Embu tutafakari kidogo

Embu tutafakari kidogo

hii inakuwa kama amnesia au unakuwa hujui hata kutembea, kama kuna dunia, kuna watu yani kila kitu
Yeah lakini je, utakua unawaza nini kichwani? Kwasababu huna kumbukumbu zozote za kale... Wanasema kati ya kitu kinachomfanya mtu asiwe bora ni makelele ya nje ndio maana ukiwa katika hali ya utulivu unaweza kuiona future, kwamfano ukiwa umelala ubongo ukiwa haurecall chochote kwenye past ndio wakati ambao unaweza umaota matukio ambayo baadae yanatokea kwa namna ile ile kama ambavyo uliota.

So ile hoja ya mtu kuwa na pande mbili ndio hapo ambapo naonaga inamake sense pia, ila shida ni kujua upande upi uuongoze upande mwingine.
 
Tunazaliwa bila kujua chochote.

Taarifa zote zinazo ingia kwenye ubongo tunazikuta hapahapa duniani kutoka kwa watangulizi wetu.

Hatuwezi kujua tusivyo vijua ila tuna endelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, udadisi na uchunguzi zaidi.
 
Hatari... Watu wa kwanza waliwezaje kuanzisha hizi taratibu? Ni kwamba wao walikua bora kuliko sisi au na wao walikuta baadhi ya info tayari zipo.
 
Yeah lakini je, utakua unawaza nini kichwani? Kwasababu huna kumbukumbu zozote za kale... Wanasema kati ya kitu kinachomfanya mtu asiwe bora ni makelele ya nje ndio maana ukiwa katika hali ya utulivu unaweza kuiona future, kwamfano ukiwa umelala ubongo ukiwa haurecall chochote kwenye past ndio wakati ambao unaweza umaota matukio ambayo baadae yanatokea kwa namna ile ile kama ambavyo uliota.

So ile hoja ya mtu kuwa na pande mbili ndio hapo ambapo naonaga inamake sense pia, ila shida ni kujua upande upi uuongoze upande mwingine.
Duh! Sijawahi kufikiria hii kitu kabisa, nawaza sijui itakuwa ni mbaya au amani kwako
 
Mazingira yenyewe yapo tu.

Wala hayalazimishi mtu kufanya uchunguzi.

Ni sisi binadamu tu, tulikuwa na kiu ya kuchunguza Mazingira.

Ndio maana watu walifanya tafiti na udadisi.
Hakuna utafiti uliofanyika bila sababu, so kwanza mazingira yatakupatia sababu au kukuingiza kwenye mfumo utakaopelekea ufanye utafiti.

Kama ni ugonjwa utaumwa kwanza ili ujue kumbe upo then baada ya hapo ndio utafiti unafuata.

So ni kama mazingira yanaamua ya kwamba now hili linapaswa lijulikane coz ili iwe possible yanakupa sababu za wewe kufanya utafiti.
 
ukiangalia weather ni zile zile maisha tunayoishi ukisoma historia ya watu wa zamani sana kama watu wa Messepotamia utaona ni maisha yale yale mpaka tech walizotumia ni kama tunacopy kwao, mzunguka wa jua unakuwa unatabirika sababu ni una pattern

Ni kama vile kila kitu kinasabibishwa na kitu nyuma yake, ulimwengu wa vitu unaojirudia hakuna mwanzo wala mwisho sababu mwanzo umetokana na mwisho na mwisho umetokana na mwanzo, Big Cycle ya maisha, Ma buddha walijua hizi ishu ndio maana min -me anawakubali sana

Mimi pia nawakubali kinoma.
 
Kuna sehemu mkuu The coder, unasema ulimwengu hautaki tufike level flan ya maarifa, na ukatoa mifano ya sodoma, gharika, nk, kwanini usiwaze kua Kuna utawala mkuu sehemu flani ulimwenguni unaodhibiti hizo Hali, au ukubaliane na watu wa dini wanavyoamini?
 
Ukivuliwa tabaka zote za kumbukumbu ulizozikusanya kwa miaka mingi, ni kitu gani hasa kitabaki kukufanya uwe wewe?

Embu tafakari kwa kina hapa…
Huenda unachokiita akili si chochote zaidi ya maktaba ya mabaki ya jana iliyojificha ndani ya ubongo wako.

Maana mwanadamu haishi kwa kile anachokijua sasa, bali kwa kivuli cha yale yaliyokwisha pita.

Angalia, elimu yako ni marejeo ya kale,

Lugha yako ni mwangwi wa sauti zilizotamkwa kabla yako, Mwendo wako, maamuzi yako, hofu zako, imani zako na hata namna unavyoitazama dunia, vyote vimefungwa kwenye masanduku ya historia yaliyohifadhiwa kichwani mwako.

Ndiyo maana jamii humuita mtu huyu mwenye akili na mwingine asiye na akili kwa kupima ukubwa wa hazina ya marejeo aliyobeba.

Angalia hapa…
Daktari huitwa bingwa kwa sababu amehifadhi simulizi za magonjwa yaliyopita.

Mwanasheria hushinda kesi kwa sababu ameweza kuvuta kivuli cha hukumu za jana na kuzileta leo.

Na ushahidi wenyewe ni nini kama si mabaki ya jambo lililokwisha kufanyika muda uliopita?

Kwa kifupi ni kwamba hakuna hoja inayokubalika bila kupewa kaburi la zamani ili iweze kulalia.

Ndio maana ukisema jambo ambalo halijawahi kutokea, dunia hukutazama kama mwendawazimu. Lakini ukisema jambo ambalo lilishawahi kutokea, hata kama ni la kipuuzi, watu hulipa heshima fulani kwa sababu lina historia.

Ndiyo maana dunia yote inaonekana kana kwamba haiishi kuanzia sasa kwenda mbele, bali inaishi ndani ya makumbusho ya mambo yaliyopita na sasa. Kwasababu kila mfumo umejengwa juu ya ibada ya jana.

Leo hii mtu akikwambia ametoka sehemu unayoifahamu, hutaki kumuamini mpaka akupe alama za kale unazozijua zipo kwenye eneo hilo, akizitoa kwa namna sahihi, unaamini vinginevyo huwezi muamini.

Na hapo ndipo siri kubwa ilipojificha, ya kwamba binadamu haamini ukweli hadi uwe ule unaofanana na kumbukumbu zake au zozote zile za kale.

Na kwa sababu hiyo, sayansi nayo si kitu kingine isipokuwa historia iliyokataa kufa.
Historia ya kawaida huzikwa kwenye jana.

Lakini sayansi ni historia inayojirudia kwa nidhamu maalum hadi watu waiite sheria.

Mfano, mvua ilinyesha jana, ikarudia leo, ikitarajiwa kesho ndio tunasema kuna mfumo wa kisayansi unaoweza kuelezea mvua, kutokana na kujirudia rudia kwa tabia zile zile Kila mvua inapotaka kunyesha, lakini msingi wake bado ni ule ule, kumbukumbu ya yaliyopita.

Ila dunia ikikutana na jambo lisilo na mizizi kwenye jana. Kwa mfano, ugonjwa ambao hauna mfano wowote uliowahi kuwepo, usio na pattern, usiorudia tabia, usiokubali kuhifadhiwa kwenye rekodi.
Ndipo utaona namna akili zote zitakavyosimama pasinakujua wapi waanzie na wapi wamalizie.

Kwa sababu uwezo wa mwanadamu haujazoea kuumba kutoka mwanzo, ila umezoea kurejea kutoka kwenye kile ambacho tayari kilishakuwepo.

Hata AI mnayoihofia leo, haifanyi kazi kwa kuona kesho bali inavuta vipande vya jana na kuvipanga upya ila yenyewe hufanya kwa kasi kubwa kuliko mwanadamu.

Kwahiyo, future ndiyo eneo pekee ambalo akili hushindwa kutawala, ndiyo maana kesho hubaki kuwa fumbo na jana hubaki kuwa mwalimu na kipimo cha werevu.

Ukifaulu mtihani kwa A zote, huenda hukua na akili kuliko wengine bali huenda ulikuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kubeba mizoga ya taarifa za zamani kichwani mwako na hii ikafanya ukaitwa genius kwa sababu uliweza kukariri historia kwa usahihi mkubwa kuliko waliokaa pembeni yako.

Na hapa ndipo dunia ilipojenga mfumo wake wa ulinzi.

Kwamba, ukileta hoja isiyo na kumbukumbu ya zamani, wenye dini watakuambia unakufuru ikiwa imelenga upande huo na ukileta mbele ya wasomi, watakuambia thibitisha.

Na kuthibitisha huko maana yake ni nini?
Wanataka urudi jana ukatafute ushahidi.

Ukishindwa kufanya hivyo, hoja yako hufa kabla hata haijasikilizwa.

Ndiyo maana watu wengi hurudi kwa hiari ndani ya gereza la kawaida la fikra, gereza la historia. Kwa sababu huko hakuna pingamizi na ni sehemu salama ya akili zinazohitaji kivuli cha jana ili ziweze kupumua.

Lakini swali ambalo wengi hawathubutu kujiuliza ni hili…
Je, ni nani aliyeufuma mfumo huu wa kuabudu yaliyopita?

Kwa nini dunia inaonekana kana kwamba inaruhusu kujua kile kilichokwisha kuwepo pekee, na inazuia kufikiri kuhusu kile ambacho hakijawahi kuwepo?

Kana kwamba kuna ukuta usioonekana unaozuia akili kuvuka mipaka ya historia, na dunia pamoja na mifumo yake yote hufanya juu chini kuulinda ukuta huo usionekane.

Na huenda ndio maana hakuna jipya chini ya jua, na si kwa sababu mambo mapya hayawezi kutokea, hapana, bali kwa sababu akili nyingi zimefungwa ndani ya maktaba ya jana kiasi kwamba haziwezi kutambua kile ambacho hakina kumbukumbu.

Imani yangu inaniambia sisi ni bora ya zaidi ya hivi tulivyo, ila ni vile tumefungwa kwenye eneo ambalo halitupi mwanya wa kuona zaidi ya vile ambavyo tunalazimishwa tuvione.

Ndio maana nasema, ukifutiwa kila ulilowahi kujifunza, kila uso uliowahi kuuona, kila neno ulilowahi kusikia… usingebaki na akili bali ungebaki na utupu unaohitaji kufundishwa historia upya ili uweze kuruhusiwa kuishi tena ndani ya mfumo wa dunia kwasababu akili unayohisi uko nayo huna bali imetengenezwa na kuwa shaped kinamna ile dunia inataka iwe.
Ukitoka nje ya solar system tuliyopo.. more far kuna jua lingine na solar sytem nyingine yenye Dunia kama hii na watu kama sisi.

Nje ya hiyo tena kuna nyingine tena na tena.. ukienda north- south, east -west..

Hivyo hii solar sytem yetu ipo ndani ya solar sytem nyingine ambayo na yenyewe ipo ndani solar sytem.. and more …and more like that.

Hivyo MAISHA TUNAYOISHI YALIKUEPO na yataendelea kuepo. Ni mawazo yangu tu.
 
Inawezekana ni sahihi wanachokisema ndio maana labda tupo limited kwenye mambo kadha wa kadha.

Au labda ni asili ya dunia yenyewe tu, kwamba inaamua jambo lipi liwepo jambo lipi lisiwepo katika wakati gani.
 
Mkuu mi nimejiuliza kwa hoja zako hizi wewe unadhani ilipaswa/ulitaka iwaje?. Kwasababu existence ya Ulimwengu ni matokeo ya utumwa wa Time+Space+Matter
 
Hata huo utumwa wa Time + Space + Matter unaonekana kufanya kazi kwa msingi wa kumbukumbu tu.

Kwa maana muda wenyewe hauwezi kueleweka bila kumithirisha kilichopita na kilichopo sasa, vile vile space huwezi kuitambua bila reference ya sehemu nyingine ulizowahi kuziona na matter nayo hupata maana kutokana na patterns ambazo tayari zilishawahi kuonekana hapo kabla.

Kwahiyo hoja yangu kuu ni kwanini consciousness ya mwanadamu imefungwa ndani ya mfumo unaolazimisha kila kitu kiwe interpreted kupitia past?.

Kwa maana hata physics yenyewe haiwezi kufanya prediction bila kutumia previous observations.

Hakuna formula inayotabiri future kutoka kwenye utupu so lazima ichukue data za kale then ndio ijenge sheria fulani.

Ndio maana nikaja hapa tusaidiane kutafakari kwenye hili eneo, ila pia tujiulize kwa pamoja...

Je, sisi tunajua ukweli wa mambo,
au tunajua tu repetition ya mambo?

Kwasababu hata ukisema universe ni matokeo ya Time + Space + Matter, bado understanding yako ya hivyo vitu vitatu umetengenezewa na historical observation... Au nadanganya mkuu?

Hujawahi kushika future,
umeshika mabaki ya jana kisha ukayatumia kukisia kesho, hivi ndivyo always tunafanya.

So kutokana na Hilo ndio maana nikasema huenda hapo ndio limitation ya akili ya mwanadamu ilipo, ya kwamba haiishi nje ya mfumo wa kumbukumbu, ya kwamba asipokua na kumbukumbu yoyote ya kale kichwani mwake hawezi kuwa kama alivyo sasa.

Ila pia nikasema, sayansi yenyewe ni historia iliyokataa kufa.

Kwa sababu sheria zote za kisayansi ni matukio yaliyotokea mara nyingi sana hadi tukayapa hadhi ya ukweli wa kudumu ila in reality bado msingi wake ni past.

So andiko lote limekaa kutafakari zaidi pasipo kudemand au kutaka kubadili chochote kwenye universe especially dunia ila kwa jinsi mambo yalivyo naona tunaishi past na sasa sio sasa na future.
 
Ukitoka nje ya solar system tuliyopo.. more far kuna jua lingine na solar sytem nyingine yenye Dunia kama hii na watu kama sisi.

Nje ya hiyo tena kuna nyingine tena na tena.. ukienda north- south, east -west..

Hivyo hii solar sytem yetu ipo ndani ya solar sytem nyingine ambayo na yenyewe ipo ndani solar sytem.. and more …and more like that.

Hivyo MAISHA TUNAYOISHI YALIKUEPO na yataendelea kuepo. Ni mawazo yangu tu.
Huenda unachokisema ni kweli mkuu, maana ukiangalia kwa umakini utagundua ni almost kila mfumo upo ndani ya mfumo mwingine kisha baada ya hapo hauelewi.

Mfano, solar system ndani ya galaxy, galaxy ndani ya cluster, cluster ndani ya structure mama.

So, kwa mtazamo huo huenda hata hii tunayoiita universe ni chembe ndani ya kitu kingine kikubwa tusichoweza kukiona.

Kwahiyo, maisha tunayoyaona na kuyaishi yanaweza kuwa si tukio jipya kama tunavyodhani bali inawezekana ikawa ni pattern inayojirudia milele katika viwango tofauti vya existence.

Kwa sababu ukiiangalia dunia kwa jicho la kawaida utaona vitu na mambo mengi yanakufa, lakini ukiiangalia kwa jicho la tafakari utaona mambo mengi hayafi bali yanabadilisha tu sura.

Kwamfano, vizazi vinaondoka lakini tabia zilezile zinarudi. , falme zinaanguka lakini mifumo ileile inajengwa tena kwa majina tofauti, teknolojia zinabadilika lakini tamaa, hofu, mapenzi, vita, nguvu, udhaifu na maswali yanabaki yale yale.

Hii inamaanisha nini sasa?, hii inamaanisha kwamba...

Existence yote inaendeshwa na repetition kubwa yenye masks tofauti kila baada ya muda fulani.

Na ukiendelea kutafakari hapo kwenye hoja yako basi utaenda mbali zaidi hadi kuhisi labda sisi sio mwanzo, wala mwisho wa maisha,
bali ni mwendelezo wa pattern ambayo imekuwa ikijirudia kwenye kona tofauti za reality kwa muda usiojulikana.

So ni kama hakuna jambo jipya bali kuna muonekano mpya wa jambo la zamani.

Na kama hii hoja ya kila kitu kunajirudia ni kweli, basi hata sisi pamoja na hiki tunachokiwaza tulishawahi kuwaza hivi katika namna tofauti ila yenye maana hii hii hapo kabla.

Then utamalizia kusema future ni historia ambayo bado hatujaifikia?

Kisha hapo utagundua maisha ni infinity loop ambayo huanzia leo itakayogeuka kuwa jana na kesho itayogeuka kuwa leo katika mtindo wa kujirudia rudia ikiwa zimebebwa na matukio tofauti tofauti ila yenye maana ile ile moja 😅😅.

Anyway, wacha nikalale sasa...
 
Kuna sehemu mkuu The coder, unasema ulimwengu hautaki tufike level flan ya maarifa, na ukatoa mifano ya sodoma, gharika, nk, kwanini usiwaze kua Kuna utawala mkuu sehemu flani ulimwenguni unaodhibiti hizo Hali, au ukubaliane na watu wa dini wanavyoamini?
Noted
 
Back
Top Bottom