Enloop Business plan software | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enloop Business plan software

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kweli, Jun 3, 2011.

 1. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Inapokuja katika masuala ya kuandika mpango wa biashara(Business plan), hakuna uhaba wa zana mitandaoni na tutorials kusaidia wajasiriamali kugeuza mawazo yao kuwa ya ukweli. Lakini ni ngapi kati ya zana hizo zinao uwezo wa kutumia mahesabu ya algorithm na kukutabiria uwezekano wa biashara yako kufanikiwa?

  Enloop ni tovuti ambayo wiki hii imetoa software ambayo imeahidi kufanya hivo, unahitaji tu kusaini nao kwa muda wa majaribio bure (free trial)

  Wanasema hii software mbali na kukusaidia kuweka sawa text, pia itakusaidia kwenye kujua makisio ya mapato (financial forecasts) ikiwemo faida na hasara (profit and loss) muenendo wa mapato (cash flows) na pia uwezekano wa kupata mkopo.

  Basically unajaza maelezo kwenye auto form vitu kama business idea yako, product, walengwa nk. kama desturi ilivyo unapoandika business plan yoyote. Ukimaliza utapata Score yako alama ngapi na kadiri unapopata alama nyingi ndio itaashiria urahisi wa kupata fundings kwa ajili ya venture yako, mfano mkopo wa benki.

  Mimi nahisi kwa wale wanaotaka kujua probability or rough idea ya wao kupata bank loans based on their business plans to try this little software, it worth a try and cost you nothing.
  Hii habari na Link yao utaipata hapa:

  Enloop Writes Your Business Plan For You (And Tells You If It's Crazy or Not)
   
 2. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  safi sana nitaijaribu ila banki za bongo lazma ukate kidogo kwa loan officer au akupe mtu ndo aandike bizz plan yako ili aipitishe ,ukija na biz plan yako haipiti ng'o
   
 3. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Asante kwa taarifa... ngoja niifanyie kazi..
   
 4. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hilo ndio tatizo kubwa kwa benki zetu, hawa loans officers hawana ethics kwenye kazi zao, kwao ni lazima uwagaie karushwa ndio wakuhudumie, mdogo wangu alitaka start-up loan na nilimuandalia business plan ya kufa mtu na niliweka sawa mambo yote usajili wa kampuni, aina ya biashara, ofisi, bank statements, cashflow projection etc, na house title deeds yenye thamani ya milioni 50 kama bondi kwa mkopo wa mil. 20 tu.
  Matokeo yake walimpiga na chini bila sababu za msingi, eti sababu yao kubwa ni kwamba kwa sababu ndio anaaza wanamuona 'bad risk' wakati benki hiyo hiyo imetoa mikopo kwa starters ambao ni high risk zaidi kwa vile tu walinyoosha mkono kwa maofisa mikopo.
  Nchi yetu hii kazi kwelikweli kutoka kwa sisi wanyonge.
   
 5. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Jaribu mkuu, good luck.
   
Loading...