Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,752
Habari za siku nyingi wakuu wangu...Heri ya mwaka mpya....
Baada ya kipindi kirefu cha kutokuwa hewani leo nimeona tuanze awamu nyingine ya 'Enzi Hizo' ambapo tunapata fursa ya kuzikumbuka nyimbo zilizotamba kipindi cha nyuma,kupitia mashairi ya nyimbo hizo pamoja na kuangalia maisha ya wanamuziki wa Dansi waliotamba enzi hizo hapa nchini kwetu Tanzania,DRC(Zaire),Congo Brazaville na kwingineko barani Afrika,zaidi tunaujadili muziki wa nyumbani Tanzania...Katika bandiko hili pia utajadili matukio/mambo mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika kipindi cha nyuma(kuanzia mia ya 90 kurudi nyuma) ambayo kumbukumbu yake ni burudani iliyopitiliza....
Ni matumaini yangu wakuu wangu akina Mzee Mwanakijiji,Baba Desi,Sanda Matuta,Gang Chomba,FMES na wengineo tutashirikiana katika kukumbuka muziki na matukio ya zamani ambayo kwa hakika ni hazina isiyochuja....Kwa kuanzia ninaomba tuanze kumjadili Daktari wa Muziki Tanzania Ramadhani Mtoro Ongala 'Dk.Remmy Ongala' aliyetutoka tarehe 13 Desemba na kuleta kilio kikuu miongoni mwa wapenda muziki wa Tanzania.....