Elishilia Kaaya kumuunga mkono Joshua Nassari mgombea ubunge kupitia CHADEMA

Wanachama wa CCM wamechoka na sasa imekuwa ni aibu kubwa huko Meru kwa namna vitendo vya kuchafuana vinavyoendelea baina ya wagombea wawili SIOI na SARAKIKYA. Matusi, rushwa, uzushi, mnyukano na kila aina ya siasa zenye upuuzi wa hali ya juu.

Elishilia kaaya na kambi yake kupitia kwa aliyekua meneja wa kampeni za ndani ya chama kuwa sasa wameamua kumuunga mkono kijana wao Joshua Nassari, "Nassari ni wetu ni mmeru wetu, tunaaamini akishinda atawatumikia wameru". Hii vita ya urais tuwaachie hao hao wasituletee maafa huku.

Meneja huyo amethibitisha hayo kwa kusema kuwa, hawawaambii wanachama wa CCM meru kuhama chama ila katika mazingira ya ukweli mgombea pekee ambaye ataisaidia meru ni NAssari wa CHADEMA kwa sababu hatatumikia kundi la watu hawa wachafu na hivyo KUATAKA WAMERU WOTE WAMPIGIE KURA JOSHUA NASSARI.

Elishilia ambaye naye alipigwa dafrao kubwa, amekiri kuwa kwa namna mkutano wa chadema wa kura ya maoni ulivyoendeshwa na kusimamiwa na uongozi wa ngazi husika bila manung'uniko wala shida ni dhahiri kuwa chadema wapo serious, haya mambo mengine ya ukada yanatia gharama za bure. Kaaya amekuwa akijulikana kama kada maarufu wa CCM, amejikuta katika aibu nzito ya kiutu uzima pale ambapo kwa macho yake alikuwa akiona namna siasa chafu za ccm huwa zinachezwa.

UVCCM, wameapa kuwa asipopitishwa SIOI basi hawatashiriki kampeni za uchaguzi.

Watupishe huko, hatuwataki. Wafu na wazikane!
 
Haiwezekani elishilia atoke ccm , ccm ndo imemfikisha hapo alipo sasa hivi . Na labda anategemea akitoka aicc aende kuwa balozi . Kumuunga mkono nasary ni risk kubwa sana kwake hawezi kufanya hivo kama anaipenda future yake . Huo utakuwa uzushi mnene.

achana na mawazo yaliyomwagiwa tindikali maisha yake na future yake anaijua yeye na hata alipofika ni juhudi zake binafsi ukizoea mbeleko siku ikikatika utajifunga hata mshipi na utaanza maisha mapya ya fikra komavu.
hongera kwa kuachana na magamba na shauri na wengine waige mfano huu.
 
Wanachama wa CCM wamechoka na sasa imekuwa ni aibu kubwa huko Meru kwa namna vitendo vya kuchafuana vinavyoendelea baina ya wagombea wawili SIOI na SARAKIKYA. Matusi, rushwa, uzushi, mnyukano na kila aina ya siasa zenye upuuzi wa hali ya juu.

UVCCM, wameapa kuwa asipopitishwa SIOI basi hawatashiriki kampeni za uchaguzi.

Nashindwa kuelewa hapa. Watu wa rangi za Kijani na Njano wanagombania kwenda Bungeni, na ikiwa Spika toka rangi hizo amesema "kuwa Ubunge siyo dili hauna maana yoyote kutokana na posho ndogo, hata wabunge wengine wanataka kujiuzulu"

Sasa hawa nao wanataka kutoana ROHO kwa kazi ambayo wenyewe wanakili siyo DILI tena.

Tumieni Busara wajameniiiiiiiiiiiiiii!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hivi hawa jamaa kupigana vikumbo vyote hawajamsikia spika Makinda kuwa bungeni kuna njaa, wabunge wana dhiki hawawezi hata kujenga nyumba, na nusu yao wanataka kuacha kazi hiyo isiyolipa?! Wanagombania dhiki hawa!

dhiki aliyonayo makinda tofauti na ya sio na wenginei, bi kiroboto ni kati ya wanawake matajiri tz, alikua anatutia mchanga wa macho, hivi huyu mama si alifunga mtaa wa kutoka kijitonyama kuingia sinza jina la mtaa nimelisahau kisa alikua anapoomosha li nyumba pende ilee, bi kiroboto mnafiki ni wa kuachana nae
 
Wanachama wa CCM wamechoka na sasa imekuwa ni aibu kubwa huko Meru kwa namna vitendo vya kuchafuana vinavyoendelea baina ya wagombea wawili SIOI na SARAKIKYA. Matusi, rushwa, uzushi, mnyukano na kila aina ya siasa zenye upuuzi wa hali ya juu.

Elishilia kaaya na kambi yake kupitia kwa aliyekua meneja wa kampeni za ndani ya chama kuwa sasa wameamua kumuunga mkono kijana wao Joshua Nassari, "Nassari ni wetu ni mmeru wetu, tunaaamini akishinda atawatumikia wameru". Hii vita ya urais tuwaachie hao hao wasituletee maafa huku.

Meneja huyo amethibitisha hayo kwa kusema kuwa, hawawaambii wanachama wa CCM meru kuhama chama ila katika mazingira ya ukweli mgombea pekee ambaye ataisaidia meru ni NAssari wa CHADEMA kwa sababu hatatumikia kundi la watu hawa wachafu na hivyo KUATAKA WAMERU WOTE WAMPIGIE KURA JOSHUA NASSARI.

Elishilia ambaye naye alipigwa dafrao kubwa, amekiri kuwa kwa namna mkutano wa chadema wa kura ya maoni ulivyoendeshwa na kusimamiwa na uongozi wa ngazi husika bila manung'uniko wala shida ni dhahiri kuwa chadema wapo serious, haya mambo mengine ya ukada yanatia gharama za bure. Kaaya amekuwa akijulikana kama kada maarufu wa CCM, amejikuta katika aibu nzito ya kiutu uzima pale ambapo kwa macho yake alikuwa akiona namna siasa chafu za ccm huwa zinachezwa.

UVCCM, wameapa kuwa asipopitishwa SIOI basi hawatashiriki kampeni za uchaguzi.
"Saa ya ukombozi ndio sasa" By Christopher Mtikila
 
Back
Top Bottom