Acha utoto wewe gamba.tatizo sio elimu hapa..tatizo ni kua godbless lema hana personality ya kuongoza jimbo lenye hadhi kama hili la arusha...unaweza kusoma mbaka nywele zika nyonyoka ila ukakosa hekima..hana hekima kabisa.....mie nimemuona kwa macho yangu nilipo kwenda kwenye kilio cha dada mmoja hapa arusha,wakati ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu kwa kupotelewa na msichana mdogo huyu lema akaingia kwenye nyumba yenye msiba.....alipo ingia unaweza sema petrol station inatembea,alikua ananukia breweries ya kutosha..huku watu wakiwa na huzuni kubwa,akasema "jamani msilie sana,ni swala la kuomba tu ili arudi tena dunia,haya jamani tumuombee afufuke"hiyo kauli iliwafanya ndugu wengine marehemu kutoka nje......sasa hii ni kutokua na hadhi ya uongozi!!!
Ni kweli huyu jamaa hajasoma huyu, tunataka viongozi kama akina Kikwete ana Degree ya Uchumi na kaitumia vizuri kutufikisha hapa tulipo.
Elimu ya baadhi ya wabunge wa nchi hii ni vichekesho vitupu.
Elimu ya Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, GODBLESS LEMA aliyoieleza Mahakamani wakati ya kesi inayomkabili kufuatia ushindi wake wa Ubunge jimboni humo ni tofauti kabisa na ile iliyoko kwenye profile yake iliyooneshwa kwenye tovuti ya Bunge. Aidha hakuna ukweli wa moja kwa moja wa CHUO ambacho Mh. huyo mwenye Mbwembwe sana alichosomea.
Lameck wa Rorya ana elimu gani, hata kujenga hoja hajui zaidi ya kuhonga na kuwadanganya wananchi.
Msimbane mbavu mtu kwa elimu ktk kitu ambacho ni haki yake, kwani hata akiwa na elimu ndogo hastaili kuwa mbunge? Haya godbless jonathan lema anaelimu ya msingi (darasa la saba) je, sheria inamzuia kugombea ubunge?
Mbona mimi sioni tatizo la kujadili hapo?.Kwani kavunja sheria gani tena hata kuanzisha mahakama nyingine humu jamvini?.Kwani katiba ya tz inasemaje kuhusu elimu ya mbunge?.Wangapi walikuwa na elimu ya std 7 na wakawa mawaziri enzi za Mwalimu?.Na hata leo wengi ni wabunge lkn std .....?
Wewe elimu yako ikoje???