gracious86
JF-Expert Member
- Mar 25, 2011
- 437
- 55
Nakumbuka enzi za afande miraji makongo basi kulikuwa na mti wa maembe karibu na canteen ya shule ile kuona maembe yameiva akajua kuna madenti waroho wa maembe basi akaandika kibao 'ANGUA EMBE' akakitundika juu yake. Looh hakuna hata dent aliyedhubutu kusogea karibu. Kulikua na matoz wa pre form 5 walikuja kurudia masomo kuona kile kibao wakajua ruksa wakapanda kuangua embe afande miraj akawakamata kwenda kuwapa adhabu wakajua ni kwenda kupewa msitu kufyeka cha kushangaza kawapeleka kwenye ofis yake ilikuwa banda la mabati mbele yake kulikuwa na kisima cha taka basi kawaambia nisubirin hapa aingia ndan karudi na redio kaweka Taarab(mipasho) akawaambia haya vidole juu na muanze kuimba atakae onyesha mautundu atasamehewa.ilkuwa very funy
kwa wale pugu boyz wanakumbuka sana kwenda pondi na foleni za mihogo kwa mama pendo(rip),bila kusahau watu tulivyokuwa tunakata weeks bila kuoga coz shule haina maji...mvua ikinyesha ndo kila mtu anavua nguo akaoge kwenye mvua.
Mkuu umegusa penyewe, namkumbuka "Braza" Mpande na mambo yake ya kuja kuamsha watu kwenda mchaka mchaka. Kuna siku alikuja na kali ya mwaka: Eti akiwaona watu mjini alikuwa anawakariri uso, sasa watu wamegundua wakimwona tu wanageuka upesi na anashindwa kuwakariri uso, basi akasema atakuwa anakariri visogo. Baada ya majuma kadhaa akasema wanafunzi wakimwona basi wanageuka na kuvua mashati wanayafunga kichwani ili kuficha visogo, sasa akasema basi nitakuwa nakariri (ashakum siyo matusi) ******, nikiliona linaenda hivi au hivi basi nitajua ni la fulani,,, alikuja kutuacha hoi siku alipo-prove jinsi mbinu yake inavyofanya kazi kwa kumtolea mfano jamaa mmoja aliyemwona town Moshi,,
Yule Mwalimu sintokaa nimsahau aisee..
Mkwawa Complex and Casino, I just love it...Nilikwenda kufanya 'hijja' pale but was sad coz sasa imekuwa university. The government needs to preserve some sites for historic interests.
Mkuu umegusa penyewe, namkumbuka "Braza" Mpande na mambo yake ya kuja kuamsha watu kwenda mchaka mchaka. Kuna siku alikuja na kali ya mwaka: Eti akiwaona watu mjini alikuwa anawakariri uso, sasa watu wamegundua wakimwona tu wanageuka upesi na anashindwa kuwakariri uso, basi akasema atakuwa anakariri visogo. Baada ya majuma kadhaa akasema wanafunzi wakimwona basi wanageuka na kuvua mashati wanayafunga kichwani ili kuficha visogo, sasa akasema basi nitakuwa nakariri (ashakum siyo matusi) ******, nikiliona linaenda hivi au hivi basi nitajua ni la fulani,,, alikuja kutuacha hoi siku alipo-prove jinsi mbinu yake inavyofanya kazi kwa kumtolea mfano jamaa mmoja aliyemwona town Moshi,,
Yule Mwalimu sintokaa nimsahau aisee..
Watu waliosoma tanga tech hawatamsahau mr.mdoe.Nakumbuka ile mida ya saa 12 jioni tulikuwa na utaratibu wa roll call.Basi inapowadia saa 12,wanaume tulikuwa na tabia ya kujongea taratibu eneo la parade,basi akiwaona kitaa tu,utamwona anavyotoka nduki kuwa overtake ili akahesabishe roll call kabla hamjafika,halafu alikuwa na'ikibinda nkoi'fulani kama demu,yaani alikuwa na visa!Mkuu umenikumbusha sana Moshi Tech...
Kuna siku mpande alikuja dom letu no. 39 Karume kule na kutudaka kisa eti mshkaji mmoja alizima taa wakati tu kaingia bwenini. Sasa akatupeleka pale TYL ofisini na kuanza mikwara na vibao kibao kwa yule mshkaji ili amtaje aliezima taa. Jamaa kuona vibao akamtaja mshkaji wangu basi alikula vibaooo na wakati akiendelea kula vibao akamwambia Mpande... "..Basi ticha umeshinda..." Dah!! Utafikiri ndo alichochea mafuta kwenye moto, alikula makofi, vichwa, nakoz za kufa mtu mpaka tukataka kumzuia ticha ila mshkaji mwingine akadai tuache tu. Iliniuma sana hata kesho yake siku tuliyokuwa tunamaliza shule mshkaji aliepigwa akataka tukamuage ila nikamchomolea as hasira zilikuwa bado zipo..
Kwa waliosoma ile shule hawatomsahau Mpande aisee...
Love square!Kweli mkuu hasa yale maeneo ya bomba tatu na kibanda simama....
Mkwawa high school kwa sisi tuliosoma o level seminari tulipata shida sana nyakati za mwanzo kusoma na mabinti hasa nyakati za prepo. Kombolela hasa siku za jumatatu katika mabweni ya wavulana...
Mi nakumbuka mwaka 1994 tukiwa sengerema secondary a.k.a Singapore, ile tunaingia form 5 kuna mwalimu mmoja tulimkuta anaitwa mwalimu BUGA.kumbe bwana lilikuwa jina la utani...siku moja akanikamata sijaenda parade, basi akawa ananiuliza namjua yeye ni nani? me kwa kujiamini nikamwambia wewe si mwalimu BUGA.. aiseeeeeee nilichezea kichapo cha hatari..kumbe bwana BUGA lilikuwa jina la utani,,kwa vile alikuwa anavaa suruali zile BUGA..yaani ile juu imebana afu chini umemwagika..ahahaha sitasahau kabisa..
nakumbukuka niko sec siha ,siku moja jioni kuna jamaa kutoka kigoma alienda kujisadia ,na alikuwa na ada kwenye walet ghafla ikadondoka chooni,alikuwa form 6,akaanza kutindua choo kwa pembeni, akaingia na kuitoa ada ,bahati nzuri kulikuwa na vyoo vya kulenga set mbili.alinyoa nywele zote mpaka kwenye kope,he had a strange personality.