Eneo la kibiashara Ubungo kwa EA, litakua na utofauti gani hasa?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Naomba kujuzwa, jee ni mbadala wa kariakoo?
Zaidi ya kariakoo? Au tofauti na Kariakoo?

Kila mtu ana majibu yake, kama kuna anayejua msaada tafadhali..
Moja ya majibu
"itakua ni soko kubwa la bidhaa za jumla zaidi ya k.koo jee ni kweli"?

Kama hujui una maamuzi ya kupita kimya au faida ya kujifunza,
Usijaze nzi kwa comments chafu..
 
Naomba kujuzwa, jee ni mbadala wa kariakoo?
Zaidi ya kariakoo? Au tofauti na Kariakoo?

Kila mtu ana majibu yake, kama kuna anayejua msaada tafadhali..
Moja ya majibu
"itakua ni soko kubwa la bidhaa za jumla zaidi ya k.koo jee ni kweli"?

Kama hujui chagua kupita au kujifunza,
Usijaze nzi kwa comments chafu..
Kwanini hili soko lisingejengwa Mbezi au Tegeta kupunguza msongomani mjini hapa ?
 
.wangejenga kibaha kabisa au chalinze...
Unajua watu wanaopata madaraka ya maamuzi wengine wamekuja mjini watu wazima....hiyo misongamano wanaona kama ndo kawaida ...hawakuwepo mjini kipindi misongamano haikuwa mikubwa hivi
 
Hakika pale Ubungo hapakustahili kabisa kutengeneza msongamano wa kujitakia.

Dar es Salaam inastahili masoko mengine makubwa saizi ya kariakoo pembeni kabisa ya Mji Kibaha Kibamba au Bagamoyo huko badala ya kuweka ubungo ambapo hakuna hata barabara za kutokea.
 
Unless walifunge la kkoo ...
 
Kati ya kitu ambacho nakipinga, nitaendelea kipinga ni hilo soko.
Wachina hawakupaswa kuja fungua maduka Bongo, walipaswa wajenge viwanda.

Serikali imekosea sana na inaendelea kosea.

Taifa letu litakuwa dampo la made in china, wataleta kila kitu na kuuza.

Hadi wamejenga hapo kuna incentives serikali imetoa
 
Ni sawa na kariakoo,
Sioni ubaya wa hilo soko kwani limekuja wakati sahihi maana mahitaji ya bidhaa yameongezeka na watu wanazidi kupata pesa kila siku,
 
Back
Top Bottom