Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,624
- 47,250
Habari wa kuu.
J3 ndio inaishia hivyo,hatuna budi kurelax kidogo wakati tukiisubiria j4.
Jioni ya leo nimejikuta nakumbuka maisha yangu ya utotoni na vituko vyote nilivyopitia kwa kadri nilivyoweza kukumbuka. Katika matukio mawili niliyoweza kuyakumbuka,ni mawili ndio yamenigusa na kunikumbusha mbali.
La kwanza nakumbuka tulikuwa tunacheza kwenye migomba kwa masaa mengi na watoto wenzangu,katika mkungu wa ndizi kuna kile kikonyo mwishoni kabisa,hicho ndio nilikuwa nakichezea,nakichanua kuangalia vindizi vidogo vilivyokuwa ndani. Sasa mida ya mchana nilipoitwa kula,nilinawa mikono ila ule utomvu haukuisha. Kila nikila chakula kwangu ladha ilikuwa chungu,mwanzoni nilivumilia ila badae ikabidi niulize "Hivi ladha ya chakula mnaionaje? Mbona upande wangu kichungu?"
Mama ndio alikuja kunifumbulia fumbo lile,hapo msosi ndio ukaanza kushuka vizuri.
Kisa cha pili kwenye kucheza kombolela na wenzangu,niliokota kichupa flani hivi cha rangi ya silva. Kutokana na udadisi,nilihangaika sana kukifungua. Nilikiponda sana na jiwe pamoja na chuma,hatimae kikafunguka. Nakumbuka kwenye kuta za ndani kilikuwa na unga unga mweusi,hakukuwa na kitu kingine zaidi. Nilikinusa ili kujua harufu yake. Ilo lilikuwa kosa,mwili ulianza kuishiwa nguvu taratibu. Nikakitupa na kurudi home. Hali ilizidi kuwa mbaya,ikabidi Baba akakitafute kile kichupa then nkapelekwa nacho hospitali kupata matibabu. Nilipona,ila sitosahau.
Wewe mwana JF mwenzangu unakumbuka nini??
Share your childhood experiences with us.