Eric Omondi: Namshukuru sana Diamond, ndiye aliyenifungulia mlango kwenye soko la Tanzania

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
16463885_1261927390564600_5944890162558271488_n.jpg


Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya, Erick Omondi ijumaa iliyopita ya tarehe 10 alifunguka jinsi Diamond alivyomsaidia kupenya kwenye soko la Tanzania.

Omondi anasema kwa mara ya kwanza alikutana na Diamond Mombasa nchini Kenya akiwa kwenye harakati za kurekodi wimbo wa Diamond unaoitwa Nabeba Mawe.

Katika mazungumzo yao Diamond alimualika Omondi kwenye show kubwa maarufu kama "Zari All White Part" na kumuomba awe MC wa show.

Katika show hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya wahudhuriaji 10,000 , redio na TV nyingi za Tanzania Omondi hakufanya kosa kama MC, alitumia kudhihirisha kipaji chake cha uchekeshaji na ikawa ndio mwanzo wa kujulikana Tanzania.

Omondi anasema bila Diamond kumwalika Tanzania huenda asingeweza kupenya katika soko la Tanzania, soko lenye mashabiki wengi sana wa kazi zake.

Mpaka sasa Erick Omondi ana mpango katika kipindi cha miezi miwili ijayo, kuanzisha Comedy TV show nchini Tanzania kwenye moja ya Runinga maarufu hapa nchini.
Japo hakuweka wazi kipindi hicho kitarushwa hewani kupitia kituo cha habari cha shirika lipi.

Source: NTV ya nchini Kenya.
 
Diamond platnumz kawabeba wengi, japokuwa wengine viburi hawataki kuadmit lkn bila diamond platnumz mziki wao usinge simama, kila mtu anataka kujenga beef na diamond, kila mtu akifanya kitu lazima akilinganiashe na diamond. Ila tuna washukuru waungwana wachache (ninacho sikitika si watanzania manake sisi tumejaa chuki, wivu na majungu) kama Omondi na Jah Preyah wa Zimbabwe kwa kuliona hili.
 
Hata Kiba alikuwa kaanza kufifia kama kina Bizman, GK na wengine, ila kwa bifu fake na Mondi ndo akatokeamo tena....

Eti King is back!!!!! Ha ha haaa
 
Nice one!! kama mtu anaweza mpe appreciate yake anastahil sio kuendekeza chuki binafsi
 
Hawa kina Eric wa bongo sio wabunifu kwakweli,wao wanasubiri kampeni za fisiemu ndio wapige hela,na kujipendekeza ili wapewe nyadhifa,mtakaa sana Acha Erik apige mijihela
 
Back
Top Bottom