Cesar Saint
JF-Expert Member
- Nov 18, 2016
- 423
- 727
Heshima kwenu wakuu;
Katika ulimwengu huu tunaoishi ambao teknolojia ya mawasiliano imekuwa ikipanuka na kushamiri kwa kasi kiasi cha kufanya dunia kuwa kama kijiji kwa kuwaunganisha watu kupitia mitandao (internet) na simu za mkononi (audio calls, video calls, voice messages ,pictures messages) na vingine vingi ambavyo vimekuwa vikiongeza matumizi na mahitaji ya satellite kwa kiwango kikubwa .
Space X kupitia kwa CEO Wake ELON MUSK wanajiandaa kurusha roketi ya Falcon 9 itakayokuwa imebeba satellite mbili za majaribio ya “Global broadband service envisioned “ . Satellite hizi ambazo ni Prototype zinazojulikana kwa majina ya Microsat-2a na Microsat-2b kwa mara ya kwanza ziliwekwa wazi uwepo wake kwa jamii na bwana ELON MUSK kupitia Twitter lisaa limoja kabla ya kuroshwa angani siku ya jumatano ingawa wadadisi wa mambo waliweza kujua kutokana na kujazwa kwa Federal Communication Commission ya Marekani .
Uwepo wa “Starlink" global internet service utamaliza tatizo la ukosefu wa mtandao kwenye sehemu kubwa ya dunia nadhani na kutufanya tuwezaidi ya kijiji hasa kuwa mtaa mmoja .
Leo siku ya jumatano 21/02/2018 walishindwa kurusha kutokana na uwepo wa upepo mkali katika anga la juu sana panapo majaaliwa kesho Alhamisi mambo yakikaa sawia basi Space X watarusha roketi yao hii na kufidia kwa sehemu kubwa gap linaoachwa na hivi visatelite vidogo tulivyonavyo sasa .
Asanteni.