Enzi hizo

kipindi hicho tulikua tunaita bazoka..nlikua napenda kununua vitu vitamu vitamu sana hasa nikitoka shule na kwa thamani ya hiyo pesa ilikua inanitosha kabisa
 
kipindi hicho tulikua tunaita bazoka..nlikua napenda kununua vitu vitamu vitamu sana hasa nikitoka shule na kwa thamani ya hiyo pesa ilikua inanitosha kabisa


Uliza waliokuwa wanakata kiu kwa beer wakati huo walikuwa wanatumia " dala " ngapi kupata chupa moja?
 
Waliowahi kutumwa
( kuagizwa) dukani kwa kutumia hii dala
 
nakumbuka nlikuwa nanunua pipi flani zinavimistari vya rangi tofauti, sikumbuki vizuri jina la hizo pipi!
 
ice cream...ilikuwa sh 1 ..na mihogo ya kukaanga @1 shilingi 1/=..hapo ni mihogo 4 na ice cream...hyo nakumbuka ndy pesa ya shule hyo....kila siku napewa 5/=


mhhh !bas wewe umesoma mjini umeongelea( ice cream) au umesoma zaman ! mie naikumbuka zaid sh 10!
 
Dah nakumbuka enzi hizo kipindi cha mwaka mpya ilikuwa raha sana, wazee, watoto, vijana walikua wakishirikiana kuzunguka mtaa kwa mtaa kupiga madebe na familia ambazo siku hiyo walilala walipata tabu mawe yalirushwa juu ya bati na mayai viza yalitupwa milango. Kwa watoto baruti ziliandaliwa mapema kabisa.
Dah kitu kingine bila nguo ya sikukuu au kitu cha gold/pilau siku hiyo hapakaliki hapaliki. Watoto wa siku hizi sijui vipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…