Chimunguru
JF-Expert Member
- May 3, 2009
- 10,678
- 4,378
kwanza mdingi kanipeleka akaniacha na shs 200 hiyo ilikuwa 1989 dah kumwambia naogopa anasema si mnakula bure!
Hapo mkuu sina swali hahahaha lakini uchumi bado ulikuwa imara siku hizo
msosi wenyewe sasa ni dona na dagaa always, ule ugali uliitwa makana. dagaa hakuna kuchambua linafunguliwa gunia nusu linamwagiwa kwenye pipa la kupikia wakiiva wakati wa kula mnakutana na zile shells za konokono mchizi unatupa tu huko unaendelea kumanga.
Dah!mlikua makauzu zaidi ya dagaa!enzi hzo ndan ya ikizu.kipindi cha kiangaz maji yalikuwa ya shida sana.ikawa tunaoga mtoni,kwa kuwa hatukuwa na taulo tunatembea naked kuelekea skonga ili mkaukie njian mvae nguo hii ndiyo ilikuwa tabia.day moja tukiwa kama ppipo kumi na tana tuko naked tume tumejipanga njiani tumetoka kuoga na kufua mton kama kawa tukakutana na akinamama nao wanaelekea mtoni wako na watoto wao wa kike na kiume,hakuna aliyepisha njia walivyoona tuko naked halafu hatupishi njia wakakimbia.
Ahahahaaah!! Hii ni kali aisee...enzi hzo ndan ya ikizu.kipindi cha kiangaz maji yalikuwa ya shida sana.ikawa tunaoga mtoni,kwa kuwa hatukuwa na taulo tunatembea naked kuelekea skonga ili mkaukie njian mvae nguo hii ndiyo ilikuwa tabia.day moja tukiwa kama ppipo kumi na tana tuko naked tume tumejipanga njiani tumetoka kuoga na kufua mton kama kawa tukakutana na akinamama nao wanaelekea mtoni wako na watoto wao wa kike na kiume,hakuna aliyepisha njia walivyoona tuko naked halafu hatupishi njia wakakimbia.
Ahahahahaaah!! Wapi huko?Ebwana nimekumbuka, form one tulikuwa tunalala wa mwisho, ukifika muda wa kulala form one mnaanza kuimba wimbo wa Taifa huku unamshushia jamaa neti kama vile bendera.
Mi nakumbuka pale kibaha sec alikuwepo kiranja wa msosi mnoko na mbabe balaa.Alikuwa akikufuma unavusha msosi atakufukuza,atakukamata na kumwaga msosi wote kisha unapewa adhabu ya kudeki jikoni.Kuna siku kwa makusudi nilitoka na ki-sadolin kitupu chenye mfuniko nikajifanya navusha msosi mbele yake.Tulifukuzana umbali mrefu mpaka uwanja wa shule ndo akanikamata.Alipogundua chombo changu hakina msosi alimaindi ile mbaya,mi niliamua kumchosha tu!
Tehe tehe heeeh!! Ulimkomoa kwa kweli...Mi nakumbuka pale kibaha sec alikuwepo kiranja wa msosi mnoko na mbabe balaa.Alikuwa akikufuma unavusha msosi atakufukuza,atakukamata na kumwaga msosi wote kisha unapewa adhabu ya kudeki jikoni.Kuna siku kwa makusudi nilitoka na ki-sadolin kitupu chenye mfuniko nikajifanya navusha msosi mbele yake.Tulifukuzana umbali mrefu mpaka uwanja wa shule ndo akanikamata.Alipogundua chombo changu hakina msosi alimaindi ile mbaya,mi niliamua kumchosha tu!
Me niliambiwa nenda bweni(jina kapuni) ukwamuulizie jamaa anaitwa Bunsen burner!!! LOH! Nilipofika hapo bwenini jamaa wanistukia kuwa
nimeingizwa mkenge nao wakanambia ametoka nimsubiri kama dakika sita hivi atarudi!! ndugu niliuza chai mpaka nikakoma, baadae ndo
wakanielewesha.. nilimind we acha tu.
Nyegezi seminary pale..kulikua na ticha mmoja kwa jina la Pasu..kwavile alikua anapenda msosi huyo kiasi kwamba alikua anataka kwenda pasu kwa pasu na wanafunzi haswa siku za wali kwa nyama au siku za sikukuu...basi siku moja alinikamata nimetoka kuvusha wali jikoni (baada ya kucheza deal na mpishi) kabla ya muda, akataka niende nae pasu..nikagoma. Kwa vile mwalimu Pasu pia alikua mpenda sifa, eti akataka mimi na sufuria langu la kichele twende kwa mkuu wa seminari (rector) ili nikajishitaki, hapo tifu likatoke, nikamkunja shati, kumtupia sufuria na kutokomea....ila usiku nikapata bakora za kutosha kutoka kwa rector!!!
maisha ya boarding kwa kweli yalikua si mchezo.
Ha ha ha ha haaaah!!! Pole sana mkuu!Boarding, Musoma Alliance au Tec, nakumbuka Deputy HM Fundisha, alilkuta tunaoga wakati wa pared akatunyanganya nguo kisha akaanza kutuchana stick, mimi nilikimbilia upande wa Musoma mjini na wenzangu wakaelekea Mutex, jamaa lilinichagua mimi na kunifukuza hadi barabarani wakuu. Takribani 1.2 km huku watu wanashangilia kwa kuniona niko uchi. Sitasahau, kurudi ilikuwa issue. Afu jamaa halikumind tena
<br />IFUNDA TECH huko nako balaaa nakumbuka POLI/MSITU ambapo watu waliamishia madawati huko, tifu lilikuwa pale wanakijiji wanapochoma moto misitu mara SAA 9 USIKU Mnasikia king'ora cha shule kwenda kuzimaa motoooooooooo nyooo