The Hunter
JF-Expert Member
- Dec 25, 2010
- 1,049
- 307
Naamini u mzima, na najua huwa unapita hapa kama baadhi ya watendaji wako wanavyopita kwa majina bandia.
Mgomo wa madraktari ndo ushatangazwa naamini mkuu utaweka siasa na kiburi chako pembeni katika kutatua swala hili, japo ulijaribu kuwatuliza kwa maneno yaliyojaa siasa kwenye hotuba yako ya mwisho wa mwezi amini mkuu haijasaidia kitu, kwani makubaliano ilikuwa ni within a month baadhi ya matatizo yawe yameshatatuliwa, swala la kutangaza kwamba waziri mkuu ndo kapokea faili dakika za mwisho za mwezi huo mliokubaliana ni uthibitisho wa kwamba mliwadanganya madaktari, mlitumia siasa kukubaliana nao huku mkisahau mwezi mmoja ni siku thelathini tuu.
Chief najua wewe ni mbishi na utaacha madaktari wagome kwani wewe huumii kwa lolote, najua utataka kuweka muscle kidogo kwa kutishia kuwafuta kazi, mkuu Stuka maamuzi ya hovyo katika swala hili yatagharimu maisha ya wengi, yataibua migomo toka kada nyingine na amini nalokuhasa itakugharimu mkuu.
Enzi za bora liende zimekwisha, fanya kazi kama ulivyoomba wananchi wakuamini na kukupa madaraka.
Ikulu si mahali pa kupatia visa za kwenda kuzurura nje ya nchi kila kukicha, Ikulu ni nyumba inayokutanisha Pure cream and Think Tanks ya taifa.