Eminem aongoza orodha ya Rappers wanaotoza mkwanja mrefu kwa collabo moja

Mdudubitehunter

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
305
514
Majarida mbalimbali nchini Marekani yameorodhesha rapper 10 ambao wanachaji kiasi kikubwa sana cha pesa kwa ajili ya kumshirikisha kwenye wimbo wako wowote ule.

Katika orodha hiyo mkongwe Marshall Bruce Mathers III alimaarufu kama Eminem kwenye umri wa miaka 50 amewafunika vijana wengi sana kwenye suala la kuchaji kiasi cha pesa ili umshirikishe kwenye wimbo wako.

Eminem anachaji dola milioni 3 sawa na Tsh 7,020,000,000/= yaani bilioni saba huku akifuatiwa na Drake ambaye anachaji kiasi cha dola milioni 1 ambazo ni sawa Tsh 2340000000/= yaani bilioni 2.34.

Katika orodha hiyo rapper ambaye wengi hawakutarajia ni J Cole ambaye anachaji dola 2,000 kwa neno moja kwenye wimbo wako ambayo ni sawa na Tsh 4,680,000/= yaani milioni nne na laki sita za Kitanzania kila neno kwenye wimbo wako inategemeana na maneno mangapi.

Katika orodha hiyo wengi wame-comment wakishauri Future anatakiuwa kuongeza malipo yake huku wakisema kuwa dola laki mbili na nusu ambazo ni sawa nna T sh 585,000,000/= yaani zaidi ya milioni mia tano sio saizi yake.

Unahisi kwa Tanzania msanii gani anaongoza kutoza kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya collabo??

Credit: Bongo5
FB_IMG_16787887483046534.jpg
 
Hiyo see write up below katika cell ya Jay z na Kanyewest wamesema wao hawachaji hata shilling mia tano kufanya nao Collabo bali wanaangalia tu heshima ya msanii husika na aina ya wimbo wenyewe

All in all Drake ni bidhaa kubwa sana sokoni ukibahatika kufanya nae Collabo kwa hiyo dolla millioni moja tegemea kuwa superstar na kuzalisha maradufu ya pesa uliyoiweka kwa collabo Diamond inabidi amtafute huyu au amuulize mwenzake Wizkid alivyofanywa kuwa Global superstar na Drake
 
Kabisa Mkuu,.
Umeongea Ukweli.

Ila kumpata huyo Drake ufanye nae ngoma ndo kipengele.
 
Back
Top Bottom