Hata huo utumwa wa Time + Space + Matter unaonekana kufanya kazi kwa msingi wa kumbukumbu tu.
Kwa maana muda wenyewe hauwezi kueleweka bila kumithirisha kilichopita na kilichopo sasa, vile vile space huwezi kuitambua bila reference ya sehemu nyingine ulizowahi kuziona na matter nayo hupata maana kutokana na patterns ambazo tayari zilishawahi kuonekana hapo kabla.
Kwahiyo hoja yangu kuu ni kwanini consciousness ya mwanadamu imefungwa ndani ya mfumo unaolazimisha kila kitu kiwe interpreted kupitia past?.
Kwa maana hata physics yenyewe haiwezi kufanya prediction bila kutumia previous observations.
Hakuna formula inayotabiri future kutoka kwenye utupu so lazima ichukue data za kale then ndio ijenge sheria fulani.
Ndio maana nikaja hapa tusaidiane kutafakari kwenye hili eneo, ila pia tujiulize kwa pamoja...
Je, sisi tunajua ukweli wa mambo,
au tunajua tu repetition ya mambo?
Kwasababu hata ukisema universe ni matokeo ya Time + Space + Matter, bado understanding yako ya hivyo vitu vitatu umetengenezewa na historical observation... Au nadanganya mkuu?
Hujawahi kushika future,
umeshika mabaki ya jana kisha ukayatumia kukisia kesho, hivi ndivyo always tunafanya.
So kutokana na Hilo ndio maana nikasema huenda hapo ndio limitation ya akili ya mwanadamu ilipo, ya kwamba haiishi nje ya mfumo wa kumbukumbu, ya kwamba asipokua na kumbukumbu yoyote ya kale kichwani mwake hawezi kuwa kama alivyo sasa.
Ila pia nikasema, sayansi yenyewe ni historia iliyokataa kufa.
Kwa sababu sheria zote za kisayansi ni matukio yaliyotokea mara nyingi sana hadi tukayapa hadhi ya ukweli wa kudumu ila in reality bado msingi wake ni past.
So andiko lote limekaa kutafakari zaidi pasipo kudemand au kutaka kubadili chochote kwenye universe especially dunia ila kwa jinsi mambo yalivyo naona tunaishi past na sasa sio sasa na future.