwekea akiba na kupambana na gharama za maisha'' wengine wakisema kuwa ''serikali haipendi shughuli za kibiashara. Hivyo kudhibiti mzunguko wa fedha''.
3) Kuna televisheni moja pekee nchini humo.
Watu wengi wanapenda kutazama chaneli za kigeni za televisheni
Eri-Tv ni televisheni pekee iliyo nchini ya serikali ya Eritrea. Ni chombo kinachoisemea serikali, lakini ukiwa na satelaiti unaweza kutazama televisheni nyingine za kimataifa.
Kamati ya kutetea waandishi wa habari (CPJ) inatazama kwa karibu suala la uhuru wa vyombo vya habari nchini Eritrea, ikiitaja kuwa nchi inayodhibiti zaidi uhuru wa vyombo vya habari'', nyuma ya Korea Kaskazini.
Hatahivyo, Waziri wa habari Yemane Meskel anasema kuwa asilimia 91% ya nyumba za watu zina mabeseni ya satelaiti.
4 ) Vijana wadogo wanataka kuondoka
''Kupata pasi ya kusafiria ni kama ndoto iliyokuwa kweli,'' anasema kijana mmoja.
Lakini anasema vijana hawapewi pasi za kusafiria mpaka baada ya kufuzu mafunzo ya jeshi.
Wengine huhatarisha maisha kwa kufanya safari wakivuka bahari ya Mediterrania ili kufika Ulaya, wengi hufa kutokana na njaa na kiu kwenye jangwa na baharini.
Tanzania majina ya vituo vya televisheni ni mengi lakini taarifa ya habari ni moja kwa vituo vyote.
 
Wewe na wenzako hamjui mnachoongea. Eritrea na Ethiopia walianza hivi hivi kama Jiwe anavyo-jimwambafai. Mara hiki kimezuiwa leo, mara kile kimezuiwa kesho. Mwisho wakafika hapo walipo leo. Kama hamna akili ni vizuri kunyamaza na kula ugali wenu kimya kimya na kuwaacha wenye akili walinde uhuru wenu wa kikatiba.

Tatizo letu Watanzania ni kukosa kumbukumbu. Mtu kasema hadharani kuwa anatamani malaika wangeshuka kuja kuzima mitandao; sijui watu walidhani anamaanisha nini.
 
Zitto Kabwe anayelalamika udikteta aende akaishi huko ili auone udikteta wa kweli unafanana vipi.

Mtu analia kunyimwa uhuru wa habari wakati akijisikia tu anaweza kupeleka andiko lake ni likachapishwa gazetini.
 
ukiwa na malaria 1 bado unaumwa hata kama icu kuna mtu hajitambui kwa maradhi,haiponyi maradhi yako
 
Back
Top Bottom