Enzi hizo

Enzi hizo

Enzi hizo mliokuwepo mnatumia kabla ya kutoka out
tupeni simulizi.....
 
The Boss hayo yalikuwa yananukia vibaya mno hivi bado yapo????Kulikuwa na ya kike pia nakumbuka
 
Alikuwa anatumia dada yangu; akienda shule akirudi vumbi linakuwa limemganda miguuni enzi hizo alikuwa Arusha Patandi; mimi niliogopa kupaka mafuta ya dada nilikuwa napakwa vaseline
 
Nimetumia haya hadi nimechoka...kabla ya hapo, si unakumbuka na yale mafuta ya bei rahisi ya Shanti...ya njano ukipakaa yanang'aaaa, afu ukipita kwenye kichaka chenye nyuki lazima wakutafune...ukipita kwenye vumbi lazima yadake vumbi lote...
 
Yale mafuta ya Ashanti ukipaka liwake jua dah utalia na nyuki, yalikuwa yananukia mpaka nyuki wanaanza kukufuata.
 
Du kweli mmenikumbusha mafuta ya shanti halafu soda DOUBLE COLA mnaikumbuka?
 
na yale ya quality ya chini Simba cjui..........ulikuwa ukipaka yanaacha pumba pumba zingaa juani!

Yu ilikuwa inahusu sana; hasa mkialikwa disco Iringa girls!
 
Du kweli mmenikumbusha mafuta ya shanti halafu soda DOUBLE COLA mnaikumbuka?

da! umenichekesha sana ndugu! DOUBLE COLA! enzi hizooooooooooo! ukinywa tumbo linajaa hadi vifungio vya gauni vinakatika! kwi! kwi! kwi!
 
Yap! Ilikuwa na gesi balaa; ukiinywea maandazi ndio usiseme! Kiwanda kwa hapa bongo kilikuwa Mwanza nakumbuka :becky:

Hahahaha hapo inakuwa kama umepiga kinti au common faida mara mbili unashiba balaa.
 
Nayakumbuka sana,yalikuwa mazuri hayo. Si unajua kila jambo na wakati wake mkuu...
 
Nimekumbuka na mengine yaliitwa Yollanda ilikuwa kazi kweli maana ukipita lazima watu wanyanyue pua kusikilizia marashi
 
Mzee signature yako tu ndiyo imenimaliza kabisa, au umeiandika hivyo kimakusudi?
 
Back
Top Bottom