Epuka wizi wa taarifa zako binafsi kwenye simu kupitia nyaya za USB

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Salaam Wakuu,

Katika kuendelea kukumbushana umuhimu wa kulinda taarifa binafsi, leo nimeona nieleze kwa ufupi suala la wizi wa taarifa binafsi unaofanywa kupitia nyaya za kuchajia simu (USB). Tazama kwenye picha hapa chini:

1655788329039.jpeg

Picha> USB Cables za aina mbalimbali

Ni wazi kuwa kutokana na sababu au mbalimbali tunajikuta kwa namna moja au nyingine tunachaji simu zetu maeneo ya umma (Public areas). Inaweza ikawa kwa kutumia USB za wengine au kuchomeka simu zetu kwenye compyuta nk.

Sasa ipo hivi wataalamu wa masuala ya kidijitali wanatahadharisha kuwapo umakini wa matumizi ya USB pindi tunapochaji simu zetu maeneo ya umma kwa sababu kifaa hiki kinaweza kutumika kuhamisha taarifa zako binafsi.

Aidha, inabainishwa kwamba katika nchi zilizoendelea yapo maeneo ya umma ambayo ukichaji simu kwa kutumia USB inayoruhusu taarifa kuhamishika basi unaweza kuibiwa taarifa zeko kwa urahisi hata kama sio kompyuta.

Zaidi ya hayo, mifumo mingi ya 𝗨𝗦𝗕 𝗰𝗵𝗮𝗿𝗴𝗶𝗻𝗴 𝘀𝘁𝗮𝘁𝗶𝗼𝗻 ya public kama (Super Market, Migahawani, mabasi nk) imetengenezwa kwa namna inayoruhusu kusafirisha data. Hivyo wakati wa kusafirisha taarifa zako hupelekea kuingiza virusi, Malware pia hata kukuibia taarifa zako muhimu wakati unatumia, Mfumo huu ujulikana kama Juice Jacking.

Juice jacking
What is juice jacking? - Definition from WhatIs.com ni aina moja wapo ya shambulio la kimtandao (cyber attacking) inahusisha port ya chaji ambapo huweza kusafirisha data zako kupitia USB.

Pia wizi wa taarifa binafsi kupitia USB unaweza kujitokeza pale unapochaji simu yako kwa kutumia vifaa kama vingine kama kompyuta, redio, TV nk.

Hivyo ili kulinda taarifa zako unapochaji simu maeneo ya umma unashauriwa kufanya yafuatayo:
1. Tumia USB ambazo haziruhusu data zako kuhama kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye chombo kingine

2. Ikiwa USB hiyo inaweza kuhamisha mafaili yako basi chagua option ya charge only na uifunge simu yako ili data zako binafsi zisihamishwe. Tazama katika picha hapa chini.

1655790536862.png

Picha> Sehemu ya kuchagua Charge only

3. Tumia USB Kondom, hiki ni kifaa maalumu kinachozuia usafirishaji wa data zako kutoka kwenye simu yako kwenda kwingine unapochaji simu kwenye maeneo ya umma au kwenye compyuta isiyo yako. Tazama picha hapa chini.

1655790354840.jpeg

Picha> USB Condom
4. Tumia Power Bank, hiki ni kifaa maalumu kinachohifadhi nishati ya umeme inayoweza kutumika kuchajia vifaa mbalimbali. Ili kulinda taarifa zako binafsi unashauriwa unapokuwa maeneo ya umma chaji simu yako kwa power bank kwa sababu mfumo wake hauruhusu kuhamisha taarifa za mtu.
 
Kweli kama ni kucharge tu, ni kumake sure simu iko locked na pin, pattern, password au biometrics kabla ya kucharge ili kurestrict access, kama ipo unlocked ni kama mtoa mada alivyosema chagua Charge only.
 
Salaam Wakuu,

Katika kuendelea kukumbushana umuhimu wa kulinda taarifa binafsi, leo nimeona nieleze kwa ufupi suala la wizi wa taarifa binafsi unaofanywa kupitia nyaya za kuchajia simu (USB). Tazama kwenye picha hapa chini....
Ahsante sana kwa elimu.
 
Back
Top Bottom