Hii kali, yaani brief case ya studio, sigara ya studio, lofia ya studio, uwa la studio, koti la studio, na hako kijimeza kilichooza pia cha hapo studio. Kwa vyovyote huyu alikuwa anatisha sana huko mitaani akitembea na hii picha yake, tena inaelekea alikuwa hatongozi mademu, yeye anaonesha tu picha basi kina mama wanaanguka chini kumuona Origino CEO na kumgombania. Dah raha kweli hii mtu unaonyesha picha tu then unachukua bila hata papara.
Siyo kituko bali alikuwa anakumbuka enzi zake kwani siku hizi hakuna muziki wa kweli kila kitu computer then mtu anajiita mwanamuziki wakati hajuwi hala hata moja ya muziki.
Si kweli. Moni Afinda - Orch: Kiam. Engunduka - Zingzong ya Veve Stars, Masua (Assossa) Orch: Les Kamale, na Mbale - Orch: Kiam, ila pia palikuwa na Lipua Lipua, Fuka Fuka, Kamavasty, Shamashama, Bella Bella, we acha tu. Muziki ulikuwa kipindi kile si siku hizi kelele tupu na mambo ya computer.