Enzi zetu za shule

Duh kaazi kwer kwer Njenje wa Jitegemee, na Capt Ngajua enzi hizo ukikosa anakwambia "Shika Pu..u" kama adhabu, Wajadi na Sabini walikua wanatoa dozi ya viboko utafikiri walikua wanafanyiwa KPA ya kuchapa, ukisikia waitana Mjomba ujue balaa ndani ya class, Jitengeni Kihurio Mzee Zayumba na fegi zake RIP man
 
Akyanani hili neno...................KIPOLI......limenikumbusha mbali saaanaaaaa.........JAMANI SHULE KULIKUWA NA RAHAAAA SAAANAAAAA

'Kipoli' na 'Kipute'... duh...those days! Bweni la wasichana tulilibatiza jina 'sinza'. Nadhani kutokana na jinsi mapaa ya majengo yake yalivyokuwa (nyumba nyingi maeneo ya sinza (dsm) kipindi hicho yalikuwa na mapaa ya jinsi ile!)

Nakumbuka wimbo wetu wa shule ule ambao tulikuwa tukiuimba kwenye matukio makubwa kama 'school baraza' nk. Nakumbuka baadhi ya beti!

Ifuunda the glorious,
Technical school,
Live long forever,

With our motto, 'Skill and Efficiency'

And our school,
Shall shine forever more
Oooh, god bless our school

Ngalikihinja, kama unakumbuka maneno yote ya wimbo huu wa shule tafadhali nikumbushe!
 
Kwa wale tuliopita bweni hakuna harufu ilikuwa nzuri puani mwetu kama harufu ya bondo! Hakyanini utaomba kipindi kiishe!
 
Wewe chijana umenikumbusha mbaaliii!!!

Nimekumbuka sana maisha ya sekondari fulani ambapo tulikuwa na majina kibao kwa walimu wetu. Nakumbuka mwalimu mmoja tulimwita Kifaru na mke wake tukamwita Kidedea kwa jinsi miili yao ilivyokuwa mikubwa. Chakushangaza majina hayo walikuwa wanayafahamu. Watundu wachache wakambadilishia jina huyo mwalimu wa kiume nalo akalifahamu. Basi siku moja akajilipua morning assembly. Akasema, vijana kumezuka mtindo wa kupeana majina hapa shule. Mliniita Kifaru, nikakubali. Mke wangu mkamuita kidedea, nikakubali; sasa hili jina la popobawa litakwenda na mtu!!!
Basi alikuwa akipita karibu na mabweni ya wanafunzi watu wanaanza kuita kwa sauti POPOBAWA popobawa na asifanye kitu.
Baadaye alikuja mwalimu mkuu mmoja mkorofi sana, hakiyanani alinifanya nitoroke parade za asubuhi kwa jinsi alivyokuwa akiadhibu. Siku mmoja alimkoa jamaa wa nyuma yangu konzi zito ambalo lilihamishia maumivu kwangu na siku hiyo nikasoma kwa shida kwa ajili ya ule mlio. Huyo mzee nasikia alishafariki, kama kweli r.i.p Msasa. Huyo tulimwita Hitler na makamu wake alipewa jina la Natenyahu ambapo yeye wenyewe alikiri kapewa jina zuri.
Kuna jamaa lingine sijui mzima ama sio mzima, yeye alijiita UNYAMAUNYAMA maana ukiwa na soo nae mnamalizana kwa fimbo ama ngumi. Na hata ukimshinda hana kesi na wewe bali anajipanga upya. Hili jamaa lilikuwa linakuja kutuamsha saa 11 alfajiri kwamba tutoke kwenye magorofa ya serikali na kwenda kufanya usafi. Lilipenda kusema mkitaka raha jengeni zenu!!! Wanafunzi nao wanamtukana kuwa wenzake wamelala na wake zao yeye anakimbizana na wanafunzi kwa kuwa mke wake kipoli. Na yeye anajibu hata km kipoli mimi najali mchezo. It was real funny with those guys.

Mkuu..
Umenikumbusha huyu mwalimu mkuu wangu wa kwanza kule SabaSaba secondary Mtwara... Mgogo alikua bonge la baba halafu sisi tuko kama mbilikimo, alikuwa anapiga fimbo za juu ya mgongo hadi unatamani kuacha shule... sitasahau lile bango lake la swahili speakers...
Ila nasikia bado yuko hai anaishi maeneo ya Ukonga kule karibu na Hiltek bar
 
Hizo nicknames siku moja kidogo linitokee puani pale nilipodhani jina tajwa ni jina haswa la mwalimu.
Mimi nilichelewa ku-report shule na wakati nafika huyo mwalimu alishasema neno lililomfanya kubatizwa jina. Alikuwa akija darasani nasikia wenzangu wakisema mwalmu tabula-rasa amekuja. Kwa kweli sikujua maana ya neno hilo na huyo alikuwa mwalimu wangu wa darasa. Baadae nilitakiwa kumtafuta mwalimu huyo kwani ni mwalimu wangu wa darasa ili anisaidie kupata chumba cha kulala. Basi nikajitambulisha ofisini kuwa ni mwanafunzi wa kidato cha tano combination fulani na ninamtafuta mwalimu wa darasa kwa jina nimemsahau. Basi walimu wakajitahidi kuniambia jina lake na mimi nakataa kuwa sio huyo ninaemtafuta kwani nilisahau jina la tabularasa na jina lake sahihi sikulijua. Basi alipotokea nikasema namtafuta huyu na wao wakasema si ndo fulani tulikuwa tunakwambia? Nilishtuka lakini nikamezea na baadae nikawauliza wenzangu juuu ya tukio hilo.
Jamaa walinicheka sana na kunipa pole endapo kama ningekubulka jina hilo.

Wajameni hayo majina ni mazuri kama unajua mwanzo wake na maana yake.

Nimemkumbuka mwalimu mmoja mhaya aliyekuwa akifundisha shallow physics A-level. Mwalimu huyo alipewa jina la KIFUTU kwa ufupi wake na unene wake. Na zaidi ya hapo alikuwa mkali kweli kweli kila kesi anataka mwanafunzi aingie kwenye black book. Na akiwa anakucha analia sauti fulani.
 
Ifuunda the glorious,
Technical school,
Live long forever,

With our motto, 'Skill and Efficiency'

And our school,
Shall shine forever more
Oooh, god bless our school

Kwa kweli umenikumbusha mbali sana.

Wimbo wenyewe full ni huu hapa.

Ifuunda the glorious,
Technical school,
Live long forever x 2

With our motto, 'Skill and Efficiency'
We shall build, 'Our national strong'

And our school,
Shall shine forever more

Oooh, god bless our school x 2

Nawakumbuka sana wafuatao enzi zilee za mwishoni mwa miaka ya themanini na mwanzoni mwa tisini
1. Kinyakanyaka............ akianza kukuchapa fimbo anataja .....BLOOD KINYAKANYAKA
2. Mbungi wa umeme............ AKIKUKAMATA ALIKUWA ANASEMA...UNANILETEA MBINGI MIMI
3. Brigedia mwakalindile...........WIKI YA ZAMU YAKE ILIKUWA NI BALAA
4. Olu wa kiingereza
5. People ..........KILA BAADA YA NENO MOJA AU MAWILI LAZIMA ASEME ..... PEOPLE

Pia kulikuwa na "Per T T" yule mwalimu wa Physics ( Engineering Science) form I kila saa alikuwa anapenda kusema "per time what...?? part time taken, par t".
Huyu jamaa alikuwa anapenda totoz sana alikuwa anaramba wasichana wazuri wote wa form I.Wakishapanda madarasa hana habari nao anasubiri form I tena.

Duh kumbe IFUTESCO( Ifunda Tec Sec School) tupo wengi...

Nilikuwa bweni la Chabruma pale F5 na F6
 
Nipe nipe moto wayaka, washa washa washa x2
Doremidoo...........washa washa washa
 
mnanikumbusha neno " SHIKWAMBI" hili lilikuwa neno la kubuni tu pale Moshi Tech.

SHI - Shiba
KWA - Kwa
MBI - Mbinu.

Pia maneno kama TOP LAYER - Utando wa juu wa maharage yaliyoungwa kwa wese.
ZERO - kwenye mabweni ya wasichana

Kuna mwalimu wa Vijana - alikuwa hatari kwa super six akikukuta hujakimbia mchakamchaka soo lake afadhali ukamatwe umebaka - ni super six kila siku wiki nzima na adhabu kali ya kufukua visiki kule orchard (shamba la michungwa)
 
Pia kulikuwa na "Per T T" yule mwalimu wa Physics ( Engineering Science) form I kila saa alikuwa anapenda kusema "per time what...?? part time taken, par t".
Huyu jamaa alikuwa anapenda totoz sana alikuwa anaramba wasichana wazuri wote wa form I.Wakishapanda madarasa hana habari nao anasubiri form I tena.

Duh kumbe IFUTESCO( Ifunda Tec Sec School) tupo wengi...

Nilikuwa bweni la Chabruma pale F5 na F6
Mi nilikuwa form 1B (kwa mchili) and then group four niliishi D2 seuta mwanzo hadi namaliza............
 
Kuna mwingine pia alikonga roho zetu enzi hizo Mwl. Nyakunga; very senior citizen; mkereketwa wa footbal na chama chetu! Kipenzi cha wanafunzi! Akishika zamu watu wanawahi bila kusumbuana kwani wanajua wamalizapo kazi asubuhi mwal lazima toe dk 30 za footbal! Hata akisema anawattakeni 12 kamili watu walikuwanajitolea! cjui yupo hai huyu!

Sitasahau end of 1st quarter moja alisimama assembly hall na kwa kututahadharisha vijana wake na ukimwi alinza na maneno yafuatayo

"Vijana Chama na serikali vinasisitiza; wakati huu ni wakati wa ULANZI! kaweni makini huko majumbani; sitapenda kuhudhuria msiba wa yeyote kati yenu kwa sababu ya ulanzi!" ilikuwa ni masika na ndio ile made in Tanangozi ilikuwa ni kwa wingi sana mjini Iringa!
 
Lol!...kwa ma-veterans wa Ifunda salute kwenu!
Ile shule ilkuwa ni KAMBI ndogo ya JESHI?, form two's walikuwa na uwezo wa kufunga bweni moja na kuwatembezea kichapo wote, forget about form one ambao walikuwa ni zaidi ya watumwa!

BTW: Per T T ni marehemu sasa, Ukimwi umeua /unaua sana walimu wetu aisee!, huyu alikuwa ukiwa na soo naye sepa halafu bdae ukiridu msifie kwa hasira zake, 'kuwa mwl ungeniua pale thats y nikakimbia, ww ni noma mwl, lazma alegee, au mmtume demu akajieleze lazma atawapotezea..lol!'...
 
BTW: Per T T ni marehemu sasa, Ukimwi umeua /unaua sana walimu wetu aisee!,

Its so sad. Amefariki lini? Nakumbuka niliwahi kukutana nae hapo baraza la mitihani (nadhani mwaka 2004 hivi).

Ni kweli walimu wengi wameshawahi mbele ya haki kwa hili gonjwa wangali bado vijana.
 
Its so sad. Amefariki lini? Nakumbuka niliwahi kukutana nae hapo baraza la mitihani (nadhani mwaka 2004 hivi).

Ni kweli walimu wengi wameshawahi mbele ya haki kwa hili gonjwa wangali bado vijana.

Sijui/sikumbuki mwaka exactly, lakini ni baada ya 2004. B4 that tulikuwa naye pale...RIP Pe T T!
 
Nakumbuka wakati nasoma Makongo High School miaka ya mwanzoni mwa 2000 form six kulikuwa na mwl anaitwa Gwimile a.k.a Gwimz,huyu mwalimu alikuwa na mdomo mkubwa(lips) na kuna wakati aliomba apewe ofa ya soda darasani huku akiendelea kufundisha somo la History A-Level.Akinywa tu soda utatamani kuiokoa chupa maana pale penye tundu la chupa limefunikwa kabisa na lips zake maana huoni kitu pale.

Kuna mwalimu mmoja alitufundisha somo la GS,alikuwa anaitwa Luteni mstaafu Kalokola,tulimpachika kwa jina la Be flexible maana alikuwa anapenda sana kulitaja hilo neno mara kwa mara.

Makongo mpooooo!
 
Lol!...kwa ma-veterans wa Ifunda salute kwenu!
Ile shule ilkuwa ni KAMBI ndogo ya JESHI?, form two's walikuwa na uwezo wa kufunga bweni moja na kuwatembezea kichapo wote, forget about form one ambao walikuwa ni zaidi ya watumwa!

BTW: Per T T ni marehemu sasa, Ukimwi umeua /unaua sana walimu wetu aisee!, huyu alikuwa ukiwa na soo naye sepa halafu bdae ukiridu msifie kwa hasira zake, 'kuwa mwl ungeniua pale thats y nikakimbia, ww ni noma mwl, lazma alegee, au mmtume demu akajieleze lazma atawapotezea..lol!'...

Duh..!! aisee this is a real sad news..its even worse bcoz jamaa alikuwa anakula wanafunzi kwa vitisho and taking advantage ya ugeni wao shuleni.

Naona kamfuata rafiki yake Mwalimu Masala ambaye alitangulia mbele ya haki mapema sana kwa gonjwa hili hili. Hali ni mbaya sana pale, ule ni mji mdogo na ni rahisi sana watu zaidi ya mmoja kutembea na mtu mmoja.

Tuombe mungu.
 
mie namkumbuka mwalimu mmoja aliitwa askofu na yeye akalikubali kutokana na kupenda usafi kwenye bweni lake....
 
Wewe chijana umenikumbusha mbaaliii!!!

Nimekumbuka sana maisha ya sekondari fulani ambapo tulikuwa na majina kibao kwa walimu wetu. Nakumbuka mwalimu mmoja tulimwita Kifaru na mke wake tukamwita Kidedea kwa jinsi miili yao ilivyokuwa mikubwa. Chakushangaza majina hayo walikuwa wanayafahamu. Watundu wachache wakambadilishia jina huyo mwalimu wa kiume nalo akalifahamu. Basi siku moja akajilipua morning assembly. Akasema, vijana kumezuka mtindo wa kupeana majina hapa shule. Mliniita Kifaru, nikakubali. Mke wangu mkamuita kidedea, nikakubali; sasa hili jina la popobawa litakwenda na mtu!!!
Basi alikuwa akipita karibu na mabweni ya wanafunzi watu wanaanza kuita kwa sauti POPOBAWA popobawa na asifanye kitu.
Baadaye alikuja mwalimu mkuu mmoja mkorofi sana, hakiyanani alinifanya nitoroke parade za asubuhi kwa jinsi alivyokuwa akiadhibu. Siku mmoja alimkoa jamaa wa nyuma yangu konzi zito ambalo lilihamishia maumivu kwangu na siku hiyo nikasoma kwa shida kwa ajili ya ule mlio. Huyo mzee nasikia alishafariki, kama kweli r.i.p Msasa. Huyo tulimwita Hitler na makamu wake alipewa jina la Natenyahu ambapo yeye wenyewe alikiri kapewa jina zuri.

Kuna jamaa lingine sijui mzima ama sio mzima, yeye alijiita UNYAMAUNYAMA maana ukiwa na soo nae mnamalizana kwa fimbo ama ngumi. Na hata ukimshinda hana kesi na wewe bali anajipanga upya. Hili jamaa lilikuwa linakuja kutuamsha saa 11 alfajiri kwamba tutoke kwenye magorofa ya serikali na kwenda kufanya usafi. Lilipenda kusema mkitaka raha jengeni zenu!!! Wanafunzi nao wanamtukana kuwa wenzake wamelala na wake zao yeye anakimbizana na wanafunzi kwa kuwa mke wake kipoli. Na yeye anajibu hata km kipoli mimi najali mchezo. It was real funny with those guys.

Hii imekaa kama Mazengo vile. Bweni chafu la Ujamaa ndiyo walikuwa na tabia ya kufukuzana na mwalimu na kusema tuko huku.......

Msasa alinifundisha biology. Darasani hapigi ila acha atoke nje...... Mgogo huyu bwana. Mie nilimkuta akiwa ndiyo Sec masters. Kabla yake tuliambiwa alikuwepo Dudu. Mmasai yule vyoo vyote walikuwa wameandika Dudu Ku******.

Kipoli, Gima, nyuka, Kikuyu na Vikuyu, nguruwe wa mwezi wa 7 na wa kwanza.
 
mnanikumbusha neno " SHIKWAMBI" hili lilikuwa neno la kubuni tu pale Moshi Tech.

SHI - Shiba
KWA - Kwa
MBI - Mbinu.

Pia maneno kama TOP LAYER - Utando wa juu wa maharage yaliyoungwa kwa wese.
ZERO - kwenye mabweni ya wasichana

Kuna mwalimu wa Vijana - alikuwa hatari kwa super six akikukuta hujakimbia mchakamchaka soo lake afadhali ukamatwe umebaka - ni super six kila siku wiki nzima na adhabu kali ya kufukua visiki kule orchard (shamba la michungwa)

Pia yapo Shiba kwa jasho.

Nakumbuka masanduku yameandikwa SUMATA yaani sukuma maisha taratibu.
 
Back
Top Bottom