Enyi wanasiasa, ulimwengu si mahali pema

m2020

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
979
1,353
Kuna la kujifunza kubwa sana kwa wale wanaokumbuka semi zifuatazo hapa chini:-

1. Dunia tambara bovu.
2. Dunia mti mkavu usi uelemee.
3. Asiyefunzwa na ***** hufunzwa na ulimwengu.

Semi hizi tatu hapo juu zimenifanya asubuhi ya leo niwasihi sana wanasiasa wa vyama vyote nchini mjitafakari sana kwa kauli, vitendo na tabia zenu kwa taifa letu. Viashiria vikubwa vya kuanguka kwako ama kuanguka kwa jamii na taifa lako ni kauli, tabia na mienendo yako. Tujifunze kupitia semi hizo hapo juu kwa kauli na vitendo vyetu kinyume chake ni mahangaiko na mateso.

Sifurahii yaliyomkuta Tundu Lissu hata kidogo na ni kinyume cha ubinadamu na ustaarabu lakini napata fundisho kubwa na ninahisi kuna sababu iliyopelekea yamkute yaliyotokea kwake na niombe na kuwasihi wanasiasa na wanajamii tuwe makini dunia si mahala pema sana pa kuishi na kujivunia.

Tujitahidi kuishi kwa staha tukitumia hekima, heshima, maarifa, busara na akili zetu vyema huku tukimtanguliza mungu mbele siku zetu zote za maisha yetu. Kwani biblia takatifu inasema dunia mapito, tulitoka mavumbini na mavumbini tutarejea.

JIEPUSHENI NA SIFA, VIBURI, MAJIGAMBO NA TAMAA ZA MADARAKA NA MENGINEYO YANAYO FANANA NA HAYO KWANI DUNIA TAMBARA BOVU HUCHANIKA POPOTE.
 
Back
Top Bottom