Enzi za utoto: Funny life experieces

Enzi za utoto: Funny life experieces

Nikiwa primary ndondo lilikuwa halipandi fresh. Yani wakipika ugali maharage ndio kabisaa hamu ya kula inakata.

Nikaja nikagundua kamchezo kakuweka sukari kwenye maharage. Nikitoka skul nachanganya sukari na maharage then ndio nakula. Sasa kuna siku nikiwa nishachanganya sukari na maharage,kumbe beki tatu alisahau kutenga mboga ya ucku. Kuja kucheki anakuta nimechota maharage mengi. Akanimind alaf akachukua bakuli yangu akaenda kupunguzia kwenye sufuria.

Kimbembe ilikuwa usiku wakati wa kula,dingi kamind kwenye chakula kuna sukari. Beki 3 anakataa anasema mchana walikula fresh tu jioni kafanya kuipasha tu hajaongeza kitu. Badae yule beki 3 alikuja kuusoma mchezo akanichoma pale pale. Uzuri wa dingi hanaga michongo ya kalete bakora,yeye huwa anatoa makofi kadhaa ya ghafla alafu shughuli zinaendelea
 
Nakumbuka marehemu mama yangu, alikuwa mtu wa ngwasuma balaa, yaani ukiharibu mambo utamtambua vizuri.


Siku hiyo tuko kondeni tunachunga ng'ombe, mimi na ndugu wengine wa ukoo wetu lika langu.mimi niko mbali nao kidogo(siko eneo moja na wao), kumbe kule waliko wamefumwa na afisa mtendaji wa kijiji wana najisi ng'ombe chini ya mti.kawazingua na makwenzi mawili matatu harafu akaondoka.

Nawakuta jamaa zangu wakanipa mkasa wakidhani yameishia pale.sasa muda wa kurudi nyumbani naingia tu nyumbani na deko kwa maza, namkuta afisa kakaa na maza anampa mkanda, dah.

Naingia tu maza akaninyaka fasta, afisa akaingilia kati kwamba huyu hakuwepo, walikuwa ni wenzi
e.nikasamehewa ile natoka mlangoni napishanana na mzee niliyemtukana siku mbili nyuma.

Nilihisi nina mkosi sana siku ile maana nilipigwa sana.
Hahaha dah kweli siku hiyo ilipangwa upigwe tu.
 
Duh!!! ninaKumbuka nilikuwa naogopa sana sindano enzi ya utoto wangu.
Nilikuwa na tabia ya kuweka maji kwenye kikombe then nina yaficha upande wa chini ndani ya freezer. Yanaganda na kuwa barafu kabisa,Nina ya gonga gonga na kuyala huku Nina yatafuna,Hata maziwa nikipewa nilikuwa nakunywa nusu na nusu nilikuwa nafanya upuuzi huo.

Baada ya muda,Nikaanza kusikia koo linaniuma nikimeza mate. Mama yangu alikuwa nesi,nikaawa najua kidoho kuhusi panadol inatuliza maumivu nikawa nakunywa dawa hizp kwa siri na kupata nafuu. After a week Kaanza kusikia natoa harufu mbaya nikiongea,nakumbuka Mara nyingi akawa ananiulza umepiga mswaki Leo?,najibu Ndio.

Baada ya muda akaanza kunikagua kinywa,akagundua Nina tatzo akaniuliza unakunywa maji ya baridi,nikakataa. Wakati Huo sijastop ile tabia ya kugandisha maji na panadol zangu. Mama akaanza kunichunguza,nikawa sometimes siyakuti maji yangu niliyoweka na kwasababu ya akili za utoto sikuwa najiuliza nikawa narudia kuyaweka nakuta yametolewa mpaka usiku Naenda kulala sipati barafu zangu.

Siku moja toka agundue Nina nini mdomo alanifuata shuleni tukaenda hospital,nikasikia neno injection,nikamuuliza mama mnanichoma sindano mama akasema NO, sio za kwako. Baadae akaniambia twende huku,nikisoma kibao cha mlangoni naona chumba cha sindani,nilikimbia kurudi nyumbani. Walinitafuta sana mlinzi aka confirm nilitoka nakimbia,mama akanigombeza sana. Alivyorudi nyumbani. Usiku nimelala alinichoma sindano nikaanza kulia usiku tena kwa nguvu sana. Sitokuja kusahau,na iliendelea kuchomana sindano usingizini mpaka zilipoisha. Nikawa asubuhi nagoma kwenda shule eti sindano zinauma it's my living memory jamani,sitasahau yaani
kulikuwa na hii kitu inaitwa Crystapen (benzylpenicillin) ni hatari kubwa
 
Chandimu

Mchezo wa kutekana (nakumbuka tushawahi teka mtoto wa mtu Siku nzima tukamuachia usiku sana)

Sigara za majani ya mpapai, tunanyongea kwenye jani la muhindi... Baadae nikaanza na vishungi vya Dingi.. Baadae nikaanza kununua za kwangu

Kuogelea.. Hapa ndo palikua patamu, ukiingia mtoni (mto nakasanga) nje wahuni wanaficha nguo zako

Kibaba baba.. Huku ndo watu tumejifunza kutongoza..

Daaah... A lot of memories mazee
 
Kwenye bafu ilikua shughuli, nakumbuka siku moja nimeoga nikamaliza nakupaka mafuta nikarudi tena kuoga nikasema naoga na ya kesho.
 
Sio Botswana bana

Thats Setwana, inaongelewa Lesotho, Gauteng Province (southa africa) ambayo ina Pretoria, Jos, bluefontain, mafikeng, kishwa Botswana yote,
Dumela mma maana yake hujambo mama?

Lerato maana yake ni mapendo/ mapenzi/ upendo nk inategemea na sentensi
 
Thats Setwana, inaongelewa Lesotho, Gauteng Province (southa africa) ambayo ina Pretoria, Jos, bluefontain, mafikeng, kishwa Botswana yote,
Dumela mma maana yake hujambo mama?

Lerato maana yake ni mapendo/ mapenzi/ upendo nk inategemea na sentensi
asanteeeee kwa kulijua hili. I was in love na hili jina na lingine Lindiwe.
 
Nilidabwa na Bibi naxhuxha mistari kwa lea yan niliondoka kimya kimya kama nimemwagiwa maji
 
Utoto raha sana. Nikikaa nikikumbuka mara nyingi nabaki natabasamu 🙂🙂
 
Shukran BAK kwa kucheka,kicheko ni afya.
16122422_1784621171860477_3113117601811660800_n.jpg

Sijui huyu busara Numbisa anazipata wapi hizi picha zinachekesha sana lol!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom