Eneo la shule kuwekwa maduka

Eneo la shule kuwekwa maduka

Mimi ni Mkazi wa Pugu,Ninapokuwa njiani kuelekea kazini/Mjini nilikuwa nikishuhudia kuvunjwa kwa sehemu ya uzio wa shule na ujenzi wa frame za maduka....
Hiyo shule ni ya elimu ya Msingi Pugu Kajiungeni.
1. Je,hili suala ni linaruhusiwa...
2. Kama ni sawa ,mfumo wa uksanyaji pango na faida yake, kisheria unakuwa chini ya taasisi gani?
View attachment 3653476
1. Ujenzi wa maduka kwenye eneo la shule , tena shule za umma, hauruhusiwi. Serikali ya kipigaji inaruhusu maana kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake

2. Kodi ya pango inakusanywa na mkuub wa shule / mwalimu mkuu. Hapo inagawanywa, fungu flani linaenda kwa afisa elimu wilaya, fungu lingine kwa afisa elimu mkoa. Mwalimu mkuu asipokata posho basi anahamishwa shule na hao mabosi wake aliowanyima posho.

3. Mwalimu mkuu anagawana na kamati ya shule. Shule iliyopo katikati ya mji, kama zile za Temeke, mwalimu mkuu ni milionea, afisa elimu anakula fungu kati ya 1m - 5m kila mwezi, kulingana na wingi wa frem na location shule ilipo.
 
Uchumi wa fremu...kila uzio unajengwa fremu hadi uzio wa kambi za jeshi! Enzi hizo tuko wadogo kupita tu kwenye uzio wa jeshi unaogopa leo kunajengwa fremu na bar!
Haya yanaondoa sana Hadhi ya Jeshi
 
Kawaida tu,Pamba Sec ya jijini Mwanza wana hayo maframe miaka inafika 20 sasa hapo Mitimirefu tena itakuwa ni PPP ya Bwana Kafulila.

Wazazi hudhurieni vikao shuleni lazima kamati ya shule ambayo inajumuisha wazazi ishatoa maelezo huko.
 
Kawaida tu,Pamba Sec ya jijini Mwanza wana hayo maframe miaka inafika 20 sasa hapo Mitimirefu tena itakuwa ni PPP ya Bwana Kafulila.

Wazazi hudhurieni vikao shuleni lazima kamati ya shule ambayo inajumuisha wazazi ishatoa maelezo huko.
Swali la Msingi
1.Je,inaruhusiwa kisheria...?
2 Je,ni sawa kitaaluma

Kuna shule zipo hivyo ,ukichunguza shule ipo ndani ya eneo la Taasisi mf.Shule ya msingi Mbuyuni.
Eneo ni la Kanisa Katoliki

Sehemu moja kukosea na kufumbiwa macho,haihalalishi jambo halam...
 
Swali la Msingi
1.Je,inaruhusiwa kisheria...?
2 Je,ni sawa kitaaluma

Kuna shule zipo hivyo ,ukichunguza shule ipo ndani ya eneo la Taasisi mf.Shule ya msingi Mbuyuni.
Eneo ni la Kanisa Katoliki

Sehemu moja kukosea na kufumbiwa macho,haihalalishi jambo halam...
1.Hakuna sheria inazuia shule au taasis ya elimu ya umma kutokuwa na vitega uchumi.

2.Kitaaluma napo hakuna tatizo sababu shule za mijini zimezungukwa na hayo mafremu ya watu binafsi so hata wasipojenga wao bado hawazuii wengine kujenga jirani yao.
 
Hiyo ni E.K au Elimu ya kujitegemea shule itakusanya mapato yatakayosaidia kuendesha mambo madogo madogo kama chai na chakula Cha mchana kwa walimu kununua baadhi ya VIFAA vya stationary
 
Back
Top Bottom