Emmanuel Macron siyo Rais wa kwanza kuzabwa kofi

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,738
155,423

Emmanuel Macron: Rais wa Ufaransa sio wa kwanza kushambuliwa kwa njia hiyo​


mACRON

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amepigwa kofi usoni wakati wa ziara rasmi ya kusini mashariki mwa Ufaransa

Kwenye video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Bwana Macron anaonekana akitembea kwenda kwa kizuizi katika safari ya kwenda Tain-l'Hermitage nje ya jiji la Valence.

Mwanamume anampiga kofi bwana Macron usoni kabla ya maafisa kuingilia haraka. Rais, wakati huo huo, anakimbizwa kupelekwa eneo salama.

Wanaume wawili wamekamatwa kufuatia tukio hilo, kulingana na vyombo vya habari vya Ufaransa.

Rais anapopigwa kofi, maneno "Down with Macron-ism" yanaskika

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Wanasiasa wamekashifu haraka tukio hilo

Waziri Mkuu Jean Castex aliliambia Bunge la taifa muda mfupi baadaye kwamba wakati demokrasia ilimaanisha mjadala na kutokubaliana kwa njia halali "lazima iwe kwa vyovyote vile haina maana ya vurugu, uchokozi wa maneno na hata shambulio la kujeruhi".

Kiongozi wa mrengo wa kushoto Jean-Luc Mélenchon aliandika katika twitter "mshikamano na Rais" mara tu baada ya kiongozi huyo kushambuliwa kwa kofi.

mACRON

CHANZO CHA PICHA, EPA
Rais Macron kwa sasa anafanya ziara nchini Ufaransa na alikuwa ametembelea shule ya hoteli huko Tain-l'Hermitage. Ziara yake katika eneo hilo ilipangwa kuendelea Jumanne, maafisa walisema, na safari ya taasisi ya ufundi kwa vijana walio na miaka umri wa miaka 25-30.

Ziara ya rais inakuja usiku wa kuamkia hatua kubwa kwa baa na mikahawa ya Ufaransa, ambayo itaweza kufunguliwa tena kwa wateja wa ndani baada ya miezi saba ya kufungwa. Amri ya kutotoka nje wakati wa usiku nchini Ufaransa pia inasongeshwa nyuma siku ya Jumatano kutoka saa tatu hadi saa tano usiku.

Visa vingine vya mashambulizi dhidi ya viongozi

Kuna visa vingine ambavyo vimewahi kutokea wakati marais wa nchi nyingine walishambuliwa na watu katika umati . miongoni mwa visa vinavyokumbukwa sana ni cha maajuzi mwezi machi ambapo rais wa Argentina .Mwingine aliyewahi kushambuliwa pia ni rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy mwaka wa 2011.

GSPR officers protect Mr Macron at public and private events

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Nicolas Sarkozy-2011

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy pia aliwahi kujipata mashakani katika tukio kama la Macron wakati alipokuwa akiwasalimia wananchi kisha ghafla mwanamme mmoja aliyekuwa kwenye umati alipomshika koti na kujaribu kumpiga kofi.

Sarkozy alijibu haraka na alionekana akikwepa na hakujeruhiwa; muda mfupi baadaye alikuwa amerudi kuwasalimia watu wakati maafisa wa usalama wakimkamata mwanaume wa umri wa miaka 32 aliyejaribu kumshambulia

Rais Alberto Fernández - 2021

Katika tukio hilo mwezi machi waandamanaji kadhaa walishambulia basi dogo lililokuwa limembeba Rais wa Argentina, Alberto Fernández, katika mkoa wa Patagonia nchini humo.

Umati wa watu ulikusanyika karibu na Bwana Fernández na kurusha mawe na kupiga gari lake nje ya kituo cha jamii katika mkoa wa kusini wa Chubut.

Rais alikuwa akitembelea eneo lililoharibiwa na moto wa misitu, ambao ulisababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine .
Lakini maandamano hayo yalikuwa dhidi ya mipango ya kuanza tena uchimbaji wa madini katika mkoa huo.

Waandamanaji walikasirika na mapendekezo ya serikali ya kuruhusu miradi mikubwa kuanza tena katika mkoa huo, ambao una utajiri wa dhahabu, fedha na urani, gazeti la Clarín liliripoti.

Picha za shambulio hilo zilionyesha watu wakikusanyika kwenye lango la kituo cha jamii wakati Bwana Fernández akiongozwa kuelekea gari lake.

Umati kisha ulimfuata rais na kuanza kupiga ngumi na mateke basi dogo, kupiga madirisha kwa mawe na kujaribu kuizuia isisogee.
Rais Fernández baadaye alijaribu kupunguza vurugu hizo, akisema aliamini ni kazi ya idadi ndogo ya watu ambao hawakuwa na msaada wowote huko Chubut au kote Argentina.

George W Bush -2008

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari Desemba 14, 2008 katika ikulu ya waziri mkuu huko Baghdad, Iraq, mwandishi wa habari wa Iraq Muntadhar al-Zaidi alimshambulia rais wa Marekani wakati huo George Bush kwa kumrushia viatu vyake.

"Hili ni busu la kuaga kutoka kwa watu wa Iraq, wewe mbwa." Alifoka mwanahabari huyo. Al-Zaidi alipata majeraha wakati alipobanwa chini na maafisa wa ulinzi na vyanzo vingine vilisema aliteswa wakati akiwa kizuizini, waziri mkuu Nuru Al Maliki alijaribu kuvizuia viatu hivyo kumjeruhi rais Bush.

Silvio Berlusconi 2009

Mnamo mwaka wa 2009 waziri mkuu wa Italia wakati huo Silvio Berlusconi alishambuliwa na mwanaume mmoja wakati alipokuwa akitia saini vijitabu kwa wananchi waliofurika eneo moja ili kumtazama.

Iliripotiwa kwamba waziri mkuu huyo aligongwa kwa kifaa kama kinyago ama ngumi na mwanaume mmoja katika kanisa kubwa la Milan ,Duomo.Kiongozi huyo alianguka na kupata majeraha mabaya usoni na kulazimika kukimbizwa hospitalini. Alikuwa akitia saini vijitabu hivyo na kuwasalimia watu mikononi aliposhambuliwa.
 
Wanakwama wapi?Waje kujifunza mbinu kwa CCM.Wanaandaa wauza kahawa na wachoma mahindi wao kabla ya kwenda kuwasabahi wananchi.😝😝😝😝😝
 
wanafanya ulaya tu !
hapa ukichora katuni au kukosoa kitakacho kutokea ! shetani labda kukuonea huruma.

je ukizaba kofi hata askari tuanzie hapa !
 
hata libashite lilimkata ng'wara mzee Waryoba na likamtembezea nakoz kwenye katiba ya waryiba
 
Back
Top Bottom