Enzi za utoto!!! Tukumbushane

PATIENCE PB

Senior Member
Apr 3, 2014
163
37
Tulipokuwa Wadogo,ukienda Kucheza Mbali Na Nyumbani Kidogo Hasa Hasa Mpira Wa Miguu, Mtaa Kwa Mtaa.Ukichelewa Kurudi Nyumbani Tayari Jua Limekwishazama,hapa Kuna Ka-jua Fulani Ka Mwisho Mwisho Hivi Kalikuwa Kanatudanganya Wengi,yani Jua Kama Linachomoza Hivi Kumbe Ndo Linazama,si Tulikuwa Tunaita Haka Ka-jua Ka Mwisho "akalemba-bazane" Yaani Ka-natudanganya Sisi Wachezaji. Basi Ndo Ka-giza Kashaingia Ukifika Home Tu,swali La Kwanza Kwa "Beki Tatu" kama wengi mlivyozoea kuwaita, unauliza " Vp Mshua Yupo?" "Ameshaniulizia?" Jibu Unalopewa "kakuulizia Mara Kibao Na Kakata Viboko Vipo Chini Ya Kabati" basi kwa jibu hilo moyo unaenda kwa mapigo ya mwendokasi kwa uwoga.
Basi Unachukua ki-mjani Fulani Hivi(nimesahau jina lake,kwa anayekumbuka anikumbushe) unaweka mdomoni chini ya ulimi kama ugoro ili Baba yako asikupige.
Baada Ya Chakula Cha Usiku,unachezea Stick Za Kutosha Kisa Umekuja Nyumbani Saa 12 Na Nusu Jioni ,afu Unaenda Kulala.
BASED ON TRUE STORY
WATOTO WA SIKU HIZI hivi vitu hawajui
 
Enzi za utoto mgeni akija home basi sifa zinaongezeka. Unajiona much-know mara unapanda kwenye makochi hapo maza anakuangalia tu, ngoja sasa mgeni aondoke hapo unachezea stick ujanja wote kwisha!!!
 
Enzi za utoto unamendea soda ya menlo anakumiminia maza anakusikilizia after mgeni kuondoka unakula njukuti za kutoshaaa
 
Back
Top Bottom