Enzi hizo kuogeshwa

Umenikumbusha mbali duh! Enzi zetu nakumbuka sabuni tulizokua tunatumia Lexona na Kwanga sikumbuki aina nyingine,mafuta ni mamis,jua kali,yolanda ya kwenye mkebe! Tumeona mengi hadi mambo ya vipi kukaba watu vifuani!
 
hii imenikumbusha mbali sana.....tulikuwa na housegirl mnoko sana....alikuwa ananisugua miguu na jiwe basi ananikwangua huyo......nilimchukia sana.......

Du huyo hausigeli noma sana, alikuwa anakukwangua kwangua, hakukuchubua sehemu laini laini?
 
1. Halafu unanyweshwa kidogo maji ya kuogea.......sijui maana yake
2.Mguuni unaguliwa na jiwe "laini" (siyaoni siku hizi)
3. Ole wako uwe na michubuko kwenye miguu kutokana na kucheza mpira halafu unakumbana na mama kauzu utakoma
4. Ukimaliza kuoga unakaushwa juani na kupakwa mafuta ya mamis na kuvishwa nguo ya mtumba

Hapo kwenye red mkuu huyo mama yako alikuwa mchafu eti? Hata mimi nimeogeshwa kwenye jiwe lkn hayo ya kunyweshwa maji mimi ndio nasikia na wewe. Labda ni ushirikina wa kabila lenu
 
hii imenikumbusha mbali sana.....tulikuwa na housegirl mnoko sana....alikuwa ananisugua miguu na jiwe basi ananikwangua huyo......nilimchukia sana.......

Watoto wa miaka ya 90. Enzi zetu hakukuwa na watu wanaoitwa HAUS GELI. Ni dada yako au mama mwenyewe
 
nilikuwa sipendi kuogeshwa nilikuwa napenda nijiogeshe mwenye, mtu akitaka kuniogesha kila atakapogusa ntalalamika nina kidonda hadi aniachie
 
Haya mambo ya kusugua binadamu na mawe ndiyo leo nayasikia kwenu. Kwa mimi nijuavyo ni terrazzo tu ndizo husuguliwa na mawe!!

ndugu sasa wengne maisha yetu tmesuguliwa na hayo mawe.. Mshukuru mungu kwakuwa uliishi maisha standard
 
ilikuwa ukimwagiwa maji kichwani unapagusa kauso na mkono huku unapuliza maji ili upumue kwa amani kidogo.,, mie nlikuwa nkiogeshwa mikono naziba kwenye ofisi... Kimbembe ilikuwa kuchanwa nywele babuu kipilipili si mchezo..,
ikitokeo uneoga mwenyewe ukaguzi unasuguliwa mgongoni,tumboni, miguuni lazma kuna sehemu maji yasifike
 
hahahaha jamani mmnikumbusha mbali sana, alafu kwenye goti palikuwa na uchafu umeganda hata uuoshe vipi ikitoka na damu na baanda ya siku 5 hiyoo umetia timu tena, yaani kama kenge vile! sujui pale kwa nini hapakuwa panasafishika!!
 
halafu uking'ang'ania kuoga mwenyewe ukirudi sabuni kila mahali, na mkono usoni kufuta maji, nyuma ya miguu itakuta michirizi ya maji eti umetoka kuoga! dah, utoto raha!!
 
kali ni pale baada ya kuoga unavalishwa kaptula ya kushona kwa mkono, kiunoni unafungwa manati aisee yanabana hayoo usiombe!! na nyuma kuna matundu mawili kila tundu lina saburi (kalio) kama taa za starlet
 
Times change....picha hii inanikumbusha miaka mingi iliyopita....nimesahau kabisa kama nilikuwa naogeshwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom