Leonard Robert
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 11,138
- 7,398
Yule mama kauzu kweli, siku moja alinikuta nafagia nyuma ya bweni la sina acha anizodoe,'lione form five lizima halijui kufagia' nami nikamjibu nilikotoka kulikuwa na wafanyakazi wa shule ndo walikuwa wanafagia, halafu yule mama hawapendi a-level hasa form five mara atawambia 'yaone yanazuzuka na maghorofa' wakati maghorofa yenyewe magofu sijui sahivi kama yashafanyiwa ukarafati.ahahahahah....enzi hizo Tabora boyz..kulikuwa na chemba moja katika bweni la mkwawa inaitwa university..mle tulikuwa tunalala pipo kama kumi na moja hivi tukiwemo viongozi..mke wa headmasta jina la utan nyumelo alikuwa na tabia ya kuja kutuamsha asubuh na mapema mabwenini..siku hiyo kaja kakuta pipo zote zimelala naked chemban coz tulipanga tumkomoe...ahahah yule mama eti akasema wala hatishiki coz keshaona kubwa zaidi ya zetu..mwee..but atleast alipunguza kuja akawa anaishia bweni kuu...vituko vya mesini hasa siku za nyali aka ubwabwa we acha tu..
Nakumbuka wakati nipo form 2 tulikua na tabia ya kuwatesa,kuwasumbua na kuwanyayasa form 1 ili kulipiza yale yaliyotukuta b4,kulikua na dogo wa form 1 mbishi kichizi kiasi kwamba alikua hapendwi na kila m2 aliyemzidi kidato.kwa hiyo kukawa na kampeni ya kumuadhibu,mara kitanda chake kime mwagiwa maji,kimepakwa upupu,wa2 wanakata godoro kusafishia viatu,kuchambia nk.Ikabidi aombe uhamisho lakini kabla ya kuondoka alitaka kulipa kisasi.Basi usiku watu tumetoka prepo genereta limezimwa watu tumelala halfu mvua inayesha tukasikia m2 anapiga kelele za moto,moto,moto.utaratibu ulikua ukishasikia hiyo mbiu toka fasta bwenini,watu na mabegi yetu,magodoro,mizinga tukatoa kwa kasi kuviokoa kwa moto halaf baada ya muda tukakuta kimyaaa wala hatuoni moto wala moshi.Ikabidi tufuatilie chanzo cha hiyo sauti, tukamkuata yule dogo amewka headphone masikioni,walkman mfukoni anayarudi mangoma ya kiafrica (africa moto,moto,afrika moto).tulitaka kumtembezea kipigo lakini bahati yake patroni alikua on time.Ila sita msahau
hahaaaa! siku hiyo sasa ndani ya MALANGALI HIGH SCHOOL! kitu cha wali nyama ilikua mara mojamoja kchizi, jamaangu akadokoa nyama katika sahani ya mwenzake. yule mshikaji ambae nya ilidokolewa kutok sahani yake akaachia sahani yopte ya wali na nyama zilizobaki ikadondoka chini eti kisa anangangania ile nyama moja iliyo dokolewa...........!
Wazee wa mazengo Mpoooo? Kwa Kweka usiombe, Nilikuwa nakaa lile Bweni la Askofu, na yule mwalimu mwingine, yeye alikuwa anafundisha olevel Kithungu ilikuwa zero, sasa akawa anatoa Speech of a day...." Dear students, we intruce to you a new timetable of Makande, chew it then tell us" akimaanisha kaeni muijadili halafu tuambieni kama inafaa..alikuwa anafundisha drawing, akiwa na kitu cha kuchora, anavizia madent wakiwa hawaangalii then anachora faster kinoma, then anatambaa zake kama vipi madent ndo waende kuomba wachore.....Jina simkumbuki...headmaster yeye, ngoma iliwatuma madent kwenda kuiba viti dom sec, vilipoingia tu vilipigwa chapa ya mazengo, headmistress alipokuja akaambiwa angalia kama kuna kiti chako...all mazengo sec school...
Enzi hizo headmaster nani, mr mbao? Nakumbuka ili kutatua tatizo la purukushani za chakula mesini makanyagio ilikua kimbilio langu la kudumu asubuhi, mchana na usiku.
Mi nakumbuka mwaka 1994 tukiwa sengerema secondary a.k.a Singapore, ile tunaingia form 5 kuna mwalimu mmoja tulimkuta anaitwa mwalimu BUGA.kumbe bwana lilikuwa jina la utani...siku moja akanikamata sijaenda parade, basi akawa ananiuliza namjua yeye ni nani? me kwa kujiamini nikamwambia wewe si mwalimu BUGA.. aiseeeeeee nilichezea kichapo cha hatari..kumbe bwana BUGA lilikuwa jina la utani,,kwa vile alikuwa anavaa suruali zile BUGA..yaani ile juu imebana afu chini umemwagika..ahahaha sitasahau kabisa..