Elimu ya Godbless Lema utata mtupu

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Elimu ya Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, GODBLESS LEMA aliyoieleza Mahakamani wakati ya kesi inayomkabili kufuatia ushindi wake wa Ubunge jimboni humo ni tofauti kabisa na ile iliyoko kwenye profile yake iliyooneshwa kwenye tovuti ya Bunge. Aidha hakuna ukweli wa moja kwa moja wa CHUO ambacho Mh. huyo mwenye Mbwembwe sana alichosomea.

Hebu tuangalie hii ya bunge ilivyo na utata yenyewe kwanza:

  • Kamaliza darasa la saba 1989 na kuanza kidato cha kwanza kwaka huohuo wa 1989. Je hii inawezekana?
  • Ameanza kidato cha kwanza mwaka 1989 na kumaliza 1991. Je miaka hiyo elimu ya kidato cha nne ilikuwa ni miaka 3 badala ya minne?
  • Amemaliza kidato cha nne mwaka 1991 na mwaka huohuo akaanza kidato cha tano. Je hili liiikuwa linawezekana?
  • Hii Diploma aliyosoma Cambridge College ni ya nini? siasa? uchumi? fundi mchundo? au nini?

Iko haja sasa Sheria ifuate mkondo kwa TCU kukagua CV za Wabunge wetu ili kuepusha Nchi yetu kuingia katika majanga yatakayosababishwa na Wanasiasa wa aina hii.

GENERAL
SalutationHonourableMember picture
1748.jpg
First Name: Godbless
Middle Name:Jonathan
Last Name:Lema
Member Type:Constituency Member
Constituent:Arusha Mjini
Political Party:CHADEMA
Office Location:Box 16531, Arusha
Office Phone: +255 764 150747
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail:
Member Status:
Date of Birth
EDUCATIONS
School Name/Location Course/Degree/Award Start DateEnd DateLevel
Kalangala Primary SchoolPrimary Education19831989PRIMARY
Geita Secondary SchoolO-Level Education19891991SECONDARY
Kolila Secondary SchoolA-Level Education19911993SECONDARY
Cambridge International CollegeDiploma20082010DIPLOMA
Cambridge International CollegeDegree2010TodateNOT COMPLETED
CERTIFICATIONS
Certification Name or TypeCertification No. IssuedExpires
No items on list
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From DateTo Date
The Parliament of TanzaniaMember - Arusha Urban Constituency20102015
PTNChief Executive Officer (CEO)20072008
Tanzania Labour Party, TLPDistrict Secretary General20052008
DENETRIADirector20052008
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/LocationPositionFromTo
Chama Cha Demokrasia na MaendeleoMember of Parliament2010Date
Tanzania Labour Party, TLPDistrict Secretary General20052008
Tanzania Labour Party, TLPCandidate, Member of Parliament2005
PUBLICATIONS
DescriptionPublished Date
Lema Godbless: Msaada wa haraka kutoka katika Biblia, Arusha2008
Godbless Lema: Wisdom Time, Arusha2008
SPECIAL SKILLS
Skill Name or DescriptionYears ExperienceAcquired ThroughSkill Level
No items on list
RECOGNITIONS
Recognition TypeRecognition DateReasonAction TakenIssued by
No items on list
 
Elimu ya Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, GODBLESS LEMA aliyoieleza Mahakamani wakati ya kesi inayomkabili kufuatia ushindi wake wa Ubunge jimboni humo ni tofauti kabisa na ile iliyoko kwenye profile yake iliyooneshwa kwenye tovuti ya Bunge. Aidha hakuna ukweli wa moja kwa moja wa CHUO ambacho Mh. huyo mwenye Mbwembwe sana alichosomea.

kwa hiyo?
 
Wewe elimu yako ikoje???
 
Lema, wakili ‘wapigana vijembe’ mahakamani Send to a friend
Wednesday, 14 March 2012 19:14
Peter Saramba, Arusha
VIJEMBE na malumbano kati ya shahidi wa kwanza wa upande wa utete, Godbless Lema na wakili , Alute Mughwai anayewawakilisha wadai katika kesi kupinga matokeo ya ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini, ni miongoni mwa mambo yaliyotawala ukumbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha jana.

Hali hiyo ilimlazimisha Jaji Gabriel Rwakibarila, kuingilia kati mara kwa mara na kutoa muongozo ili kuokoa muda wa mahakama.

Malumbano hayo yalisababishwa na aina ya maswali kutoka kwa wakili Mughwai na majibu ya Lema ambaye ni Mbunge wa Arusha Mjini na ambaye ni mdaiwa wa kwanza katika shauri hilo lililofunguliwa na wapiga kura watatu.

Walalamikaji hao ni, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo wanaoimba mahakama, kutengua ushindi wa Lema kwa madai kuwa alitumia maneno ya kashfa na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian.

Baadhi ya hoja zilizozua malumbano kati ya wakili na shahidi huyo ni pamoja na hatua ya Mughwai kuhoji kama shahidi anajua mila na desturi za kabila la Waarusha (Wamaasai) na Wachagga zinazowabagua wanawake katika nafasi za uongozi wa kimila na zile za kupigiwa kura

“Mimi siyo kiongozi wa kimila, bali ni kiongozi wa kisiasa na kiserikali, hivyo sijui mila na desturi za uongozi wa kimila za jamii ya Waarusha, Wamaasai na Wachagga. Kwa nafasi yangu ya ubunge mimi ni kiongozi wa makabila yote yaliyoko katika Jimbo la Arusha Mjini wakiwemo Wanyaturu na wewe (wakili Mughwai),”

Akijibu swali kuhusu sababu za kutokuwapo kwa mwanamke aliyewahi kuchaguliwa kushika nafasi ya ubunge katika wilaya za jamii ya Waarusha, Lema alidai wengi wamejitokeza kugombea akiwamo mgombea wa Chadema aliyegombea katika Jimbo la Longido lakini hawakuchaguliwa.

Alisema wanawake hao hakuchaguliwa katika kura za jumla au kura za maoni ndani ya vyama kama ilivyotokea kwa wakili huyo aliyeshindwa kwenye katika kura za maoni ndani ya CCM katika Jimbo la Singida Mashariki.
“Baadhi walishindwa kwenye kura za maoni kama wewe ulivyoshindwa kule Singida Mashariki. Wengine walishinda kura za maoni lakini hawakuchaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa Dk Burian hapa Arusha,” alidai Leman na kufanya wasikilizaji kuangua kicheko.

Shahidi huyo aliendelea kumrushia maneno wakili Mughwai baada ya kudai kuwa amedanganywa na wateja wake kwa kumweleza kuwa aliomba Dk Burian asichaguliwe kwa sababu siyo mkazi wa Arusha.

Alidai kuwa kisheria, Mtanzania yeyote ana haki ya kugombea ubunge katika jimbo lolote bila kujali ukazi wala asili yake ya kuzaliwa.

“Kwamba nilisema Dk Burian asichaguliwe kwa sababu ni mkazi wa Zanzibar ni hoja ya uwongo na mufilisi, wateja wako wamekudanganya sana kuhusu hilo kwa sababu hoja hiyo isingefanya asichaguliwe ndiyo maana mimi ni mchaga wa Hai, Kilimanjaro lakini nimegombea Arusha na kushinda na leo ni mbunge wako,” alidai Lema.
Kauli ya kudanganywa na wateja wake, ilionekana kumkera wakili Mughwai na kuamua kumuonya kwa mara nyingine sahidi huyo kuacha tabia ya kumpiga misumari kwa kumrushia maneno, badala yake ajibu maswali anayomuuliza.

“Kwa mara nyingine nakuonya usinipige misumari kwa kunirushia maneno. Wewe jibu maswali yangu,” alisema wakili Mughwai.

Wakili Mughwai anayesaidiana na Modest Akida kuwakilisha wadai katika shauri hilo, aliingia kwenye malumbano mengine na Lema alipomzuia kumalizia kukariri maneno yake kuhusu mikopo kwa wanawake, aliyoyatamka katika mikutano yake ya kampeni kitendo kilichomfanya shahidi kukataa kujibu swali lake hadi atakapomaliza kukariri maneno yote.

Kitendo hicho kilichomfanya Jaji Rwakibarila kuingilia kati na kumruhusu amalizie.
Lakini alipoanza kukariri maneno hayo, kuhusu taratibu ngumu za mikopo kwa wanawake, wakili Mughwai aliingilia kati na kumtaka ajirejeshe nyuma na kuzungumza kama vile anahutubia mkutano wa hadhara mwaka 2010, kitendo kilichomfanya mbunge huyo kuanza kwa kauli mbiu na salama ya Chadema ya ‘Peoples’ huku wasikilizaji wakiitikia power….

“Hapana, hapana, hiyo ya peoples’ power acha kwa sababu muda hautoshi, rudia tu maneno yako kuhusu mikopo kwa akina mama kwa kukariri maneno halisi uliyoyatamka kwenye mikutano yako ya kampeni kuhusu hoja hiyo,” alisema wakili Mughwai akimkatisha Lema.

Awali hoja kuhusu utata juu ya elimu ya mbunge huyo iliibuka baada ya wakili Mughwai kuhoji taarifa zake za elimu zilizopo katika kumbukumbu za nyaraka za bunge, hoja iliyojibiwa na shahidi huyo kuwa imetokana na makosa ya uchapaji uliosababishwa na Bunge lenyewe akidai tayari aliiandikia ofisi ya Bunge kuelezea hilo na kutaka marekebisho.
 
Elimu ya Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, GODBLESS LEMA aliyoieleza Mahakamani wakati ya kesi inayomkabili kufuatia ushindi wake wa Ubunge jimboni humo ni tofauti kabisa na ile iliyoko kwenye profile yake iliyooneshwa kwenye tovuti ya Bunge. Aidha hakuna ukweli wa moja kwa moja wa CHUO ambacho Mh. huyo mwenye Mbwembwe sana alichosomea.

WanaJF, kuna utata mkubwa sana wa taarifa za wabunge zilizopo katika kumbukumbu za bunge. Nadhani ni uzembe wa kitengo cha uchapaji unaoendekezwa na bunge lenyewe. Kwanza hawana utamaduni wa ku update profile za wabunge.

Hata hivyo kuna baadhi ya wabunge wameshatoa taarifa juu ya kukosewa kwa taarifa zao, na bado kitengo hicho kimeshindwa kufanya marekebisho muafaka. Hivyo taarifa nyingi zinazohusu wasifu wa wabunge kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge sio RELIABLE
 
Unachosema ni kweli ila kwa Profesa Maji marefu kuishia darasa la saba ni taarifa sahihi hakuna walipokosea na wala hakuna makosa ya uchapaji.
 
WanaJF, kuna utata mkubwa sana wa taarifa za wabunge zilizopo katika kumbukumbu za bunge. Nadhani ni uzembe wa kitengo cha uchapaji unaoendekezwa na bunge lenyewe. Kwanza hawana utamaduni wa ku update profile za wabunge.

Hata hivyo kuna baadhi ya wabunge wameshatoa taarifa juu ya kukosewa kwa taarifa zao, na bado kitengo hicho kimeshindwa kufanya marekebisho muafaka. Hivyo taarifa nyingi zinazohusu wasifu wa wabunge kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge sio RELIABLE

Ni kweli mkuu manake kila ukipitia hizo profile za wabunge unakuta ni vituko vitupu. Sijui kwa nini walijitutumua na kuanza kuweka hizo information.

Reliability ya Bunge lenyewe nayo inakuwa in stake!!
 
WanaJF, kuna utata mkubwa sana wa taarifa za wabunge zilizopo katika kumbukumbu za bunge. Nadhani ni uzembe wa kitengo cha uchapaji unaoendekezwa na bunge lenyewe. Kwanza hawana utamaduni wa ku update profile za wabunge.

Hata hivyo kuna baadhi ya wabunge wameshatoa taarifa juu ya kukosewa kwa taarifa zao, na bado kitengo hicho kimeshindwa kufanya marekebisho muafaka. Hivyo taarifa nyingi zinazohusu wasifu wa wabunge kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge sio RELIABLE

Kama kweli chombo chetu cha kutunga sheria kinaendeshwa hivyo as if bado tuko kwenye STONE AGE basi hii ni hatari. Vijana wa IT wamejaa mitaani na hii kazi ya kuboresha WEBSITE YA BUNGE na kuifanya USER FRIENDLY wanaweza kuifanya tena kwa ujira mdogo. Kwanini MBUNGE asipewa USER NAME AND PASSWORD akawa na access na maelezo yake including CV yake kwenye website ya Bunge akawa na UWEZO wa kui UP DATE kila mara atakapoona inafaa. Jamani hili lina ugumu gani?

No wonder wakati akina Zitto wanatumia Ipode kuwakilisha bajeti bungeni, bado akina Mkulo and co wanatumia mtindo wa KIJIMA wa KULAMBA MAKARATASI. Hawa wazee inabidi tuwapige chini hawawezi kutupeleka popote uwezo wao wa kufikiri umeshafikia mwisho.
 
hao wenye madegree wametufikisha wapi??! Acheni kulalama na majungu acheni jamani,andrew chenge na elimu yake anamchango gani kwenye hili taifa zaidi ya hasara inayoligharimu taifa kwa miaka nendarudi.lema amekaa kwenye ubunge muda mchache tu alakini arusha lami zimeanza kujengwa karibu mitaa yote.hilo la elimu mimi siliafiki kabisa,nimrod mkono ni msomi tena wa havad university alakini ni mwizi na anatumia ujanja ujanja tu kaliibia taifa na kudhulumu watoto wetu wasipate elimu.ushabiki wa kipumbavu acheni jamani.
 
Kama kweli chombo chetu cha kutunga sheria kinaendeshwa hivyo as if bado tuko kwenye STONE AGE basi hii ni hatari. Vijana wa IT wamejaa mitaani na hii kazi ya kuboresha WEBSITE YA BUNGE na kuifanya USER FRIENDLY wanaweza kuifanya tena kwa ujira mdogo. Kwanini MBUNGE asipewa USER NAME AND PASSWORD akawa na access na maelezo yake including CV yake kwenye website ya Bunge akawa na UWEZO wa kui UP DATE kila mara atakapoona inafaa. Jamani hili lina ugumu gani?

No wonder wakati akina Zitto wanatumia Ipode kuwakilisha bajeti bungeni, bado akina Mkulo and co wanatumia mtindo wa KIJIMA wa KULAMBA MAKARATASI. Hawa wazee inabidi tuwapige chini hawawezi kutupeleka popote uwezo wao wa kufikiri umeshafikia mwisho.

kwenye red spelling mistake ni Ipod na huwezi kutumia Ipod kuwakilisha bajeti alitumia Ipad
 
Elimu ya Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, GODBLESS LEMA aliyoieleza Mahakamani wakati ya kesi inayomkabili kufuatia ushindi wake wa Ubunge jimboni humo ni tofauti kabisa na ile iliyoko kwenye profile yake iliyooneshwa kwenye tovuti ya Bunge. Aidha hakuna ukweli wa moja kwa moja wa CHUO ambacho Mh. huyo mwenye Mbwembwe sana alichosomea.

Mbona kweli itadhihiri tu.... jamaa ajiandae kuumbuka
 
Elimu ya Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, GODBLESS LEMA aliyoieleza Mahakamani wakati ya kesi inayomkabili kufuatia ushindi wake wa Ubunge jimboni humo ni tofauti kabisa na ile iliyoko kwenye profile yake iliyooneshwa kwenye tovuti ya Bunge. Aidha hakuna ukweli wa moja kwa moja wa CHUO ambacho Mh. huyo mwenye Mbwembwe sana alichosomea.
Ni kweli huyu jamaa hajasoma huyu, tunataka viongozi kama akina Kikwete ana Degree ya Uchumi na kaitumia vizuri kutufikisha hapa tulipo.
 
Hebu niwekeni sawa wana JF, kwani daraza la saba na Form four huwezi kuwa mbunge???
Na kama nimeishia form four na profile ya bunge inasema STD 7 ni kosa la nani??
 
Back
Top Bottom