Mbona hata hapa jiwe anatuburuza apendavyo. Ni kama hapa tu, kinachofanyika mpaka kufikia huko vyombo vya dola hutumika na sana ni kwakupewa mishahara minono, na hawasumbiliwi wala kukaguliwa vyeti fake. Vyombo vya dola huweza kufanya lolote na hutekwa na maneno ya viongozi kwa kujifanya wazalendo, ghiliba hiyo huwaingia vyombo vya dola na hasa ukizingatia mishahara na marupurupu manono wanayopewa hugeuka vipofu wa unyama wote. Kisha huundwa kundi la watu wasiojulikana, hili hufanya ukatili wa kutisha huku vyombo vya dola vikifumbia macho mambo hayo, mfano hapa kwetu. Viongozi wa vyombo vya dola huhongwa vyeo na kuwa upande wa kiongozi kwa lolote mfano hapa kwetu. Chaguzi zote huwa kiini macho, na wanaotangazwa washindi ni wale wanaotakiwa na mtawala ili kumpitishia sheria zake za ukandamizaji, mfano huo pia uko hapa kwetu.
Bunge na mahakama nazo hujikuta katika hali hii ya kutii kila kitu kwani kundi la watu wasiojulikana hutumika kumnyamazisha yoyote anayekuwa kikwazo. Gia inayotumika kupandikiza unyama wote huu ni neno uzalendo. Yoyote asiyemtii mtawala huonwa ni msaliti. Wakati hayo yakiendelea zaidi ya nusu ya wananchi hulishwa propaganda na ghafla nchi nzima hujikita ikimsifia mtawala wa aina hiyo. Mifano ya mambo hayo iko wazi hata hapa nchini.