Elimu ya Godbless Lema utata mtupu

Kwenye misiba utani ni kitu cha kawaida sana,huwezi jua kama anautani na ukoo huo au anautani na kabila hilo.

ukoo ndo ulie mshangaa,ingekua utani nisinge poteza mdaa kuandika....huyo alikua na uchuu sana wa madaraka na ndomana ubunge wake mwenyewe unamdhuru!!
 
Kwenye misiba utani ni kitu cha kawaida sana,huwezi jua kama anautani na ukoo huo au anautani na kabila hilo.

ukoo ndo ulie mshangaa,ingekua utani nisinge poteza mdaa kuandika....huyo alikua na uchuu sana wa madaraka na ndomana ubunge wake mwenyewe unamdhuru!!
 
wenye Elimu kubwa mbona ndiyo wezi wakubwa. Hata kama hajasoma watamchagua tena tu na safari hii ccm itajuuuuuta kurudia uchaguzi Arusha mjini maanake wanazidi kuongeza chuki ndani ya jamii dhidi yao. Mimi nakaa pembeni natazama huo mpambano maanake Arusha huwezezi mwambia mtu kuhusu CCM akakuelewa. Sijui watakuja na mbinu gani? Elimu nini bana sisi tunataka maendeleo tu na siyo vinginevyo
:rockon:[/QUOT
tatizo sio kuangalia yupi ataiba na yupi hawezi,tatizo kubwa ni je tukiibiwa tutajua kama tumeibiwa??tuna elimu ya kutosha juu ya nchi yetu....usifkiri viongozi wa nchi zilio endelea hawapendi kuiba,wanataka ila haiwekani kwakua wanamchii wana elimu ya kutosha juu ya nchi yao,wana wabana kila sekta!!!
 
unajua kuna watu kama mwenye thread hii ndiyo type ya watu tulionao ccm na serikalini for that matter,elimu na uongozi wapi
?wangapi wana ma degree wanashindwa kuendesha nyumba zao utalinganisha na Lema,acheni hizo naona mna hamu ya harufu ya damu,ndiyo jibu pekee kwa Tanzania,Mungu ibariki Tanzania
 
Viongozi wote wa serikali wamesoma, lakini ni nini wanachofanya? We dont care about elimu,
 
Lema, wakili ‘wapigana vijembe’ mahakamani Send to a friend
Wednesday, 14 March 2012 19:14
Peter Saramba, Arusha
VIJEMBE na malumbano kati ya shahidi wa kwanza wa upande wa utete, Godbless Lema na wakili , Alute Mughwai anayewawakilisha wadai katika kesi kupinga matokeo ya ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini, ni miongoni mwa mambo yaliyotawala ukumbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha jana.

Hali hiyo ilimlazimisha Jaji Gabriel Rwakibarila, kuingilia kati mara kwa mara na kutoa muongozo ili kuokoa muda wa mahakama.

Malumbano hayo yalisababishwa na aina ya maswali kutoka kwa wakili Mughwai na majibu ya Lema ambaye ni Mbunge wa Arusha Mjini na ambaye ni mdaiwa wa kwanza katika shauri hilo lililofunguliwa na wapiga kura watatu.

Walalamikaji hao ni, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo wanaoimba mahakama, kutengua ushindi wa Lema kwa madai kuwa alitumia maneno ya kashfa na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian.

Baadhi ya hoja zilizozua malumbano kati ya wakili na shahidi huyo ni pamoja na hatua ya Mughwai kuhoji kama shahidi anajua mila na desturi za kabila la Waarusha (Wamaasai) na Wachagga zinazowabagua wanawake katika nafasi za uongozi wa kimila na zile za kupigiwa kura

“Mimi siyo kiongozi wa kimila, bali ni kiongozi wa kisiasa na kiserikali, hivyo sijui mila na desturi za uongozi wa kimila za jamii ya Waarusha, Wamaasai na Wachagga. Kwa nafasi yangu ya ubunge mimi ni kiongozi wa makabila yote yaliyoko katika Jimbo la Arusha Mjini wakiwemo Wanyaturu na wewe (wakili Mughwai),”

Akijibu swali kuhusu sababu za kutokuwapo kwa mwanamke aliyewahi kuchaguliwa kushika nafasi ya ubunge katika wilaya za jamii ya Waarusha, Lema alidai wengi wamejitokeza kugombea akiwamo mgombea wa Chadema aliyegombea katika Jimbo la Longido lakini hawakuchaguliwa.

Alisema wanawake hao hakuchaguliwa katika kura za jumla au kura za maoni ndani ya vyama kama ilivyotokea kwa wakili huyo aliyeshindwa kwenye katika kura za maoni ndani ya CCM katika Jimbo la Singida Mashariki.
“Baadhi walishindwa kwenye kura za maoni kama wewe ulivyoshindwa kule Singida Mashariki. Wengine walishinda kura za maoni lakini hawakuchaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa Dk Burian hapa Arusha,” alidai Leman na kufanya wasikilizaji kuangua kicheko.

Shahidi huyo aliendelea kumrushia maneno wakili Mughwai baada ya kudai kuwa amedanganywa na wateja wake kwa kumweleza kuwa aliomba Dk Burian asichaguliwe kwa sababu siyo mkazi wa Arusha.

Alidai kuwa kisheria, Mtanzania yeyote ana haki ya kugombea ubunge katika jimbo lolote bila kujali ukazi wala asili yake ya kuzaliwa.

“Kwamba nilisema Dk Burian asichaguliwe kwa sababu ni mkazi wa Zanzibar ni hoja ya uwongo na mufilisi, wateja wako wamekudanganya sana kuhusu hilo kwa sababu hoja hiyo isingefanya asichaguliwe ndiyo maana mimi ni mchaga wa Hai, Kilimanjaro lakini nimegombea Arusha na kushinda na leo ni mbunge wako,” alidai Lema.
Kauli ya kudanganywa na wateja wake, ilionekana kumkera wakili Mughwai na kuamua kumuonya kwa mara nyingine sahidi huyo kuacha tabia ya kumpiga misumari kwa kumrushia maneno, badala yake ajibu maswali anayomuuliza.

“Kwa mara nyingine nakuonya usinipige misumari kwa kunirushia maneno. Wewe jibu maswali yangu,” alisema wakili Mughwai.

Wakili Mughwai anayesaidiana na Modest Akida kuwakilisha wadai katika shauri hilo, aliingia kwenye malumbano mengine na Lema alipomzuia kumalizia kukariri maneno yake kuhusu mikopo kwa wanawake, aliyoyatamka katika mikutano yake ya kampeni kitendo kilichomfanya shahidi kukataa kujibu swali lake hadi atakapomaliza kukariri maneno yote.

Kitendo hicho kilichomfanya Jaji Rwakibarila kuingilia kati na kumruhusu amalizie.
Lakini alipoanza kukariri maneno hayo, kuhusu taratibu ngumu za mikopo kwa wanawake, wakili Mughwai aliingilia kati na kumtaka ajirejeshe nyuma na kuzungumza kama vile anahutubia mkutano wa hadhara mwaka 2010, kitendo kilichomfanya mbunge huyo kuanza kwa kauli mbiu na salama ya Chadema ya ‘Peoples’ huku wasikilizaji wakiitikia power….

“Hapana, hapana, hiyo ya peoples’ power acha kwa sababu muda hautoshi, rudia tu maneno yako kuhusu mikopo kwa akina mama kwa kukariri maneno halisi uliyoyatamka kwenye mikutano yako ya kampeni kuhusu hoja hiyo,” alisema wakili Mughwai akimkatisha Lema.

Awali hoja kuhusu utata juu ya elimu ya mbunge huyo iliibuka baada ya wakili Mughwai kuhoji taarifa zake za elimu zilizopo katika kumbukumbu za nyaraka za bunge, hoja iliyojibiwa na shahidi huyo kuwa imetokana na makosa ya uchapaji uliosababishwa na Bunge lenyewe akidai tayari aliiandikia ofisi ya Bunge kuelezea hilo na kutaka marekebisho.



........ Lakini alipoanza kukariri maneno hayo, kuhusu taratibu ngumu za mikopo kwa wanawake, wakili Mughwai aliingilia kati na kumtaka ajirejeshe nyuma na kuzungumza kama vile anahutubia mkutano wa hadhara mwaka 2010, kitendo kilichomfanya mbunge huyo kuanza kwa kauli mbiu na salama ya Chadema ya ‘Peoples’ huku wasikilizaji wakiitikia power….


Kipande hiki kimenifurahisha sana yaani inabidi wakili achanganyikiwe. Kweli Lema wewe noma
 
unataka kusema wizi wa viongozi wa ccm unahitaji degree kuelewa,waache ccm kaburi lake lipo arusha,kama walivyoenda kuuwa azimio la arusha zanzibar,nao wanafia arusha,Chadema hata wakaweka jiwe na mgombea wa ccm pale arusha jiwe litapata kura nyingi wantafuta pa kufujia pesa za walala hoi
 
wekeni ushabiki chini,bunge hawako makini kwa taarifa za hakika hakuna mbunge anayeambatanisha cv yake na vivuli vya vyeti,hivyo unaweza kusema chochote wakakubali then ni haki yetu kujua elimu na wasifu wa viongozi wetu
 
Inawezekana kusoma elimu ya sekondari kwa miaka miwili achana na mitatu, ni kwa njia ya watahiniwa huru. Na kama unaweza kufanya mtihani kama mtahiniwa huru unaweza kuanza maandalizi hata ukiwa darasa la 7. Tatizo ni kama alisoma formal school, ila kama ni alifanya kama mtahiniwa huru inawezekana. fanya utafiti kidogo.
 
tunaangalia uwezo wa mtu katika uongozi na si elimu ya mtu katika uongozi, babu zetu hawajui hata kusoma lakini wametuongoza kwa busara
 
Jamani naomba ieleweke swala hapa sio elimu bali perfomance wangapi wana elimu mbovu duniani but very strategic matajiri wangapi tunawajua no elimu lakini mabo safi. Sioni sababu tya kucomment elimu kama mtu anafanya kazi ipasavyo. Utasemaje kuhusu wanaotukana alafu mwisho wanaomba msamaha kana kwamba hukujua unatukana.
Elimu ya Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, GODBLESS LEMA aliyoieleza Mahakamani wakati ya kesi inayomkabili kufuatia ushindi wake wa Ubunge jimboni humo ni tofauti kabisa na ile iliyoko kwenye profile yake iliyooneshwa kwenye tovuti ya Bunge. Aidha hakuna ukweli wa moja kwa moja wa CHUO ambacho Mh. huyo mwenye Mbwembwe sana alichosomea.

Hebu tuangalie hii ya bunge ilivyo na utata yenyewe kwanza:

  • Kamaliza darasa la saba 1989 na kuanza kidato cha kwanza kwaka huohuo wa 1989. Je hii inawezekana?
  • Ameanza kidato cha kwanza mwaka 1989 na kumaliza 1991. Je miaka hiyo elimu ya kidato cha nne ilikuwa ni miaka 3 badala ya minne?
  • Amemaliza kidato cha nne mwaka 1991 na mwaka huohuo akaanza kidato cha tano. Je hili liiikuwa linawezekana?
  • Hii Diploma aliyosoma Cambridge College ni ya nini? siasa? uchumi? fundi mchundo? au nini?

Iko haja sasa Sheria ifuate mkondo kwa TCU kukagua CV za Wabunge wetu ili kuepusha Nchi yetu kuingia katika majanga yatakayosababishwa na Wanasiasa wa aina hii.

GENERAL
SalutationHonourableMember picture
1748.jpg
First Name: Godbless
Middle Name:Jonathan
Last Name:Lema
Member Type:Constituency Member
Constituent:Arusha Mjini
Political Party:CHADEMA
Office Location:Box 16531, Arusha
Office Phone: +255 764 150747
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail:
Member Status:
Date of Birth
EDUCATIONS
School Name/Location Course/Degree/Award Start DateEnd DateLevel
Kalangala Primary SchoolPrimary Education19831989PRIMARY
Geita Secondary SchoolO-Level Education19891991SECONDARY
Kolila Secondary SchoolA-Level Education19911993SECONDARY
Cambridge International CollegeDiploma20082010DIPLOMA
Cambridge International CollegeDegree2010TodateNOT COMPLETED
CERTIFICATIONS
Certification Name or TypeCertification No. IssuedExpires
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From DateTo Date
The Parliament of TanzaniaMember - Arusha Urban Constituency20102015
PTNChief Executive Officer (CEO)20072008
Tanzania Labour Party, TLPDistrict Secretary General20052008
DENETRIADirector20052008
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/LocationPositionFromTo
Chama Cha Demokrasia na MaendeleoMember of Parliament2010Date
Tanzania Labour Party, TLPDistrict Secretary General20052008
Tanzania Labour Party, TLPCandidate, Member of Parliament2005
PUBLICATIONS
DescriptionPublished Date
Lema Godbless: Msaada wa haraka kutoka katika Biblia, Arusha2008
Godbless Lema: Wisdom Time, Arusha2008
SPECIAL SKILLS
Skill Name or DescriptionYears ExperienceAcquired ThroughSkill Level
RECOGNITIONS
Recognition TypeRecognition DateReasonAction TakenIssued by
 
tunaangalia uwezo wa mtu katika uongozi na si elimu ya mtu katika uongozi, babu zetu hawajui hata kusoma lakini wametuongoza kwa busara
Wakati huu hapakuwa na sheria ya kuandikwa wala mikataba ya kimataifa.bila elimu wanakuwa hawajiamini,wakiona karatasi na kingereza ni kutetemeka tu.hivi mkuu bila wabunge kuwa na elimu nani? Atabadilisha sera ya madini,na nyingine kibao ambazo ni mbovu ajabu.ebu tafuta tu gvt public yeyote,then tafakari mtu kama lusinde atachangia nn?.
 
Elimu husaidia sana kufunguka, lakini wengi wenye elimu wanatuangusha. Labda kwa sababu ya copy and paste.
 
so what? it is better 4 him he has shown the ability asleader despite of what of kind of cv He has! He will win ur the looser!
 
HATUTAKI ELIMU YA MTU, TUNATAKA MCHANGO WAKE KATIKA JAMII, LEMA ANAOMCHANGO MKUBWA ndo maana namkubali. Hao maprof wamefanya nini kama sio kutuibia tu, angalia mawaziri wasomi wamefanya nini hadi leo? fikiria KAWAWA, SOKOINE, BIBI TITI na wengine ambao shule ni ndogo je?
 
hiyo sekondari kolila ilikuwa ni a-level na kumbuka a-level mwaka wa masomo ulikuwa unaanza july na kuisha may.so no wonder alianza 1991 na kumaliza 1993
 
tatizo sio elimu hapa..tatizo ni kua godbless lema hana personality ya kuongoza jimbo lenye hadhi kama hili la arusha...unaweza kusoma mbaka nywele zika nyonyoka ila ukakosa lhekima..hana hekima kabisa.....mie nimemuona kwa macho yangu nilipo kwenda kwenye kilio cha dada mmoja hapa arusha,wakati ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu kwa kupotelewa na msichana mdogo huyu lema akaingia kwenye nyumba yenye msiba.....alipo ingia unaweza sema petrol station inatembea,alikua ananukia breweries ya kutosha..huku watu wakiwa na huzuni kubwa,akasema "jamani msilie sana,ni swala la kuomba tu ili arudi tena dunia,haya jamani tumuombee afufuke"hiyo kauli iliwafanya ndugu wengine marehemu kutoka nje......sasa hii ni kutokua na hadhi ya uongozi!!!
Nimefuatilia hoja zako zote na nimegundua huna lolote zaidi ya chuki binafsi,kote ulikochangia kuusu lema point yako ya msingi imekua ni personality na ulipoona haueleweki umetafuta jingine la msiba

Ushauri wangu usiumize sana kichwa kuwashawishi wasio shawishika,wewe mchague umpendae na wengine tuache tuamue wenyewe.
 
Back
Top Bottom