Ivi uyo Dogo kwa nn alikua anavaa ndala mkononi,lol
Akiona kazidiwa ngumi kazi ni kutoka mbio kali mno bila kupata tabu ya kutafuta ndala zilipo
Nimeipenda hii ya harusi, bwana harusi kama amesahau bibi harusi😀
1. Nilikuwa nakimbia kuoga kwa bahati mbaya walikuwa hawaniwezi kwenye mbio hadi leo sio mpenzi sana wa bafu.
2. Nilikuwa namalizia vitone vya bia za mzee. Sitaki kuwaambia sikuiz nipoje.

hahahaaaa,,, yaap alkua akitokea mjanja lazima awalize kwanza kabl hamjastuka…!!Alikuja binamu yetu wakati huo akisoma Uyole basi mahindi ya kuchoma alikua anasema anatutafutia njia, ukushtuka ameshakula nusu ya hindi.
Alikuja binamu yetu wakati huo akisoma Uyole basi mahindi ya kuchoma alikua anasema anatutafutia njia, ukushtuka ameshakula nusu ya hindi.
Nimecheka!Nakumbuka enzi hizo watoto cku moja ucku baba alirud ucku akatuletea keki sasa kaka mkubwa nd akapewa kugawa,, yey ikabdi abuni utaratibu eti tufany kama wakristu wanavoend kupokea mwil wa kristu (mkate kanisani)
Sasa ikabd tujipang mstari tulkua km watatu na yy kaka wa nne,, alichokifany kaka akazima kibatari tukawa tunaenda kupokea gizani,, badala ya kutupa keki tulizonunuliw yeye akaanz kukata ugal uliobaki ucku nd anatugawia alafu yeye keki anakla, tulipokuj kustuka huo ugomvi mzee ndio alkuj kuuamua,, siwez kusaau ,utoto raha sanaa…!!
Utundu wa kucheza kwenye miti siku nikiwa na bro na marafiki wa jirani si tulivamia majani ya upupu, tuliwashwa htr hata ukioga muwasho hautoki, watoto wa sikuizi hawakumbani na hizo rabshaHabari wa kuu.
J3 ndio inaishia hivyo,hatuna budi kurelax kidogo wakati tukiisubiria j4.
Jioni ya leo nimejikuta nakumbuka maisha yangu ya utotoni na vituko vyote nilivyopitia kwa kadri nilivyoweza kukumbuka. Katika matukio mawili niliyoweza kuyakumbuka,ni mawili ndio yamenigusa na kunikumbusha mbali.
La kwanza nakumbuka tulikuwa tunacheza kwenye migomba kwa masaa mengi na watoto wenzangu,katika mkungu wa ndizi kuna kile kikonyo mwishoni kabisa,hicho ndio nilikuwa nakichezea,nakichanua kuangalia vindizi vidogo vilivyokuwa ndani. Sasa mida ya mchana nilipoitwa kula,nilinawa mikono ila ule utomvu haukuisha. Kila nikila chakula kwangu ladha ilikuwa chungu,mwanzoni nilivumilia ila badae ikabidi niulize "Hivi ladha ya chakula mnaionaje? Mbona upande wangu kichungu?"
Mama ndio alikuja kunifumbulia fumbo lile,hapo msosi ndio ukaanza kushuka vizuri.
Kisa cha pili kwenye kucheza kombolela na wenzangu,niliokota kichupa flani hivi cha rangi ya silva. Kutokana na udadisi,nilihangaika sana kukifungua. Nilikiponda sana na jiwe pamoja na chuma,hatimae kikafunguka. Nakumbuka kwenye kuta za ndani kilikuwa na unga unga mweusi,hakukuwa na kitu kingine zaidi. Nilikinusa ili kujua harufu yake. Ilo lilikuwa kosa,mwili ulianza kuishiwa nguvu taratibu. Nikakitupa na kurudi home. Hali ilizidi kuwa mbaya,ikabidi Baba akakitafute kile kichupa then nkapelekwa nacho hospitali kupata matibabu. Nilipona,ila sitosahau.
Wewe mwana JF mwenzangu unakumbuka nini??
Share your childhood experiences with us.
HahahaaaaaaaaaBro ameshantafutia sana njia ya kwenda kwa babu songea, mi nachekelea tu sijui kinachoendelea. Laah mpaka leo ukiniambia niende sifiki
Hahaa,, unakuta hindi zima halijapukuchuliwa sasa yy anafany kupukuchua mstari m1 au miwili ili kumrahisishia anayekula kweny kupukuchua…!!Anataftia vipi njia kwa kutumia mahindi?
Hahahaaa,,, mimi pia iliwahi tokea hiyo kweny mock ya la saba ,kuna madada walkua na possible sas wakawa wanaziandika kwenye mapaja na sisi wavulan tulipojua,, bila ajizi ikabd tuwe tunawafunua mapaja kila siku ili tujue kama wana possibl but in real sense ilkua ni kuwachungulia tuu……!!Loohh kuna kituko kimoja wkt tupo kidato cha nne.
Paper ya historia ilifanyika mchana, basi binti mmoja ile anaingia viunga vya shule tuu anaambiwa kuna feki umelipata. Binti kapaniki sijalipata. Yule kijana akampa point za feki.
Binti akamwambia andika paja LA kushoto na Mimi na andika kwenye paja la kulia.
Binti bize anamaliza yule kijana hata point za swali moja bado.
Akamuuliza mbona hujaandika wewe vipi? Kijana mapaja yako laini sana nimeshindwa kuandika
Kuingia kwenye paper likawa feki kweli kweli.
Skikua kabonge lakini nilikuwa sakala sana, uzuri wangu kwenye kuongea na nguvu sina, kila msuto ulinihusu.
duh!!!!huu Uzi umenifanya nikumbuke ya zamani Sana.Nilikuwa na tabia hiyo pia ndugu. Nilikuwa mbea balaa na lakini matukio ya kusutwa sio mengi na nilikuwa nikisutwa hata sisemi kitu nakuwa mdogo ukiniweka kwenye piriton miguu haifiki chini.


it's my living memory jamani,sitasahau yaani