Enzi hizo

Tumgidie bwege hilo neno halitumiki siku hizi lakini halijapoteza maana leo unamwambia bint mkutane pahala anakuja na wenziwake 5 ndo yale yaleeee!
 
Hahaaaa nimeiimba hivo hivo haahaaa
 
Tumgidie bwege hilo neno halitumiki siku hizi lakini halijapoteza maana leo unamwambia bint mkutane pahala anakuja na wenziwake 5 ndo yale yaleeee!
Duu umenikumbusha Agoro Anduru
 
Kulikuwa na camera flan hivi unatoa thumni unaanza kuchungulia pembeni yupo mwenye camera anakwambia hapo mecca na picha inayo fuatia ni vatcan hiyo ya tatu ni marekani hapo mara thumni imeisha toa nyingine.
Enzi za thumni ni miaka gani(kama hutojali.).
 
Enzi za thumni ni miaka gani(kama hutojali.).
Juzi tu hapa miaka ya 80 maana yenyewe mwisho wake kutumika ni 84 au 85 jina lingine iliitwa sungura sababu huku nyuma kulikuwa na picha ya sungura miaka hiyo senti 20 unapata kitumbua. Baada ya mwaka huo 85 biashara ya kuuziana na kununuliana kwa thamani ya thumni ikaisha ikabaki penye matumizi ya taasisikama posta benki TANESCO idara ya maji vitu kama hivyo.
 
Umesahau kitu mkuu.Enzi hzo home wakipika wali na maharage huchezi mbali na asbh huendi shule kuvizia kipolo na chai
 
Asante mkuu, zimeniwai kidogo hizo sijazikuta.
 
Umesahau kitu mkuu.Enzi hzo home wakipika wali na maharage huchezi mbali na asbh huendi shule kuvizia kipolo na chai

Hiyo inategemea sehemu na sehemu......sehemu wanazolima sana mpunga wali hakiwezi kuwa chakula cha kushtua....
 
Hiyo inategemea sehemu na sehemu......sehemu wanazolima sana mpunga wali hakiwezi kuwa chakula cha kushtua....
Ila mzee mwenzangu mpunga (cheka na watoto )kwa ndondo khabari yake nzito ila kwa mikoa ya Mbeya na kanda ya ziwa sio issue sana hapo nakubaliana nawe na morogoro pia.
 
Ila mzee mwenzangu mpunga (cheka na watoto )kwa ndondo khabari yake nzito ila kwa mikoa ya Mbeya na kanda ya ziwa sio issue sana hapo nakubaliana nawe na morogoro pia.

Yaani kuna sehemu huko siku kukipikwa ubwabwa....utajua tu maana nyumba inakuwa na utulivu wa hali ya juu sana huku nidhamu zikitawala.....

Yaani mtoto hata umtume wapi atakimbia haraka na kurudi......

Huo ubwabwa hata uive saa ngapi....watu wapo macho tu....hata ikibidi mpaka asubuhi watu wanakula nao sahani moja.....

Niliwahi kuona mahali nilishangaa sana.....

Hata uandaaji wa chakula kwenye familia siku ubwabwa utaratibu unabadilika......
 
Mpunga kuna baadhi ya sehemu una thamani ya pekee utulivu siku hiyo 100%kuna dogo mmoja alipata bahati mbaya ya kukaa na mama wa kufikia mbaya basi siku huyu bimkubwa akipika pilau ni shida kwa dogo ukimkuta analalamika tu "siku ya pilau mwenzenu mi siifaidi siku ya pilau mwenzenu mi napigwa "basi atasema hivyo na kigugumizi chake mpaka anaanza kulia.
Hili likawa jina lake na amekua nalo.
 
Jackson Five ni aina ya kofia na si mtindo wa nywele.
Tizama picha yao utaona wote wana miembe nimechukulia taswira yao na wala si kingine.
Na labda ungeandika Jackson 5 hats ingekuwa bora lakini kuandika kuwa Jackson five ni aina ya kofia sidhani kama ni sawa kifupi ukiandika Jackson five hapo unakuwa umelitambulisha kundi na si bidhaa nyingine ndio maana nikaandika miembe ili kumpa picha msomaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…