Elimu ya dini iwekewe mkazo mashuleni na iwe ni somo la lazima kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Jul 11, 2021
594
1,827
Maadili hutoa maana au muundo dhahiri wa maisha ya mwanaadamu, Maadili ni kanuni fulani za msingi ambazo zinapaswa kushikiliwa katika maisha. Maisha ya kuishi bila maadili hatimaye mtu ataishia kuhisi kutoridhika, kuhisi mwenye hatia na huzuni.

Kama mtoto asipolelewa bila sheria ni haraka zaidi kuharibika na kuharibiwa na jamii yake.

Maadili ndio yanatoa hekima ya kutofautisha kati ya lililo jema na lisilo sahihi. Uelewa wa kile kilicho sawa na kibaya (hayo ndio maadili).

Vituo vya kufundisha maadili ni Nyumbani, Shuleni na Vituo vya ibada (Misikiti, Makanisa, Madrasa na Sunday School). Kwasasa asilimia kubwa Majumbani kwetu hakuna maadili yanayofundishwa kwasababu wazazi hawana muda na watoto, wazazi wote wawili wako busy kutafuta pesa.

Hivyo sehemu inayotegemewa zaidi ni Vituo vya ibada ambapo napo kuna yumba sana hakutoi nafasi ya kutosha, nafasi iliyobaki pekee ipo Mashuleni ambapo mtoto anatumia muda mwingi zaidi huko shuleni.

Ajabu ni kwamba huko Shuleni somo la dini ambalo ndio kitovu cha maadili lipo tu kama sehemu ya mapumziko na halihesabiwi na kuwekewa uzito ipasavyo.

Ingawa nyakati za sasa watu hawalipi uzito mkubwa swala la maadili katika maisha yao. Lakini sababu kubwa ya kuporomoka kwake ni watu kuacha misingi ya dini zao na mafundisho ya imani zao, Serikali kufuta masomo ya dini na kutoyapa kipaombele katika kumpandisha au kumshusha mwanafunzi kitaaluma.

Wazazi sasa wanazingatia zaidi ujuzi wa watoto wao wa kielimu au kifedha, Lakini wakisahau kumfanya kijana wao kuwa "binadamu" mzuri, kwamba kuzingatia maadili yao kutawafanya kufanikiwa zaidi.

Ikiwa masomo ya dini yatapewa kipaombele mashuleni na kujumuishwa katika kumfelisha au kumfaulisha mwanafunzi bila shaka watoto watahudhuria Sunday School na Madrasa kwa wingi, bila shaka wazazi watawahimiza watoto wao kwenda Sunday school na Madrasa ambako huko ndiko maadili hufundishwa zaidi kuliko hata nyumbani.

Ni hatari sana binaadamu kuishi bila hofu, ni hatari sana binaadamu kuishi bila kujali chochote wala lolote. Maadili pekee ndio humpa hofu mwanaadamu, ni maadili pekee ndio humuwekea mipaka mwanaadamu.

Vijana wakiwa na maadili wizi na unyang'anyi vitapungua, umalaya na ukahaba vitapungua, wanawake watapunguza kutembea uchi, mashoga watapungua, mauaji yatapungua, talaka zitapungua, unyanyasaji utapungua, rushwa itapungua, ufisadi utapungua, ulevi utapungua, magerezani watu watapungua na bajeti ya serikali ya kukabiliana na uhalifu itapungua.

BAKIIF Islamic
Kimara, Dar Es Salaam

1711025174177.png
 
vitu vinahitaji kiasi chake sio muda wote elimu ya dini tu

ndio maana jamii kama za wachaga, wahaya, wanyakusa, wasukuma, wakinga, wakurya, n.k. wamewazidi maendeleo warangi, wazaramo, wadigo, wanaoweka kipaumbele elimu ya dini ?

Ajabu ni kwamba maeneo yanayosisitiza elimu ya dini kama Kondoa, imani za kishirikina zipo kwa kiasi kikubwa, kutafuna miraa wanasema sio dhambi kisa haiwaudhi wengine, n.k.

Chuo cha kiislam cha Morogoro waislamu wanakikimbia wanaenda jazana kwenye vyuo vya kikristo sababu wanachapa viboko
 
Dini hapana Aisee labda Ungesema Tamaduni za KMwafrika..Hizi dini za mtume MUDI na PAULO zimeletwa na Meli..Dini ni kifungo..Kabla ya Missionary na Arabs Wazee waliishi kwa Itikadi kali sana..Bint awezi kuolewa bila BIKRA.,Mwanaume lazima uende JANDO na UNYAGO ukafundishwe UANAUME..Lazima ujue KUWINDA,KUOGELEA,KUJIHAMI Hakika Tamaduni za AFRIKA zilikuwa zinavutia sana

Baada ya Ngozi Nyeupe kuingia mambo yalibadirika..Ukizaliwa kwenye Familia ya Dini moja(MUDI au PAULO) Lazima umezeshwe Sumu ya kuchukia Dini nyengine..Inahitaji Akili binafsi kujinasua kwenye kifungo cha DINI

DINI HIZI ZA SHEIKH KIPOZEO,SHEIKH SHARIIF MAJINI?NABII SHILLA,NABII BULLDOZA MWAMPOSA,BISHOPGWAJIBOY, BILA KUSAHAU MCH.MASANJA NA MC.PILIPILI NA ZUMARIDI Ndio zifundishwe darasani ili kuendeleza kizazi cha MBUMBUMBU?? HAPANA AISEE
 
ni kwanini jamii kama za wachaga, wahaya, wanyakusa, wasukuma, wakinga, wakurya, n.k. wamewazidi maendeleo warangi, wazaramo, wadigo, wanaoweka kipaumbele elimu ya dini ?

Ajabu ni kwamba maeneo yanayosisitiza elimu ya dini kama Kondoa, imani za kishirikina zipo kwa kiasi kikubwa, kutafuna miraa wanasema sio dhambi kisa haiwaudhi wengine, n.k.

Chuo cha kiislam cha Morogoro kwanini waislamu wanakikimbia wanaenda jazana kwenye vyuo vya kikristo ? hivi waliacha kuwachapa bakora wanachuo ?
Imani za kidini ni muhimu kwa matokeo ya kiuchumi na maadili, imani huimarisha sifa za tabia kama vile kufanya kazi kwa bidii, uaminifu, uwekevu, na thamani ya muda. Kumbuka pia wahalifu nao hujificha kwenye mwavuli wa dini. Msisitizo ni kwamba Elimu ya dini iwekewe mkazo mashule ili kusaidia kukuza maadili kwa jamii yetu ya sasa.
 
Elimu ya kawaida inatushinda....hadi leo wengine hawapati elimu bora..na hata waliopata imewageuza wakoloni weusi. Tusiotengeneza hata panadol.

Nakubaliana na umuhimu wa dini as a socialising agent, ila itoshe kusema tuna mambo mengi ya kufanya kama nchi, elimu hii muhimu ya dini iendelee kutolewa sehemu husika kwenye mimbari...madrasa, sunday school nk nk.
 
Nina swali la kizushi, naweza kuoa kwa ndoa ya kiislam mkoa tofauti kisa nikarudi mkoa wangu kuendelea na dini yangu huku ndoa ikiwa na vyeti vya kiislam ?

elewa swali usianze mambo ya ni haram
 
vitu vinahitaji kiasi chake sio muda wote elimu ya dini tu

ndio maana jamii kama za wachaga, wahaya, wanyakusa, wasukuma, wakinga, wakurya, n.k. wamewazidi maendeleo warangi, wazaramo, wadigo, wanaoweka kipaumbele elimu ya dini ?

Ajabu ni kwamba maeneo yanayosisitiza elimu ya dini kama Kondoa, imani za kishirikina zipo kwa kiasi kikubwa, kutafuna miraa wanasema sio dhambi kisa haiwaudhi wengine, n.k.

Chuo cha kiislam cha Morogoro waislamu wanakikimbia wanaenda jazana kwenye vyuo vya kikristo sababu wanachapa viboko
Sasa wewe hapa unakosoa elimu ya dini au umeamua kukosoa dini moja? Na kuinyanyua nyingine? Kwa kufanya hivyo bado upo ndani ya mada? Mleta mada amesisitiza kuhusu elimu ya dini ila wewe katika hizo dini ( generally) wewe umeshakuwa specific. Akili za wabongo kwenye kudadavua mambo ni nzito kweli kweli
 
Nioneshe mrangi muislam asiyekula mirungi.

Ntakuonesha mbwa wa njano
 
Dini hapana Aisee labda Ungesema Tamaduni za KMwafrika..Hizi dini za mtume MUDI na PAULO zimeletwa na Meli..Dini ni kifungo..Kabla ya Missionary na Arabs Wazee waliishi kwa Itikadi kali sana..Bint awezi kuolewa bila BIKRA.,Mwanaume lazima uende JANDO na UNYAGO ukafundishwe UANAUME..Lazima ujue KUWINDA,KUOGELEA,KUJIHAMI Hakika Tamaduni za AFRIKA zilikuwa zinavutia sana

Baada ya Ngozi Nyeupe kuingia mambo yalibadirika..Ukizaliwa kwenye Familia ya Dini moja(MUDI au PAULO) Lazima umezeshwe Sumu ya kuchukia Dini nyengine..Inahitaji Akili binafsi kujinasua kwenye kifungo cha DINI

DINI HIZI ZA SHEIKH KIPOZEO,SHEIKH SHARIIF MAJINI?NABII SHILLA,NABII BULLDOZA MWAMPOSA,BISHOPGWAJIBOY, BILA KUSAHAU MCH.MASANJA NA MC.PILIPILI NA ZUMARIDI Ndio zifundishwe darasani ili kuendeleza kizazi cha MBUMBUMBU?? HAPANA AISEE
Dini ni sehemu isiyoepukika ya asili ya mwanadamu. Kwa sababu hiyo ni muhimu watoto wetu wafahamu dini na tamaduni nyingine.

Dini ndio huchocheoa ubora wa maadili kwa vizazi
 
Sema tu watoto wafundishwe maadili mema (ethics) na sio hizi dini zilizotungwa na watu. Somo la dini ni mtu akipenda.
Maadili mema hufundishwa kwa vitendo, ni dini pekee yenye nafasi hiyo. Hata mwanao huwezi mfundisha maadili mema kwa mdomo bali ni kwa vitendo, ufanye mambo mema mbele yake nasio kumkataza kusema uongo ilihali wewe mwenyewe una muongopea.

Dini ndio ina nafasi pana katika kufunza watu maadili
 
Elimu ya kawaida inatushinda....hadi leo wengine hawapati elimu bora..na hata waliopata imewageuza wakoloni weusi. Tusiotengeneza hata panadol.

Nakubaliana na umuhimu wa dini as a socialising agent, ila itoshe kusema tuna mambo mengi ya kufanya kama nchi, elimu hii muhimu ya dini iendelee kutolewa sehemu husika kwenye mimbari...madrasa, sunday school nk nk.
Ili madrasa na sunday school ziheshimike na zipate watoto ni lazima Serikali iliweke somo la dini kua lazima katika mitaala.
 
Nina swali la kizushi, naweza kuoa kwa ndoa ya kiislam mkoa tofauti kisa nikarudi mkoa wangu kuendelea na dini yangu huku ndoa ikiwa na vyeti vya kiislam ?

elewa swali usianze mambo ya ni haram
Rejea mjadala wa Maadili kwenda sambamba na elimu ya dini
 
Sasa wewe hapa unakosoa elimu ya dini au umeamua kukosoa dini moja? Na kuinyanyua nyingine? Kwa kufanya hivyo bado upo ndani ya mada? Mleta mada amesisitiza kuhusu elimu ya dini ila wewe katika hizo dini ( generally) wewe umeshakuwa specific. Akili za wabongo kwenye kudadavua mambo ni nzito kweli kweli
Watu wanachukia kitu bila sababu
 
Elimu ya dini! Dini ipi? Kwanza fahamu nchi hii haingozwi kwa misingi ya dini. Raia wana dini zao zinazoongoza maadili yao kwa mujibu wa mila, desturi na tamaduni zao. Unataka kulazimisha dini/imani kwa wasioiamini? Mambo ya imani yafundishwe huko wanakoabudu
 
Kwa hiyo viongozi na watawala wa nchii hii wanakula kiapo kwa kutumia kitabu gani? kitabu cha mila na desturi au kitabu cha dini?
 
Back
Top Bottom