Enzi Hizo S02

sikinde.jpg
 
Usitumie Pesa-Cosmas Chidumule na DDC Mlimani Park Orch.

Sikusimuliwa haya ninayosema,nimekusikia mwenyewe ukimsimanga yule msichana,
Eti kwa nini amempenda mtu kama Chidumule,kwanza fukara sina gari wala nyumba,nitampa nini huyo bibi jamani oooo

Sikusimuliwa haya ninayosema,nimekusikia mwenyewe ukimsimanga yule msichana,
Eti kwa nini amempenda mtu kama mimi,kwanza fukara sina gari wala nyumba,nitampa nini huyo bibi jamani oooo

Ameshasema hakutaki kaa chonjo,
Ameshasema hakutaki kaa chonjo..

Lazima katika mapenzi kamwe hakuna,na penzi la pesa duniani halipo,kwani hata kobe ana mpenzi wke na kamwe haijui pesa ooo baba ninasema....
Unamponda yule kijana ili bibi akuthamini wewe,ukimpenda msichana sema nae polepole,kamwe hakuna haja ya kumkashifu kijana mwenzio baba.....

Ameshasema hakutaki kaa chonjo,
Ameshasema hakutaki kaa chonjo..

Usitumie pesa,kama fimbo baba,mambo ya pesa mpaka makubaliano hapo ndipo pesa huwa na thamani eee....
Usitumie pesa,kama fimbo kaka,mambo ya pesa mpaka makubaliano hapo ndipo pesa huwa na thamani eee....

Ikiwa mapenzi mpaka bibi akupende,hata kama fundi wa kuhonga mpaka bibi akubali ooooo

Usitumie pesa,kama fimbo kaka,mambo ya pesa mpaka makubaliano hapo ndipo pesa huwa na thamani eee....

Ikiwa mapenzi mpaka bibi akupende,hata kama mzee kimwaga lakini kwa mipango.....

Usitumie pesa,kama fimbo kaka,mambo ya pesa mpaka makubaliano hapo ndipo pesa huwa na thamani eee....

Cecy amesema Cosma mpaka kufa,nami nasema Cecy wangu wa kufa na kuzikana.....

Usitumie pesa,kama fimbo kaka,mambo ya pesa mpaka makubaliano hapo ndipo pesa huwa na thamani eee....

Hata njiwa ana mpenzi wake kwenye tundu,ingawa njiwa hajui noti wala shilingi.................

Usitumie pesa,kama fimbo baba,mambo ya pesa mpaka makubaliano hapo ndipo pesa huwa na thamani eee....
 
Nimaru-Les Wanyika

Aaaaaaaa........Nimaru mtoto wa Tanga

Sheri ee usilie mwana mama ee,najua wanipenda Nimaru mama ee,sikupenda kukuacha uteseke nyumbani pekee,
Shida na tabu zinafanya watu kutengana mama eee....

Ooooooo mwanamama oooo,Oooooooo mwanamama.....

Safari niliyonayo ni ndefu sana ooo,sijui mwaka gani nitarudi mama yoyoyoooo,
Hata mimi sina raha kuwa mbali nawe ooo,lakini ni hali ya dunia ni vigumu kuepuka aaaaaaa

Ooooo Nimaru mama ee,Nimaru mama,Nimaru bibi.....
Ooooo usilie mama ee,usilie mama,ninarudi TZ...
Ooooo nitarudi bibi ee,nikuone mama,tufurahi pamoja...
Ooooo nifurahi nawe oooooooo.....

Sheri ee usilie mwana mama ee,najua wanipenda Nimaru mama ee,sikupenda kukuacha uteseke nyumbani pekee,
Shida na tabu zinafanya watu kutengana mama eee....

Sheri ee usilie mwana mama ee,najua wanipenda Nimaru mama ee,sikupenda kukuacha uteseke nyumbani pekee,
Shida na tabu zinafanya watu kutengana mama eee....

Ooooooo mwanamama oooo,Oooooooo mwanamama.....

Sheri ee usilie mwana mama ee,najua wanipenda Nimaru mama ee,sikupenda kukuacha uteseke nyumbani pekee,
Shida na tabu zinafanya watu kutengana mama eee....

Sheri ee usilie mwana mama ee,najua wanipenda Nimaru mama ee,sikupenda kukuacha uteseke nyumbani pekee,
Shida na tabu zinafanya watu kutengana mama eee....

Safari niliyonayo ni ndefu sana ooo,sijui mwaka gani nitarudi mama yoyoyoooo,
Hata mimi sina raha kuwa mbali nawe ooo,lakini ni hali ya dunia ni vigumu kuepuka aaaaaaa

Ooooooo mwanamama oooo,Oooooooo mwanamama.....

Safari niliyonayo ni ndefu sana ooo,sijui mwaka gani nitarudi mama yoyoyoooo,
Hata mimi sina raha kuwa mbali nawe ooo,lakini ni hali ya dunia ni vigumu kuepuka aaaaaaa

Ooooooo mwanamama oooo,Oooooooo mwanamama.....
 
naomba mwenye mashairi ya wimbo wa milima ya kwetu atuwekee hapa au kama kuna mp3 yake

.......umekuwa kama helkopta ndege isiyochagua mahala pakutua eeh.......

na kama kuna mwenye wimbo washakaza I na II atuwekee hapa maana sijapata hata mp3 zake
 
Sauda-DDC Mlimani Park Orch.

Sauda,Sauda oooh,Sauda dada…
Tangu tuwe wapenzi tumependana kikweli pendo letu la moyoni,
Mioyo tusibadili wangu kipenzi dada tuepuke ushauri
Kwa mahasidi wa penzi ooh Sauda kwa mahasidi wa penzi mama ooh Sauda

Sauda ooooh mama,Sauda ooooh mamaaa

Mv Mapenzi meli ya wapendwa nao,moyo kama bahari manahodha mimi na wewe

(Gurumo) Duniani kuna mengi sawasawa na bahari,kuna papa na nyangumi tena wale wa hatri,hawapendi kuiona meli yetu baharini watafanya kila njia waifupishe safari

(Gurumo) Duniani kuna mengi sawasawa na bahari,kuna papa na nyangumi tena wale wa hatri,hawapendi kuiona meli yetu baharini watafanya kila njia waifupishe safari Sauda eeh
 
Kesi ya Khanga(Monica)-ZAITA Musica

Mama nipe nauli nikamfuate Monika ee,amekimbilia Zambia na treni ya mizigo ee,kisa cha kukimbia madeni yamemzidi doti kumi za khanga alizokopa hajalipa ee,anatafutwa na Polisi popote hapatikani,na mimi rafiki yake nipo nje kwa mdhamana ee,nililala rumande siku mbili kituoni,usumbufu nilioupata kwa kweli sina raha ee

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi

Mahakamani wameshapanga siku ya kusikiliza kesi,asipokuja nitapelekwa jela kutumikia kifungo,ee Monika eeeh uko wapi ee,Monika eeh

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi eeeeh

Mahakamani wameshapanga siku ya kusikiliza kesi,asipokuja nitapelekwa jela kutumikia kifungo,ee Monika eeeh uko wapi ee,Monika eeh

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi eeeeh
 
naomba mwenye mashairi ya wimbo wa milima ya kwetu atuwekee hapa au kama kuna mp3 yake

.......umekuwa kama helkopta ndege isiyochagua mahala pakutua eeh.......

na kama kuna mwenye wimbo washakaza I na II atuwekee hapa maana sijapata hata mp3 zake

Ngoja nianze na Milima ya kwetu mkuu

Milima ya Kwetu

Nikitazama milima ya kwetu ee,
machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo,
tulitoka wawili ninarudi peke yangu,
baba na mama wataniuliza bibi yako yuko wapi ee,
Ndugu jamaa wataniuliza bibi yako yuko wapi eee,

japokuwa ninakaribia kufika nyumbani ee,
Ninatamani gari isifikie upeesi,
kwa ile aibu nitakayopata mbele ya wazazi ii,
kwa vile ni miezi michache imepita nilitoka na bibi yangu,

(Eddy)
Nitasema nini kwa baba mimi najuta aa,
kwa pesa zake nyiingi alizopotezaa,
harusi ilifanyika kwa gharama kubwa sana,
watu walikula na kunywa na kusaza mamaa,

Nikaenda kuishi na bibi yule mjini,
kazi yake ilikuwa ni vituko,
nikaenda kuishi na bibi yule mjini kazi yake ilikuwa ni vitiimbwi,

Alianza kuweka sukari kwenye mboga,
nikaonja haviliki tukalala na njaa,

kafuatia na kuweka chumvi kwenye chai,
nilikuwa na wageni wakatoka bila kuaga,

kafuatia kuchelewa akienda sokoni,
nikimuuliza anitukana hadharani aibu,

kuna gari imekuja hadi mlangoni,
kujitetea akasema mjomba wake kaja,

hivi juzi kavunja kioo cha dirisha,
apate kuchungulia wapitao njiani,

hatimaye kunibeza na kunidharau,
shikamoo ikaisha ikabaki
Vipi babu, mambo zakoo ee x2

Nilishindwa kumuuliza ee sikutaka kumuudhi,
sababu nilikuwa nampenda nampenda saana x 2

chorus:

walisemaa dalili ya mvua ni mawingu,
niliyempenda kanitoroka mama,

(Eddy Sheggy)
Nilinyang'anywa tonge mdomoni,
nilinyang'anywa tonge kinywani,
niliyempenda kanikimbia mama yoyo,
niliempenda kanikimbia masikini nifanye nini mama,

(chorus)

Vituko ee, vituko vya bibi huyoo,
sitaweza kusahau mimi oo mama ee,
sitaweza kusahau mimi oo sheggy ee,
alikuwa kama helikopta, ndege isiyochagua mahali pa kutua ee,
kila mtaa hapa mjini jamani tazameni oo,
ana bwana mmoja ama wawili mama mama oo,
nifanye nini mama oo,

(chorus)
 
Nasikitika

Nasikitika yeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..............Maisha yamenijia magumu,nashindwa la kusema....mmmmmmmmmmm
Nasikitika eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..............Maisha yamenijia magumu,nashindwa la kusema

Ningeelewa walimwengu ni wachina,mimi nisingekubali kuzaliwa,nsingekubali kuzaliwa ee,lakini nimedanganyika,wakati nalikuwa mdogo,nalikuwa nabebwa,nalikuwa nabembelezwa,nalikuwa nalishwa ee,sikutegemea kama leo nitakuwa hivi,eeeeeeee...

Ulimwengu uwanja wa mapambano,kila mtu kujitafutia,kula kwa tabu,kuvaa kwa tabu,kila kitu kwa shida....

Ilimwengu umejaa maovu,walimwengu tumezingirwa,magonjwa chungu nzima,hata ukijifanya wewe mlevi wa Gongo jirani yako anawagombanisha mke wako na watoto wako anawapika bila sababu kwa tabu,hata ukijifanya wewe mpenda mabibi mabwana hamsini lakini ujihadhari na Ukimwi utapata ukavu kwa tabu......

Ulimwengu imani imekwisha,imani imekwisha,imani imekwisha,watu wameota mapembe,hata watoto zetu heshima hawana tena,imani imekwisha,imani imekwisha,imani imekwisha....

Ulimwengu hakuna raha,hata ukiwa na mapesa ulimwenguni,porini hawakujui,mnyama hakujui,nyoka hakunujui,hasa mbu hakujui,hata ukiwa mheshimiwa ulimwenguni,majani haikujui,porini haikujui...

Ulimwengu uwanja wa mapambano,kila mtu kujitafutia,kula kwa tabu,kuvaa kwa tabu,kila kitu kwa shida....

Nasikitika eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.....

Nasikitika yeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..............Maisha yamenijia magumu,nashindwa la kusema
Nasikitika eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..............Maisha yamenijia magumu,nashindwa la kusema
Nasikitika eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..............Maisha yamenijia magumu,nashindwa la kusema........mmmmm........eeeeeeee

Nasikitika eeeee....kula kwa tabu,kuvaa kwa tabu,kila kitu kwa shida.......eeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,mmmmmmmmmmmmmmm
 
Last edited by a moderator:

Muziki Asili yake wapi

Muziki asili yake wapi eeeeee,Muziki ni wa nani eeeeeeeeeeeee,
Muziki hakuna mwenyewe,Muziki ni mwito,
Muziki ni fundisho,Muzi maombolezo kilio
Usinione nikiimba,ukadhani ninayo furaha,kumbe ninayo huzuni moyoni.

Muziki alivyo na nguvu ulimwenguni kote,
Hata makanisani wanaimba kwaya kwa kumuomba Mungu,kumuabudu Mungu,kwa kumsifu Mungu,
Hata kukiwa sherehe za serikali,mbele ya Mwenyekiti kuhutubia,ni Muziki unaanza kuwakusanya watu;
Kumbuka Paulo na Sila waliimba gerezani Mungu amewasikia,
Kumbuka Mussa aliimba Muziki wa aina yake,kuwakomboa wana wa Israel waliopo utumwani katika nchi ya Misri..

Kukiwa na sherehe utaimba nyimbo za furaha,kukiwa na tabu utaimba nyimbo za masikitiko;
Ukifa leo utapelekwa kaburini na nyimbo za maombolezo;
Ni mzuiki pekee ulio na nguvu,utawakusanya wabaya na wazurimsiku ya mwisho Mungu akitoa hukumu.

Muziki sio uhuni,kama muziki ni uhuni kwa nini unanunua kaseti;
Kama muziki ni uhuni kwa nini unaomba nyimbo redioni;
Kama muziki ni uhuni kwa nini kwa nini unanunua rekodi;
Kama muziki ni uhuni kwa nini unacheza muziki weeee;
Kama muziki ni uhuni kwa nini unafanya top ten show...

Kumbuka siku ya mwisho ikifika,kutakuwa mlio mmoja wa parapanda utawakusanya wateule wote,
walioteuliwa katika pembe nne za dunia siku ya mwisho mungu akitoa hukumu,hukumu,hukumu.
Hata kwa Mungu malaika wanaimba oooooooooooooooooooo

Muziki asili yake wapi eeeeee,Muziki ni wa nani eeeeeeeeeeeee,
Muziki hakuna mwenyewe,Muziki ni mwito,
Muziki ni fundisho,Muzi maombolezo kilio
Usinione nikiimba,ukadhani ninayo furaha,kumbe ninayo huzuni moyoni.
 
Last edited by a moderator:

Nalilia mtoto

Nakulilia Mola wangu weee,
Nakuwaza Mola wangu wee,
Yalonipata makubwa naona balaa,
Wala hamu sina x2

Wenzangu wana watoto,
Mimi sina hata wa dawa eeeh,
Niwatumapo wana wa wenzangu,
Mama zao hunisimanga x2

Nalia nasikitika bahati sina,
Kwa waganga wa kila namna nimefika ni bure tuuuu,
Hospitali za kila namna nimekenda ni bure tuuuu,
Mola nimemuomba na sadaka nimetoa ni bure tuuuu,

Mola, Mola, Molaaa eeeh,
Mola eeeh nataka mtoto,

Mola Mola, Molaa eeh,
Mola eeh, nalilia mtoto

Mtoto angelikuwa ni nguo ningenunua,
Mtoto ni mtoto kwa mama hakui,
Hata angelikuwa kilema au mbaya kama Remmy ni mtoto tu!

Mola Mola, Mola eeeh....
 
Last edited by a moderator:

Mariamu

ataka yote akosa yote
apita ahangaika asijue la kufanya ... asijue la kufanya
mshika mawili yote yamponyoka
apita akebakeba asijiue la kujitetea
mmmhhh mapenzi yawaka moto
naitika nilikukosea sasa nihurumie
si ninafikiri zaidi kuliko wewe
nakonda kama mnazi kwa mapenzi nilionayo
nilalapo nakuota mchana kutwa sili
moyo wanichechemea mwili damu hukauka
penzii eh ..... mmmh penzi eh x 2

nasumbuka kwako unionavyo moyo wangu
wewe ndio dawa yangu
Maraimu wangu
Tanga mbali
waja leo wondoka leoo
waja leo warudi leo

Mariamu bibi
mwenzenu sina pumuzi kujizuwia siwezi ohhh
mwanaume barabara kazi ya mume kwa mke
neno ya mke chumvi kwa mumewe
neno ya muke kachumbari kwa mumewe
penzi oh penzi likamung'uma he heh heh

likamung'uma hen heh heh .... mmhhhh
mdundiko, mdundiko ........ waaaaaa
mdundiko ...... waaaa
 
Last edited by a moderator:

Tembea Ujionee

Natembea popote unapokwenda,
iwe usiku ama mchana mbele yetu kuna mwanga wa maisha,
Natembea popote lakini wajua pa kula pa kulala,
maisha ya mtu tumefautiana na tumezaliwa mahali mbali mbali,

Mtu anaweza kufanana na nduguye sio shangazi wala mjomba,
labda pengine rafiki yake,
mkifanana kwa sura mwendo tofauti,
mkifanana kwa mwendo sura tofauti,
mawazo mbali mbali,
tabia mbali mbali,
mavalio mbali mbali,

Tumefikiria kuimba hivi kutokana na kutembea sehemu mbali mbali,
kutofautisha tabia na vitendo vya huyu vipi na kile vipi,
huyu bwana vipi na yule bibi vipi,
Hii shati vipi na suruwali vipi,
hii soksi vipi na kiatu vipi,

Kila mtu na kila sehemu vinatofautiana,
hauwezi kufananisha Morogoro na Darisalama,
tembea ujionee usingoje kuambiwa,

(chorus ya akina Skassy kasambaula na wenzake)
Tembea ujionee usingoje kuambiwa,
Duniani kuna mengi yote yanakusubiri x2

(Dr Remmy)
Tembea mama tembea bibi ii,
Tembea uone mambo,
tembea ushangae,
tembea upande mabasi,
tembea tembea tembea mama tembea bibi oo x2
oo tembea oo mama,

tembea oo mama
(oo tembea bibi oo)
tembea oo bibi oo
(oo tembea uone mambo)
tembea uone mambo

embea oo mama
 
Last edited by a moderator:
Asha Mwana Seif-JUWATA JAZZ BAND

Asha mwanaSeif niambie mpenzi wangu,imekuwaje leo mama uko kimya hivyo,ni lipi jambo limekuudhi nieleze leo,sema Asha seema mpenzi wangu kama mimi nimekuudhi unieleze

Nashukuru mume wangu kwa kuniuliza ooh,unakunywa pombe huonekani mpaka siku tatu,nachekwa na wenzangu,watoto wanateseka,hata huruma huna kwa hawa malaika, nachekwa na wenzangu,watoto wanateseka,hata huruma huna kwa hawa malaika

Ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto(mama Maika), Ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto

(TX) Aa mama,nimekubali maneno yako mama(ooh mama) wakale walisema mjinga kwa kwenda kwa kurudi anajuaa,pabaya na pazuri lelele

Ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto(mama Maika), Ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto

(Mbwembwe) Natubu mbele yako hata kwa hawa malaika,unisamehe Duniani hata mbinguni,nasema…

Ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto(mama Maika), Ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto
 
Leo tuko na Msondo tu...

Binti Maringo

(TX)Penzi langu limekosa umaarufu kwa sababu sina hela ooh Binti Maringo,sifa za uzuri wako zilinifanya niingie kichwa kichwa bila kuuliza,sasa umekuwa dalali unaunadi utu wangu ooh Binti Maringo,sasa umekuwa dalali unaunadi utu wangu ooh Binti Maringo

(Wote)Hapa nilipofika panatosha nisijefuga ugonjwa nikakosa dawa(rudia tena)
najua nina kiu na wewe nitakunywa maji nitulie...Maringo Binti Maringo nitakukukmbuka daima,Maringo Binti Maringo nitakukukmbuka daima,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika

(Gurumo)Dada Kawasaki alinikanya hapa mjini nenda polepole,utavamia walanguzi wa mapenzi waikaangae Roho yako inyauke kama mti

(Wote)Maringo Binti Maringo nitakukukmbuka daima,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika

Tuma-JUWATA JAZZ BAND

Nimesimama kwenye kona ya Uhuru na Msimbazi,natizama wanaopita wanaorudi mama ee,huenda nikaiona sura yake Tuma

Nimesimama nikiwaza ahadi yetu tuliyopanga,tukutane Darisalama Tuma mamaa nia na madhumuni wazazi wakuone

Nikarudi maskani Roho yangu inauma shoga yake kanijia na kunieleza Tuma e Tuma ee kishaolewa

Nikapatwa na mshituko moyo wangu kwenda mbio,sikutegemea Tuma kama angevunja ahadi yetu,ama kweli penye udhia penyeza rupia

Usinione nimekonda ewe Tuma hakuna lingine mama ila ni wewe Tuma(rudia tena)

(TX)Usiku wote nalala nikikuwaza na kuita jina lako oooh Tuma,naomba mama kama unanisikia mama unijulishe mama japo kwa barua

(TX)Matatizo umpenda anayependwa na wengi huenda ukanywa sumu au ukajinyonga,kwa kuwa Moshi bado ni kijana kubembeleza mama kawaida yangu

Usinione nimekonda ewe Tuma hakuna lingine mama ila ni wewe Tuma(rudia
tena)

Similar Discussions

Back
Top Bottom