Endelee Kupumzika Kwa Amani Baba Wa Taifa, Tanzania Ipo katika mikono Salama Ya Mwanao Mama Samia Suluhu Hasssan

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu ni miaka Sasa Tangia Baba Wa Taifa Hayati Baba wa Taifa atutoke, Hakika lilikuwa Ni pigo kubwa Sana kwa Taifa letu kuondokewa na Baba Wa Taifa Mlezi wa Taifa, maktaba ya Taifa, Rejea ya Taifa, Mfariji wa Taifa, Mwongozo Wa Taifa, Mwenye kauli iliyosikilizwa na kuheshimika na kila mtu, Hakika alikuwa Ni Baba Wa Taifa kwelii kwelii, kauli zake ziliheshimika Sana, hotuba zake zingali zinasikilizwa mpaka kesho, maneno yake yangali hai mpaka Sasa, bado anaendelea kunukuliwa na viongozi kila Kona bila kujali itikadi ya vyama vyetu,

Sasa amelala, Amelala baba Wa Taifa, amelala usingizi Wa Milele, amefumba macho na hawezi kuona ya Duniani, Ametutoka kimwili lakini kiroho bado anaishi katika mioyo yetu, sauti yake na nasaha zake zingali zinasikika katika masikio yetu, Tulimwamini na aliaminika kwa kauli na Dhamira yake kwa Taifa hili,

Baba wa Taifa amekufa mwili lakini yupo hai katika mioyo yetu, yupo katika fikira zetu, bado tunamuona Kama mshauri wa Taifa letu kupitia hotuba zake, vitabu vyake na hata kauli zake, kila tukijikwaa Kama Taifa tunarejea kumsikiliza na kujisahihisha kupitia hotuba zake, Hakika alikuwa ni Nabii aliyeutangulia wakati au aliyekuwa mbele ya wakati, aliyetutangulia watanzania, alikuwa mbele ya muda, alifika ambako hatukufika kifikira na kimawazo,

Hakika watanzania tulimpenda Kama baba mlezi wa Taifa hili na Tulifurahi kusikia akiongea, tulifarijika kusikia sauti yake, tulipona kupitia kauli zake, alituongoza watanzania kwa upendo mkubwa Sana pasipo ubaguzi wowote ule, alituunganisha tukawa Taifa moja lenye lugha moja na umoja wa kitaifa

Pamoja na kwamba watanzania tulimpenda baba wa Taifa na kutamani Kuendelea kuwa naye, lakini watanzania Tunapata faraja mpya, Tumaini jipya na zawadi ya kiongozi anayekuja na kuyaishi na kuyatekeleza kwa matendo Yale yote aliyoyahubiri Baba wa Taifa katika uhai wake, Yale yote aliyoyapigania katika uhai wake, Yale yote aliyo hitaji kuyatimizi na kuona yakifanikiwa katika uhai wake

Huyu Ni Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Rais anayapigania na kuyatenda maono ya Baba wa Taifa, Sote Tumeona namna alivyoliunganisha Taifa letu na kujenga umoja wa kitaifa, sote tunaona namna anavyopambana kuhakikisha kuwa Haki inatamalaki katika Taifa letu na kwamba kila mtu anatendewa haki bila kujari Hali yake,

Sote Tunaona namna mh Rais anavyopambana kwa vitendo na maadui watatu wa ujinga maradhi na umaskini, sote tunaona namna anavyopambana kuhakikisha mtanzania mnyonge anainuka kiuchumi,
Hapa unaona namna ambavyo ametoa Ruzuku ya mabillioni katika kilimo secta ambayo Ni pumzi ya watanzania wengi

Sote Tumeona namna anavyopambana kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata fursa ya Elimu hata Kama ametoka familia maskini ndio sababu ya kufutwa kwa Ada toka shule za msingi mpaka sekondari huku mikopo ikipatikana na kutolewa bila ubaguzi kwa wanafunzi wa Elimu ya juu , sote tunaona namna ambavyo huduma za kijamii zikiboreshwa na kusogezwa karibu ya mwananchi, sote tunaona juhudi za mama Samia kuimarisha demokrasia yetu hapa nchini na kila mtu akishiriki katika ujenzi wa Taifa letu

Sote Tunaona namna watanzania wanavyoishi kwa amani na upendo bila hofu Wala wasiwasi wowote, tunaona namna Rais Samia alivyowafanya watanzania kujivunia utanzania wetu, tunaona namna Taifa likiwa moja na kushirikiana kwa kila kitu, Tunaona namna mh Rais wetu mpendwa mama Samia alivyojenga matumaini kwa watanzania, kila mtu Sasa anamatumaini ya kesho yake kuwa njema

Baba wa Taifa endelea kupumzika kwa Amani, Tanzania ipo katika mikono salama Ya Mwanao Mama Samia Suluhu Hassan aliyeibeba Tanzania katika mabega yake kwa upendo na uzalendo mkubwa Sana

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Back
Top Bottom