1. Halafu unanyweshwa kidogo maji ya kuogea.......sijui maana yake
2.Mguuni unaguliwa na jiwe "laini" (siyaoni siku hizi)
3. Ole wako uwe na michubuko kwenye miguu kutokana na kucheza mpira halafu unakumbana na mama kauzu utakoma
4. Ukimaliza kuoga unakaushwa juani na kupakwa mafuta ya mamis na kuvishwa nguo ya mtumba
mshikaji hiyo ha ha ha ha ulivyoiachia umenisababisha niangue bonge la kicheko ofisini.Nina mengi ya kusimulia, nimekumbuka mbali sana ila moja ni pale ambapo unakuta una vidonda si mnajua mambo ya utoto vidonda miguuni ilikuwa ni lazima, unaulizwa kwanza na mwogeshaji vidonda viko sehemu gani, unamtajia ili achukuwe tahadhari.Ila duh! akikosea, balaa lake, unanisikia umesugua kwenye kidonda(kilio).Hahahahaha!
mshikaji hiyo ha ha ha ha ulivyoiachia umenisababisha niangue bonge la kicheko ofisini.
Haya mambo ya kusugua binadamu na mawe ndiyo leo nayasikia kwenu. Kwa mimi nijuavyo ni terrazzo tu ndizo husuguliwa na mawe!!
wakati mwingine unang'ang'ania kuoga peke yako, unamaliza unaitwa mguu ukisuguliwa unatoa km unga unga, unapelekwa unasuguliwa na jiwe ukitoka hapo dah. Those good old days
wangapi waliogeshwa kwa mtindo huu utotoni?mana unaambiwa fumba macho ukifumbua sabuni yake machoni utakoma!!!!!!!! !mana unasuguliwa na dodoki,jiwe au chupi yako na usipokuwa na balanceutakoma mana unasimama na mguummojaa uone hiki nn!!!!!
Duu umenichekesha sanaMkuu siku ya kuoga peke yangu ilikuwa ni "golden chance" kwangu, nilikuwa nahakikisha maeneo ambayo yanakaguliwa lazima yawe na maji;mfano, nilikuwa naosha miguu, kichwa halafu na kupaka maji kidogo tumboni maana ukaguzi ulikuwa unaanzia hayo maeneo.Hivyo mama alikuwa akishika tumbo akikutana na ubaridi anajua nimeoga.Nilikuwa nakata siku nyingi sana bila kuoga kwa mtindo huu.Utoto!