Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,494
- 57,870
EPUKA UPOTOSHAJI MPYA WA WANA CCM
Amani iwe nanyi wadau
Leo napenda kuwaelimisha watanzania wenzangu juu ya upotoshaji mpya wa wana Ccm kwa watanzania. Ukipata ujumbe huu sambaza kwa mwingine kwa namna yeyote unayoweza, iwe Facebook, Twitter, Insta au Whatsup.
Kumetokea maneno kutoka kwa wana Ccm kuwakatisha tamaa watanzania wanaotaka mabadiliko kupitia Tundu Antiphas Lissu kuwa Eti wanasiasa hawawezi badirisha maisha yao ivyo wajikite tu kuchapa kazi!!
Watanzania wenzangu, ukisikia maneno hayo kutoka kwa mwana Ccm yeyote naomba umdharau kwa kiwango cha juu kabisa cha dharau kwa sababu Hii ni mbinu mpya wanayoitumia ili kuvunja morali ya watanzania kwenda kumpigia kura Tundu Antiphas Lissu na mwishowe kupata maendeleo ya kweli!
Ukweli ni kwamba, Siasa hasa namna ya kuchagua kiongozi awe yeyote ni lazima izingatiwe kwa namna ya kipekee kabisa na kila mwananchi, hii ni kwa sababu bila kufanya hivyo lazima utaathilika kwa namna moja au nyingine iwe unachapa kazi au huchapi kazi! Napenda kutoa mfano kwenye machache kama ifuatavyo;
1. Watanzania wote wachapa kazi wameathilika na mfumuko wa bei ya sukari kutoka shilingi 1800 kwa mwaka 2015 hadi shilingi 2800/3000 kwa mwaka huu. Hili limesababishwa na jambo moja tu la Magufuli kupiga marufuku uagizwaji wa sukari kutoka nje. Hivyo kutozingatia siasa kwa kigezo kuwa kiongozi hawezi badirisha maisha yako si kweli. Kila mwananchi anapaswa kuzingatia siasa
2. Wananchi wa mikoa ya Songwe, Rukwa, Katavi na Tabora pamoja na kuwa wachapakazi sana kwa kulima tumbaku, ila maamuzi ya serikali ya magufuli kuwazuia kuuza tumbaku zao kwa wafanyabiashara wanaowataka kwa bei wanayotaka wao imepelekea wawe masikini baada ya kulazimishwa kuuza tumbaku zao kwa vyama vya ushirika ambavyo vimenunua mazao yao kwa bei ya chini zaidi na kupelekea wao kuwa masikini. Hivyo kuchapa kazi hakujawasaidia, ni maamuzi ya mwanasiasa na serikali yake yaliyoharibu maisha yao.
3. Wananchi wa Mkoa wa Kagera, ambao walichapa sana kazi katika kuzalisha kahawa ila serikali ya magufuli ilikuja kuwazuia kuuza kahawa yao tena kwa bei ya faida nchini Uganda na wakalazimishwa kuuza kwa Chama cha ushirika kwa bei ya chini zaidi na ya hasara. Huu pia ni uthibitisho kuwa kutozingatia siasa au nani anakuwa kiongozi ni jambo la msingi sana ambalo linaweza badili maisha yako
4. Wafanyabiashara wengi ambao walikuwa ni wachapa kazi kweli , waliofungua biashara nyingi na kuajili watu wengi Ila wameathiliwa sana na Sera za serikali ya awamu ya tano za kutowajali wafanyabiashara na kuwasumbua kikodi hivyo kupelekea wengi kufunga biashara/ Makampuni yao
Mfano wa haya makampuni ni Rhino Cement.
5. Yapo mengi sana kuanzia wakulima wa Mbaazi, Korosho bila kusahau Mbao, Mchele na mazao mengi ambao wameathilika sana na maamuzi ya wanasiasa pamoja na kuwa wachapa kazi sana. Serikali ya awamu ya tano kupiga maarufu mazao kwenda nje kumeshusha sana bei ya Mchele, mahindi, mbao na kusababisha umasikini mkubwa sana kwa watanzania.
Ewe mtanzania, epuka sana huu upotoshaji wa wana Ccm unaolenga kukukatisha tamaa. Siasa na Aina ya kuongozi anaeongoza nchi ndo misingi Mikuu ya mustakabali wa maisha yako wewe na kizazi chako maana hata ukisema uchape kazi, Sera mbovu za kiongozi aliye madarakani lazima zitakuathili wewe, uzao wako na maisha yako kwa ujumla.
Ewe Mtanzania Chagua maendeleo ya kweli mwaka huu, Usiogope kufanya mabadiliko.
Chagua Tundu Antiphas Lissu awe Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025, Chagua wabunge na madiwani wa Chadema hapo Oktoba 28 mwaka huu.
Tanzania yenye maendeleo ya kweli ya watu na vitu inawezekana!
Usiacha kushare ujumbe huu!!
Lord denning.