Tume ya Mawasiliano (Nigeria) yawaonya wanaotuma matangazo kupitia simu. Tanzania sheria ipo, ila matangazo ya simu yanazidi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Tume ya Mawasiliano ya Nigeria imewaonya Watumiaji wa simu kwa matangazo (Telemarketers) kuwa ukusanyaji wa taarifa (data) za wateja kwa matumizi ya Kibiashara ni marufuku nchini humo chini ya Kanuni za Nchi.

Tume ya Mawasiliano ya Nigeria (NCC), Mamlaka ya Udhibiti wa Sekta ya Mawasiliano nchini Nigeria, imewaonya Watumiaji wa simu kwa matangazo (Telemarketers) wanaojihusisha na ukusanyaji haramu wa namba za simu za watumiaji wa simu na taarifa nyingine za binafsi kiudanganyifu kwa madhumuni ya kibiashara kuachana na vitendo hivyo.

Iliongeza kuwa Watumiaji wa simu kwa matangazo (Telemarketers) wanadai kwa uwongo kwamba wanapata namba za simu za watumiaji kutoka kwa NCC na kwamba Tume iliwapa uwezo wa kupata namba hizo kupitia Hifadhi-data ya laini za simu ambayo, kulingana na NCC, sio kweli.

NCC imesema imedhamiria kuzingatia Kanuni na Sheria zinazoongoza Ulinzi wa Faragha kama haki ya watumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu na kwamba haijaidhinisha mtoa huduma au muuzaji simu kuvamia, kuvuna, au kutumia data ya mteja katika aina yoyote bila idhini ya wazi ya mtumiaji, isipokuwa vinginevyo kama isemavyo sheria

Sheria kwa Tanzania
Kupitia sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022 Kifungu cha 35 kinasema;

35.- (1) Mhusika wa taarifa, kwa kuzingatia utaratibu utakaoainishwa kwenye kanuni, anaweza kumtaka mkusanyaji kuacha kuchakata taarifa zake binafsi kwa madhumuni ya matangazo ya biashara.
(2) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (1), mhusika wa taarifa anaweza kuingia mkataba na mkusanyaji kwa madhumuni ya kutumia au kuchakata taarifa zake binafsi kwa ajili ya kunufaika kifedha.

(3) Katika kifungu hiki “matangazo ya biashara” yanajumuisha wasilisho, kwa namna yoyote, ya tangazo la kibiashara linaloelekezwa kwa mtu fulani.

1696423534836.png


Pamoja na Kifungu hicho matangazo ya Kampuni za simu yamezidi kila siku, yaani utatuma sms ya kuiondoa lakini wapi yatarudi. Uta-block namba lakini wapi matangazo hayakomi.
 
Hii sheria itaanza kutumika lini Tanzania? Maana tukisema ipo basi ni butu au haitumiki kampuni za simu zinatumia data zetu zinavyotaka.

Mbaya zaidi unatumiwa tangazo likifunguka unakatwa mb zako as if umepatana nao wakutumie!! Tupeni elimu ili tujue tunawafunguliaje madai.
 
Back
Top Bottom