Elimu ya Godbless Lema utata mtupu

Elimu ya Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, GODBLESS LEMA aliyoieleza Mahakamani wakati ya kesi inayomkabili kufuatia ushindi wake wa Ubunge jimboni humo ni tofauti kabisa na ile iliyoko kwenye profile yake iliyooneshwa kwenye tovuti ya Bunge. Aidha hakuna ukweli wa moja kwa moja wa CHUO ambacho Mh. huyo mwenye Mbwembwe sana alichosomea.

So what!
 
Hebu niwekeni sawa wana JF, kwani daraza la saba na Form four huwezi kuwa mbunge???
Na kama nimeishia form four na profile ya bunge inasema STD 7 ni kosa la nani??

Mkubwa!

Huyu thatha yaelekea ana lake na hii thread
Na ni mtumwa wa kufa mtu kwa hawa mafisadi.
Hawana tofauti na lile group lake la Rejao, ms,,,,,,,na wengine kama yeye.

Swali.
mwinyi,mkapa,jk na mawaziri wao mafisadi pamoja na elimu zao wametufanyia nini?
Kama siyo wezi mtupu tu?
 
hapa suala la msingi ni kesi juu tya ubunge wala haliusiani na elimu.hata kama anaelimu ya chekechea lakini anaweza kuonoza na tumemkubali mpaka kamtoa wakili jasho basi inatosha.
 
Kama sijakosea ili kuwa mbunge wa TZ inatakiwa uwe raia halali umri kuanzia 18yrs ujue kusoma na kuandikausiwe ulikwisha hukumiwa kwa kosa la jinai----mengine tusaidieni wengi sana humu hatuelewi zaidi ya kupiga kelele urithi mwingine tuliojaaliwa na mwenyezi MUNGU
 
Kwani niulize ndugu zangu wana Jamii Forums, Elimu anayotakiwa kuwa nayo Mbunge ni ipi??maana naona kama tuna make so much of a big issue kuhusu Elimu za wawakilishi wetu.Kama mtu ana elimu ndogo ya darasani lakini anatuwakilisha vizuri sio tatizo, maana wapo wenye elimu kubwa zenye distinction lakini hawana wanachotusaidia zaidi ya kutufanya tunazidi kuwa maskini. Nchi yetu ina rasilimali za kutosha lakini wawakilishi wetu waliosoma hakuna wanachotusaidia zaidi ya kujisaidia wao binafsi.Let's be serious and concentrate on key issues ambazo zitatukomboa kutoka kwenye umaskini na ukoloni mambo leo. Tuliukataa ukoloni lakini sasa tumeurudisha kwa mlango wa nyuma, nadhani ni muhimu zaidi.Ahsanteni kwa kunielewa.
 
ni miaka 21 mkuu
 
Elimu ya Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, GODBLESS LEMA aliyoieleza Mahakamani wakati ya kesi inayomkabili kufuatia ushindi wake wa Ubunge jimboni humo ni tofauti kabisa na ile iliyoko kwenye profile yake iliyooneshwa kwenye tovuti ya Bunge. Aidha hakuna ukweli wa moja kwa moja wa CHUO ambacho Mh. huyo mwenye Mbwembwe sana alichosomea.

Thatha kwani hujui kazi yake ya awali? haihitaji elimu ile!
 
Kuna Pro-Chadema mmoja aliniambia Lema, ana Bachelor of Laws alichukuwa pale University of Dar es Salaam.
 
Nani sasa amesoma sana kwenye hizi siasa za TZ? Mbona kama wote wanafanana...ni kama hawajasoma vile
 
Lema bana eti kasoma Camridge International College ajasema Camridge ya wapi Austaralia au Uingereza kweli dunia na uwanja wa fujo.
 
Huhitaji elifu ya chuo kikuu kujua kuwa LEMA ni mbumbumbu kwa kuwa we fuatilia kauli zake uajua ninamaaniahsa nini!
 
Hii thread yako haina mashiko hasa kwa hali ya sasa ya mtanzania ilivyo,awe ni darasa la saba,ngumbaru au level ya PHD Lema ni mbunge mteule wa Arusha mjini! Msubiri Ngongo mkereketwa wa Lema atakusaidia
 
Kuna Pro-Chadema mmoja aliniambia Lema, ana Bachelor of Laws alichukuwa pale University of Dar es Salaam.

Kaka hili changa la macho, credit zake za form IV hazimruhusu kugusa MLIMANI, hata kuwa mfagiaji wa mabweni hawezi, ni udhalilishaji kusema lema kasoma MLIMANI na uombe msamaha.
 
WanaJF, kuna utata mkubwa sana wa taarifa za wabunge zilizopo katika kumbukumbu za bunge. Nadhani ni uzembe wa kitengo cha uchapaji unaoendekezwa na bunge lenyewe. Kwanza hawana utamaduni wa ku update profile za wabunge.

Hata hivyo kuna baadhi ya wabunge wameshatoa taarifa juu ya kukosewa kwa taarifa zao, na bado kitengo hicho kimeshindwa kufanya marekebisho muafaka. Hivyo taarifa nyingi zinazohusu wasifu wa wabunge kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge sio RELIABLE

Naona wewe unasimama kama wakili wa kumtetea lema katika hili. Hapa hatoki wengine tumemshudia jinsi shule yake ilivyo ya kimagumashi. Hiyo niyo hali halisi ya elimu ya Lema. Kasoma wapi? wakati amekulia hapa hapa arusha na garage bubu zake za magari ambazo zilikuwa vitovu vya biashara haramu ya Magari ya Wizi?. Sijawahi kumuona Lema akisoma hata ilie novel ndogo kabisa ya "MABALA THE FARMER".
 
Kwani niulize ndugu zangu wana Jamii Forums, Elimu anayotakiwa kuwa nayo Mbunge ni ipi??maana naona kama tuna make so much of a big issue kuhusu Elimu za wawakilishi wetu.Kama mtu ana elimu ndogo ya darasani lakini anatuwakilisha vizuri sio tatizo, maana wapo wenye elimu kubwa zenye distinction lakini hawana wanachotusaidia zaidi ya kutufanya tunazidi kuwa maskini. Nchi yetu ina rasilimali za kutosha lakini wawakilishi wetu waliosoma hakuna wanachotusaidia zaidi ya kujisaidia wao binafsi.Let's be serious and concentrate on key issues ambazo zitatukomboa kutoka kwenye umaskini na ukoloni mambo leo. Tuliukataa ukoloni lakini sasa tumeurudisha kwa mlango wa nyuma, nadhani ni muhimu zaidi.Ahsanteni kwa kunielewa.

Kwa hiyo suluhisho ni kuwaweka wasiyo na elimu?
 
elimu kwangu sio hoja, hoja katumiaje wadhifa wake kutatua kero za wananchi waliomchagua.

wananchi wangekuwa wanatoa kura kwa kiwango cha elimu aliyonayo mgombea na akatoa taarifa zisizo sahihi wananchi wakampigia kura kwa taarifa hizo hapo ingekuwa issue!

otherwise hoja haina mashiko zaidi ya majungu na pangu pakavu***
 
Hii thread yako haina mashiko hasa kwa hali ya sasa ya mtanzania ilivyo,awe ni darasa la saba,ngumbaru au level ya PHD Lema ni mbunge mteule wa Arusha mjini! Msubiri Ngongo mkereketwa wa Lema atakusaidia

Unafikiri watu wenye sura kama ya kwako wanaweza kutafakari zaidi ya hapo ulipoishia? Sura kama hilzo kazi yake ni kuwapagawisha less minded kama akina Lema ili wajione wako juu ya dunia.
 
Kuna watu wameweka mbele vyama utadhani sijui kitu gani yaani wamekuwa MISUKULE ya vyama.Hao hao ambao wako mbele kutaka cv za watu wasio wa vyama vyao,ikija kwenye chama anachoshabikia anageuka,yale yale ya CCM kuabudu chama,na hiyo sio sifa ya mleta mabadiliko hata siku moja.

Ukweli ni kwamba Lema ni mbabaishaji,hata ukimsikiliza akiongea.
 
Back
Top Bottom