Elishilia Kaaya kumuunga mkono Joshua Nassari mgombea ubunge kupitia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elishilia Kaaya kumuunga mkono Joshua Nassari mgombea ubunge kupitia CHADEMA

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by chachana, Mar 1, 2012.

 1. c

  chachana Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanachama wa CCM wamechoka na sasa imekuwa ni aibu kubwa huko Meru kwa namna vitendo vya kuchafuana vinavyoendelea baina ya wagombea wawili SIOI na SARAKIKYA. Matusi, rushwa, uzushi, mnyukano na kila aina ya siasa zenye upuuzi wa hali ya juu.

  Elishilia kaaya na kambi yake kupitia kwa aliyekua meneja wa kampeni za ndani ya chama kuwa sasa wameamua kumuunga mkono kijana wao Joshua Nassari, "Nassari ni wetu ni mmeru wetu, tunaaamini akishinda atawatumikia wameru". Hii vita ya urais tuwaachie hao hao wasituletee maafa huku.

  Meneja huyo amethibitisha hayo kwa kusema kuwa, hawawaambii wanachama wa CCM meru kuhama chama ila katika mazingira ya ukweli mgombea pekee ambaye ataisaidia meru ni NAssari wa CHADEMA kwa sababu hatatumikia kundi la watu hawa wachafu na hivyo KUATAKA WAMERU WOTE WAMPIGIE KURA JOSHUA NASSARI.

  Elishilia ambaye naye alipigwa dafrao kubwa, amekiri kuwa kwa namna mkutano wa chadema wa kura ya maoni ulivyoendeshwa na kusimamiwa na uongozi wa ngazi husika bila manung'uniko wala shida ni dhahiri kuwa chadema wapo serious, haya mambo mengine ya ukada yanatia gharama za bure. Kaaya amekuwa akijulikana kama kada maarufu wa CCM, amejikuta katika aibu nzito ya kiutu uzima pale ambapo kwa macho yake alikuwa akiona namna siasa chafu za ccm huwa zinachezwa.


  UVCCM, wameapa kuwa asipopitishwa SIOI basi hawatashiriki kampeni za uchaguzi.
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ok yeyote atakayeshinda awasaidie wananchi na sio kutafuta posho
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kama watanzania wote wangeona jinsi hawa jamaa wanavyohangaika kuingia uongozini, basi wangeshtuka na kuachana na CCM mara moja hata wakipewa mabilion, hayawasaidii huko mbeleni.
   
 4. E

  EMMANUEL NSAMBI JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama ni mkambo ya kweli njia ni nyeupe kwa Nasari,ila kama ni ushabiki shindwa na ulegee!
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Tangu awali nilijua mnara wa babeli usingefika mbinguni.
   
 6. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tutaona mengi safari hii ndani ya CCM Arumeru ngoja tusubiri kampen.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  CCM kwa sasa ni kama mgonjwa aliye kwenye harakati za kukata roho...mara atataka mtoto wa kwanza aje, mara atataka mtoto wa mwisho aitwe, mara atataka maji, na madai mengine mengi, kumbe ni mbinu ya kukata roho!
  Mara Sioi si raia, mara Lema alitukana Washili, mara Lowassa KAFANYA HIVI...ni mtiririko wa vituko visivyokuwa na tija na wananchi.
  Hongera sana CDM...Mmeonyesha ukomavu mzuri sana wa kisiasa!
   
 8. mpiganiahaki

  mpiganiahaki Senior Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Maandiko yametimia, ''WASIO PATANA HAWAWEZI KWENDA PAMOJA''
   
 9. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Huu msuguano wa CCM Arumeru umenivutia sana.
  Kamanda NASSARI chukua jimbo.
   
 10. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tunampogeza kama ametambua nyeupe siyo nyeusi, itakuwa vema na haki kama atawafungua na wengine macho.
   
 11. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Safi mkuu.Ila heading inamislead.Tetesi halafu wakati huo imedhibitishwa!!
   
 12. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Hivi hawa jamaa kupigana vikumbo vyote hawajamsikia spika Makinda kuwa bungeni kuna njaa, wabunge wana dhiki hawawezi hata kujenga nyumba, na nusu yao wanataka kuacha kazi hiyo isiyolipa?! Wanagombania dhiki hawa!
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ndani ya CCM kuna vyama vingi sana vya siasa! Tendwa avisajili.
   
 14. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Haiwezekani elishilia atoke ccm , ccm ndo imemfikisha hapo alipo sasa hivi . Na labda anategemea akitoka aicc aende kuwa balozi . Kumuunga mkono nasary ni risk kubwa sana kwake hawezi kufanya hivo kama anaipenda future yake . Huo utakuwa uzushi mnene.
   
 15. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hapo anaangaliwa nani mwenye uwezo wa kuwa na pesa nyingi ndo apite
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Nasari hahitaji Elishiria wala magamba yoyote kupata ushindi, na hapo kwenye red unamaanisha UVCCM gani sasa, maana arusha kuna UVCCM kama laki moja na arobaini elfu!!!

  naona degedege imewakumba walaji na watoaji rushwa
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kamanda, ikiisha ya arumeru tutarudi kwenye hoja yetu na mponda!!!

  CCM inajivua nguo moja baada ya nyingine Arusha, hadi jumatano ijayo watakua uchi wa mnyama!!
   
 18. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280

  Hapo umehitimisha kila kitu, cha kuongezea ni kuwa Hili lichama lilitakiwa livunjwe muda mrefu na viongozi wa CCM. It would have had a dignified end, right now they are heading to a shameful fate, another KANU in the making.
   
 19. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #19
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kaka wewe kuwa mende..........inashtua. Tabia ya mende ni kukaa kwenye mavi..........sasa wewe binadamu ukiwa na tabia za mende..........maana yake tuna utata ni wapi unafanya tendo la ndoa. Kule apendako mende au?
   
 20. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #20
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hivi vurugu zote hizi, vikumbo vyote hivi, mvurugano wote huu ni kutaka kuingia katika ubunge huo ambao Mheshmiwa Speaker amesema ni umasikini? Yaani hawa kina Sioi, Sarakikya sijui nanilii wanagombania kwenda kuwa masikini? Kwamba wao wanaupenda sana umasikini???

  Wapi glasi yangu.!
   
Loading...