ENZI ZILE (Tukumbushane)


Huna Laana Wewe, yaani nimecheka mpaka machozi :rofl:
 
Tasavali Pretty wengine majina kufanana, binafsi najijua sina kashfa hiyo ila wadau wengine wanaweza kuniungisha, lakini usitaje na ubini waweza vunja ndoa
 
Naona wengi mnaenda anga za mapenzi.Hakuna kumbukumbu nyingine?
Mie nakumbuka nilivyokuwa naiba migagi na wenzangu kwenye shamba la shule.


Wow umegusa upande mwingine!
Vipi mkipewa kazi ya kupanda shamba la shule..............shimo moja unarundika mbegu kibao ili umalize haraka!
 
Nakumbuka pia kulikuwa na viatu vya skuna na raba za losso ( la kuchumpa) we acha tu. vitabu vya panga la shaba na bulicheka pia mambo ya kuwekeana wanted halafu shule zikiwa zinafungwa si kuviziana. mwezio akikuchokoza mara muda wa kwenda nyumbani ni kupanda milimani kwenda kuonyeshana umwamba wa kupigana.
 
kuna siku tulikuwa tanatoka shule primary sasa njiani kuna dada mmoja alikuwa darasa la nyuma alikuwa anaharisha akaingia kichakani kujisaidia, watu tukamfuatilia (tulikuwa kama 10 hivi wale watukutu haswa) kufika yule demu akatustukia akatoka mbio tulimfukuza mpaka tukamshika sasa kuna mshikaji akamuuliza kwa nini unakunywa porini? basi yule dada huku analia akajibu tumbo la kuharisha linamsumbua tukamchukua mpaka ofisini kwa walimu kuwa tumemshika anakunya porini. Basi walimu wakamhoji walivyogundua kuwa anaumwa wakatoka wakatupigisha magoti huku tunita mvua tukaambiwa tusurudie tena
 
nimecheka sanaaaa. mie nakumbuka vijana wa enzi zetu walikuwa wanapenda kushika vititi vyetu yaani ukikutana nae popote ambapo hakuna mtu lazima ashike titi.
 
nimecheka sanaaaa. mie nakumbuka vijana wa enzi zetu walikuwa wanapenda kushika vititi vyetu yaani ukikutana nae popote ambapo hakuna mtu lazima ashike titi.
na kuna ile mtu anakutekenya kwa nyuma kwenye mbavu unaruka unaweza hata kuvunja dawati halafu tulikuwa tunahusisha na nyeg*
 
Halafu zikaja enzi zile za miaka ya 90 mwanzoni...enzi za Kriss Kross....ma jeans ya rangi rangi...ma jeans ya Karl Kani (nani anakumbuka hii clothing line?)....watu tulikuwa tunaenda pool side tumevalia wenyewe ma jeans ya mirangi rangi kibao...kijani..sijui nyekundu....na mabuti kama Naughty By Nature....aaah them good 'ol days

Nani anawakumbuka Kwanza Unit...kina Nigga One...Easy B (huyu alikuja kuwa teja), Rhymson...halafu kuna kajamaa kengine kadogo dogo hivi nimekasahau jina....

Nani anakumbuka wimbo wa Oyaa msela oyaaaa?
 
Kitu kingine nimekumbuka....mnakumbuka zamani kulikuwaga na malori yanapita mitaani yakiuza magunia ya mkaa? Basi wale wauza mkaa walikuwaga wanakaa nyuma kwenye magunia kule...basi hawa jamaa walikuwa kila wakipita mtaani lazima tuwazomee na kuwatania sana. Basi walikuwa hawapendi.....siku moja lori la mkaa likapita mtaani bana...basi mimi kujifanya mjanja si nikaanza kuwatania. Heheheheee siku hiyo wakaamua kunitolea uvivu bana...jamaa mmoja akanishukia akaanza kunikimbiza. Ebana nilitoka mkuku kaa nini unaambiwa huku nikipiga mayowe...baaaaba...baaaaba.....dah...yaaani nikikumbuka nacheka sana. Lakini uzuri hakunipata wala nini...nilimtimulia vumbi tu jamaa
 
Nyani ngabu umenikumbusha mbali sana mie nilikuwa nashinda Pool Side na sox langu kichwani jamaa wa Kwanza alikuwa anaitwa D Rob unawakumbuka kina Sindila, Othmani Njaidi, Ephraim Kibonde (4 Crews Flava), kuna demu mmoja alikuwa anavaa kama Ahaliyah. Enzi hizo tulikuwa tunaruka kwanja nyimbo za kina Daz Efx, Lords of Undergroung huku baadhi ya watu wamemzunguka Bony Luv wanamcheki anavyo scratch ma LP. Enzi zile wale kina Inspector walikuwa wadogo sana

Halafu ilikuwa DJ Charles akiingia kwenye mashine (na nyimbo za Boling za kina Awilo) watu tunaenda kugonga muhuri tunahamia Bilicanas
 
nimekumbuka yule dogo alikuwa naitwa Kubacha (KBC) alikuwa anachana mbaya, zile Karl Kani jeans nazikumbuka zilikuwa na mifuko mingi sana nakumbuka enzi zile nilikuwa nanunua jeans pale mitaa ya magomeni karibu na taa siku hizi kuna msikiti. Mnakumbuka Beach Party za Coco Beach nyimbo za Naughty na Kina Dr Dre zilikuwa zinapigwa kwa sanaa lol
 
Duh nakumbuka losso na raba mtoni shuleni kwetu ilikuwa watoto wa fulani wanavaa maana zilikuwa bei mbaya kipindi hicho.
 
hehhe hizi story za humu......mwaweza kufanya tudhaniwe wehu kwa kucheka na screen!
 
Enzi za kubandika jeans viraka vingi; ukikuta label sehemu unaikomba unaenda kuibandika kwenye Jeans

Nyani ngabu umenikumbusha mbali enzi za kuvuma kwa Naughty by Nature; miye ndo nilikuwa Treach wa shuleni kwetu (secondari) huko mkoani! teh teh basi style zote nazichukua Dar nikija likizo ili nikawakoge nirudipo teh teh; nilishapigwa na uncle baada ya kunifuma town nimepiga soksi na mnyororo mkubwa umepigwa kufuli ka mbwa teh teh teh yaani ukikiona kichwa changu hivi sasa ukaaambiwa hapa palikuwa panatoka Panki box la kufa mtu na way kama 2 hivi kwa mbele utalia kwa kucheka aaah we acha tu
 
Duuu!!!!!!!????????!!!!!!!!!Nakumbuka enzi zile zakidumu cha maji na ufagio mkononi,pia kumbuka Kibanga ampiga mkoloni,siku ya gulio katerero,,chilunda apambana na chui,ndoto za kimweri,pamela na kipini,kautipe na utumbo wa kuku,watoto wageuka mawe,sizitaki mbichi hizi,brown ashika tama, lindu amuokoa kapilima,pepe huna masikio,sisimizi shujaa,tembo na chura,chopeka na mnofu,tola alia gizani, manenge na mandawa,ulimbombo na ulindindi,juma na rosa. Hayo ni kwa wale tuliokua yunakula buluga na kubadilisha daftari bure kila linapoisha. Kweli ya kale Dhahabu
 

Mbavu sina mimi
 
mhh kweli kuna enzi na enzi...!! wakati wengine tunakumbuka enzi zile tunamfukuza mkoloni na Tanu.., wengine wanakumbuka enzi za kanda za VHS na Tape ambazo zikiisha unarewind na peni na kufanya recording unaweka redio mbili karibu..., wakati wengine wanakumbuka enzi za laizoni na bugaloo wengine wanakumbuka enzi za RTD na "Mama na Mwana"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…