Enzi ulipokuwa boarding

Issue ilikuwa ni Iyunga Sec,
  • Nakumbuka nikiwa F1 jamaa yetu mmoja alipigwa na F2 hadi kuzimia kesi ikamfikia H/master, next day akaja assemble na huyu jamaa alikuwa adimu sana assemble siku akitokea tu wanafunzi wote wanakuja kumsikiliza wanajua kuna issue ya maana. Basi kauli aliyo itoa sitasahau alisema " Nyie F2 msiwapige hawa F1 tumboni mtawaletea matatizo " akaondoka zake na kuwaacha F2 wakishangilia
  • Siku ya graduation yetu hakuna F4 aliye kula wali kwa nyama maana vyoote vilimwagwa na wahitimu wenyewe kwa scramble kubwa kutokea mesini.
 
umenikumbusha Kanta,ilikuwa balaa,mpaka leo nikiangalia uso wangu nakumbuka sekeseke!, unapewa tsh 5, uende chanji kuleta sukar 1kg, na maandiz mfuko! We acha tu. Niliwapelekea mchanga kama 2kg hv, jamaa walishuka ka mvua kutoka kwenye vitanda juu, nilipokea kichwa cha mgosi mmoja,mpaka leo ni wanted kwangu!
 
siku ya punje aka nyali aka punga MAZENGO sekondari ilikuwa vta nakumbuka kuna jamaa kutoka kigoma alikuwa anaitwa kamanda kaenda hewani balaaa yaan alifanya mesi kama yake akisimama mlangoni hapiti m2, nakumbuka kuna siku watu walijipanga wakapita nae getini wakavamia mesi basi kila m2 kagawana nyali yake na watu kibao wakamiss
 
Thread hii imenikumbusha enzi nasoma Ifunda Tech. School: tulikuwa na secondmaster wa kijaluo aliyeitwa Saka, mzee alikuwa mpole sana ila alikuwa ni mbaya sana kama atakukamata na hatia kwa vile anaweza akakupa adhabu hata ya mwezi mzima. Alfajili moja alikwenda mabwenini kushtukiza zoezi la kukimbia mchakamchaka. Alipofika katika block no.3 la bweni la Seuta akagundua kwamba kuna wanafunzi ndani kama wa5 bado wamelala, akawaamsha na kuwaamuru watoke na wenyewe wajitaje majina yao akiamini kwamba watatii. Wale majamaa walishajua kuwa kwa giza lile si rahisi awakariri sura zao hivyo badala ya kutaja majina yao halisi wakajitaja kwa majina ya wachezaji wa Simba wa wakati ule: Hussein Masha, Mohamed Mwameja, Alfred Kategile, George Masatu na Edward Chumila. Alipomaliza kuandika majina yao akawaambia waungane haraka na wenzao ktk mchakamchaka. Kituko cha mwaka ni pale muda wa assembly ulipowadia na S/master huyo kuwasoma watuhumiwa wake ili awape adhabu, kila mtu aliangua kicheko na alipoambiwa kuwa hayo ni majina ya wachezaji wa timu ya simba na yy aliangua kicheko na kuondoka zake.
 
Dah!aliona aibu.
 
aisee hiyo ya headmaster kiboko. Duh!
 
Ulikuwa mwaka gani hapo Kanta?
 
Mie nltoka shule za day o-level nikaenda advance pale malangali iringa, kilikuwa kipindi maji yalisumbua fom5 tukawa duty kuchota maji, mm nilikimbia kubundi(kusoma) maji hayakutosha wapish hawakupika 2lishnda njaa shule ikawa kama imefungwa kwani 2lisambaa vijijin kuokoa maisha ye2!
 
Mazengo kulikuwa na fangas za mapumbu tulikuwa tunaita pumbu erosion. Zilikuwa zinawasha balaa. Alaf nyuka na gima ni balaa kwa watu wa kanda ya ziwa! umenikumbusha mbali sana.
 

Ha ha ha,..asee hii kali sana.,,umenivunja mbavu asee,..ha ha ha ha
 

lo! Mlikuwa balaa
 
QUOTE=Jaguar;1862910]Tanga tech kuna kiumbe mmoja anaitwa mdoe alikuwa mwalimu wa nidhamu.Yeye mkikumbana kitaa iwe makorola,kwanjeka,sahare,raskazoni beach n.k,ukimkimbia hata akikuona kisigino au kisogo,utamsikia anavyobweka nyuma,'wewe ni goodluck johnson lema,unaishi bweni la twiga,dorm C,cube namba 3,kitanda namba 245,Form V PCM 3,kesho tuonane uwanjani ukiwa na kwanja.[/QUOTE]

ha ha,,ama hakika huyu alikuwa professionale.,,
 
hahaha...enzi za sifongo(uji hauna sukari)....mapisi(Nyama) na chui(Ugali - ulikuwa na mchanga huo..)...bila kusahau kwaya(samaki)....wali ...nimesahau banaa....waliopitia Lyamungo sec watanikumbusha -hahahaha...nimekumbuka top layer...dah maisha ya boarding yalikuwa na raha zake....hasa kwa walikuwa viongozi
 
ha ha ha! Hii thread si mchezo, nakumbuka jitegemee enzi hizo h/master sasa alikua anataka watu waongee english muda wote wakati maafande wake hawajui kuna siku nilikamatwa mara wakati napelekwa ofisi ya nidham tukakutana na mkuu ghafla akauliza what is wrong with student? Afande akatoa macho, mzee nikadakia huku nikijitetea kwa lugha ya malikia na kumkandamiza afande kwamba ananikosesha vipindi. Kanali masawe akauliza kijeshi ''is it true?'' yule afande akauka na kujibu kwa sauti kubwa ''yes sir. Mzee nikaambiwa go to the class. Mbio nilizotoka hapo!
 
Nakumbuka F1 kipindi nikiwa Ruvu Sec mateso yalikuwa makali mno kiasi kwamba tulikuwa tuishi katika mabanda ya vyombo......Nasema mateso yalikuwa makali mno siwezi kusimulia.
 

mkuu Jiteute ulikuwa mwaka gani maana na mimi nimepita hapo
 
Yaap mkuu!ulitumia udhaifu wake,kosa moja>goli nyingi.
 
Nakumbuka kibaha sec,mshikaji mmoja alikutana macho kwa uso na mkuu wa shule akiwa kanisani huku hajavaa uniform kama ulivyo utaratibu wa shule.Ulipofika muda wa sadaka,badala ya jamaa kumkimbia mkuu,yeye ndo kwanza akaenda kukaa karibu nae ili aonekane bonge la mcha mungua.Jumatatu parade jamaa akazidi kudhihirisha alivyo mjinga,akaka frontline kabisa uso kwa uso na mkuu.Mkuu akamchomoa mbele akasema;namwadhibu huyu mwenzenu kwa sababu nilimkuta kanisani bila uniform halafu halafu akanidharau hakunikimbia.Pili,kama haitoshi,mimi nilishamsahau lakini yeye amekaa mbele kabisa nimuone.Jamaa alipewa adhabu ya kufyeka uwanja wa mpira uliotelekezwa kwa miaka kadhaa.
 
nakumbuka miaka ya 96-97 loleza,mlinzi alikuwa natabia ya kutuchungulia wakati wa kuoga. Cku hiyo kapita bafuni wanafunzi walipomuona wakatoka wote uchi wakaanza kumwita wacha atimue mbio akajua wanataka kumbaka. Jamaa hakurudia tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…