HOJA Malipo ya 'Special lumpsum' ya NSSF si ya haki

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
  • Tags Tags
    nssf
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Nimekuwa nikichangia fedha kwenye mfuko wa NSSF kwa zaidi ya miezi 88.

Baada ya kuwasilisha madai ya kupata special lumpsum baada ya mkataba wa kazi kumalizika, nilipewa jumla ya kiasi kilekile nilichokuwa nimechangia bila nyongeza yoyote.

Hali hii si sahihi. Je, mfuko hautumii fedha hizo kuwekeza na kuzalisha mapato?

Kutolipwa ongezeko lolote ni aina ya dhulma, kwani thamani ya shilingi 10,000 ya mwaka 2017/2018 si sawa na thamani ya shilingi 10,000 ya mwaka 2026 kutokana na mabadiliko ya gharama za maisha na thamani ya fedha.
 
Mkataba wako na wao unasemaje maana naona juzi kwenye gawio la 90 tsh kwa kila hisa ya CRDB nao wamepata bilioni za kutosha. Inamaana pesa zinawekezwa pia. Je hakuna mgao kwenye faida za uwekezwaje wa pesa zinazowekwa?
 
Nimekuwa nikichangia fedha kwenye mfuko wa NSSF kwa zaidi ya miezi 88.

Baada ya kuwasilisha madai ya kupata special lumpsum baada ya mkataba wa kazi kumalizika, nilipewa jumla ya kiasi kilekile nilichokuwa nimechangia bila nyongeza yoyote.

Hali hii si sahihi. Je, mfuko hautumii fedha hizo kuwekeza na kuzalisha mapato?

Kutolipwa ongezeko lolote ni aina ya dhulma, kwani thamani ya shilingi 10,000 ya mwaka 2017/2018 si sawa na thamani ya shilingi 10,000 ya mwaka 2026 kutokana na mabadiliko ya gharama za maisha na thamani ya fedha.
Sijui una umri gani?

Ndio maana wamekupa chap chap.

Maana ungefikisha miezi 180, ungekuwa na sifa ya PENSION.
 
Nimekuwa nikichangia fedha kwenye mfuko wa NSSF kwa zaidi ya miezi 88.

Baada ya kuwasilisha madai ya kupata special lumpsum baada ya mkataba wa kazi kumalizika, nilipewa jumla ya kiasi kilekile nilichokuwa nimechangia bila nyongeza yoyote.

Hali hii si sahihi. Je, mfuko hautumii fedha hizo kuwekeza na kuzalisha mapato?

Kutolipwa ongezeko lolote ni aina ya dhulma, kwani thamani ya shilingi 10,000 ya mwaka 2017/2018 si sawa na thamani ya shilingi 10,000 ya mwaka 2026 kutokana na mabadiliko ya gharama za maisha na thamani ya fedha.
Pole sana, mawazo yako ni sahihi lakini ndio maana mimi natumia medical benefits yao vyakutosha
 
Hapana special lumpsum ni pesa zako zote zilizopo kwenye mfuko unazipata baada ya kusubiri siku 90 toka mkataba kuisha (unemployment benefit) kisha kufungua madai. Ukilipwa unalipwa pesa zako zote+ increment, haubakizi hata senti huko baada ya kulipwa
Habari, sasa kuna mwenzetu alienda kufwatilia mafao yake haya ya "special lumpsum" alipambana hadi akafika stage ya kuweka alama za vidole. Hapo anasubiri tena takribani siku ngapi tena mpaka alipwe stahiki zake ?
 
Habari, sasa kuna mwenzetu alienda kufwatilia mafao yake haya ya "special lumpsum" alipambana hadi akafika stage ya kuweka alama za vidole. Hapo anasubiri tena takribani siku ngapi tena mpaka alipwe stahiki zake
Mimi nilifungua madai nikaambiwa nitalipwa ndani ya siku thelathini, lakini ndani ya wiki tu nililipwa
 
Duuh !. Cha kwanza ahsante kwa taarifa, pili hapa habari inabidi imfikie ili aende tena kwa ofisi zao kukumbushia zaidi. Maana yapata wiki 3 ahangaika na alalama kwamba kupitia nssf portal yake status haisogei hatua za mbele. Alafu na alianzia hapohapo kigamboni. …. Yani ni hoi
 
Me kesi yangu ni kama ya huyo ndugu yako,sema me wameniambia nibadilshe badala ya kuomba ile unemployment benefits,,wamenishauri niombe special lumpsum nichukue mzigo wangu wote,,ndo nimeandika barua week hii ya kubadili aina ya fao hapo ubungo.
 
Oh ok ! ... basi inaonekana ni mwendo wa kwenda ofisini mwao mara kwa mara na kutia pressure, huenda ikasaidia na kutoa matunda. Kila mtu huja na kesi yake na majibu yanakuwaga tofauti.

Hapa hapa kuna ndugu yetu katusaidia na majibu yake asema amepata mzigo wake mapema wa special lumpsum. Mimi huku kuna mtu akaribia mwezi na bado hola, ukipita kwenye nyuzi za humuhumu utakuta watu wakisema wamekwama stage kama zetu yapata miezi kadhaa, na kuna wengine wamekwama nyuma ya stage hizi (ku lodge claim, hadi kutia alama za vidole). Kutokana na ninayoyasoma na kushuhudia, inanipa picha kwamba waeza kuwa na hela NSSF na kuipata ikawa kama safari ya Imani 😅. Na wengi wakipata mzigo wanasahau kuja kushusha ushuhuda umu tupeane experience ilikuaje na mtu alitoboaje.
 
Wakuu Mimi tangu February nazunguka Ofisi za NSSF hadi leo. What's should I do? Niende na vilipuzi nikafe nao?
 
Back
Top Bottom