Elimu ya bure Kuhusu umeme wa jua

Jumla matumizi yako ni watts 129 kwa (economic view huu utakua mtambo wa watts 200 ).... hapa utahitaji battery atleast ya N150 panel watts 100×2 controlla 20A(unaweza pata ata 10A sio mbaya na invetor watts 500......usiku hutowasha tv full time mpaka saa 4 then unaacha taa zenyewe zitapiga mpaka asubuhi .....ukitaka kuongeza muda wa kuangalia tv usiku unaweza kwenda na mtambo wa watts300 .......hu unakua na panel 2 za watts 150 kila moja ...controla 20A invetor watts 750 na batter mbili za N100
Ulichojibu hakihusiani na swali kaka.. lakini anyway nimeshapata ufumbuzi.
 
Nashukuru sana kwa msaada wako mkuu, ninacho fikiria ni kutafuta fundi wa kupima volt kutoka kwenye panel maana naona control charge haina tatizo.Maana nimeazima sola nyingine watt 100 ina charge vizuri kabisa.
Mkuu badili diode ni rahisi
 
Habari wajuzi wa umeme jua
Msaada hapa
Natumia solar system
panel 100 walts
Battery n100 ya unga
Cahrge controller TK20DU(LIGHT AFRICA)
Kuna siku kama 5 zimepita asubuh nilikuwa napiga pasi/kunyoosha nguo niende job kwa solar pasi
Nikasahau kuitoa kwenye solar asubuh adi jion
Narudi nakuta imenyonya battery yote
Nikalala gizani
The next day
Ika charge
Na ikaanza kufanya kazi

Madiliko yaliyotokea
1.Charge controller inaonesha battery inapokea moto hata usiku ikiwa controller inatambua ni usiku kwa kuonesha alama wa mwezi /kawaida huwa inakuwa tofauti
2.nikiwasha taa zinawaka ila controller haioneshi kama moto unapita/kawaida ukiwasha taa huonesha mshale wa umeme kupota
3.kwa siku 3 battery inaonesha ina bar 3 tu
Kwa kawaida hata nitumie vipi nikipata jua kaa siku 2 lazima ioneshe iko full/bar 5 za charge

Swali
Hapo ni nini kimekufa?
Maana charge controller ina behave tofauti na zamani
Karibuni wataalam wa umemw jua kwa ushauri
 
Salama hapa? Naomba msaada kutoka kwa wataalam

Nina Solar Panel Watts 200
Betri 100Ah DC
Inverter 230V AC output

Lakini napowasha TV iliyo katika mfumo wa AC ina 42 watts inch 32 inawaka na kuzima ndani ya dakika moja, nikiwasha tena ndani ya dakika moja inazima. Lakini ipo subwoofer ina uwezo sawa na TV inafanya kazi kama kawaida.

Je tatizo Ni nini katika TV kwanini haiwaki kama kawaida?

Au mfumo wa solar haawezi washa TV ya Aina hiyo?

Au tatizo Ni inverter maana Ni hizi za kichina aborder
 
Nahitaji vifaa vya solar genuine ikiwezekana kutoka Germany. Kariakoo nmepita maduka ni mengi lakini nna wasiwasi na ubora wake. Ni wapi naweza kupata vifaa hivyo?
 
Nahitaji vifaa vya solar genuine ikiwezekana kutoka Germany. Kariakoo nmepita maduka ni mengi lakini nna wasiwasi na ubora wake. Ni wapi naweza kupata vifaa hivyo?
kwenye solar mchawi battery, hapa ni vema ukapata za ujerumani, nenda Laptop City pale posta wanazo
 
Salama hapa? Naomba msaada kutoka kwa wataalam

Nina Solar Panel Watts 200
Betri 100Ah DC
Inverter 230V AC output

Lakini napowasha TV iliyo katika mfumo wa AC ina 42 watts inch 32 inawaka na kuzima ndani ya dakika moja, nikiwasha tena ndani ya dakika moja inazima. Lakini ipo subwoofer ina uwezo sawa na TV inafanya kazi kama kawaida.

Je tatizo Ni nini katika TV kwanini haiwaki kama kawaida?

Au mfumo wa solar haawezi washa TV ya Aina hiyo?

Au tatizo Ni inverter maana Ni hizi za kichina aborder
Angalia kama power supply cable ya hiyo tv ina amps za umeme zinazolingana na zilizoamdikwa kwenye tv
 
Salama hapa? Naomba msaada kutoka kwa wataalam

Nina Solar Panel Watts 200
Betri 100Ah DC
Inverter 230V AC output

Lakini napowasha TV iliyo katika mfumo wa AC ina 42 watts inch 32 inawaka na kuzima ndani ya dakika moja, nikiwasha tena ndani ya dakika moja inazima. Lakini ipo subwoofer ina uwezo sawa na TV inafanya kazi kama kawaida.

Je tatizo Ni nini katika TV kwanini haiwaki kama kawaida?

Au mfumo wa solar haawezi washa TV ya Aina hiyo?

Au tatizo Ni inverter maana Ni hizi za kichina aborder
angalia waya tv wa DC kuna fundo kata waya ondoa fundo kisha waya kuzimechisha kama zilivyo. kisha jaribu
 
Kinachotukatisha tamaa kwa 'Umeme Jua' ni pale unapoenda Ofisi za Watu wa Solar na wanaoamini maswala ya Solar halafu unawakuta wameweka Umeme wa Tanesco (HEP).
Pale unajua hili changa la macho
 
Kinachotukatisha tamaa kwa 'Umeme Jua' ni pale unapoenda Ofisi za Watu wa Solar na wanaoamini maswala ya Solar halafu unawakuta wameweka Umeme wa Tanesco (HEP).
Pale unajua hili changa la macho
😂 😂 😂 😂 😂
 
By Professional mie ni electronics engineer. Ninaishi dar ninaweza kumsaidia yeyote kuhusu hii system bila malipo yoyote, nitakushauri kabla ya kunua na kufunga..online
Habari nina swali kwako naomba tukutane Inbobo!????
 
Kinachotukatisha tamaa kwa 'Umeme Jua' ni pale unapoenda Ofisi za Watu wa Solar na wanaoamini maswala ya Solar halafu unawakuta wameweka Umeme wa Tanesco (HEP).
Pale unajua hili changa la macho
Hiyo ni sawa na Wizara ya Kilimo kuwa Dar es Salaam au Wizara ya Misitu kuwa Dar.

Ofisi nyingi za umeme jua zipo kwenye miji/majiji makubwa kutokana na kutafta masoko na kujitangaza. Wapo wachache wanaofungua matawi vijijini kuongeza fursa ya kuhudumia. So ni kawaida kuona ofisi ya kampuni ya umeme jua wanatumia umeme ambao wengine huwa wanazalisha wenyewe au hufunga battery back up kusaidia na kuwaonyesha wateja kuwa hawakwami ktk kutumia umeme.
 
Kwanza kabisa naomba nitahadhalishe kuwa mimi sio expert wa hii kitu ila nahakika walau mtapata mawili au matatu lakini pia naamini wataalam zaidi watakuja kufafanua na pengine kujibu maswali.

Ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi wana uelewa wa hii nguvu lakini pia nahakika kuwa kwa namna moja ama nyingine elimu ni bahari.

Kwangu nimefunga

1. Panel ya 160w (made in ujerumani).

2. Dry battery ya 500N (made in Ujerumani)

3. Inverter ya Victron/Phoenix) 12v, 350va (made in Philipine) ambayo ni auto na haina kelele

4. Dash board 15A/ solar power controller aina ya Steca/Solarix PRS 1515 ya (made in zhing zong)

Na vifaa tajwa hapo juu vinategemeana na matumizi yako ila mimi nina run

TAA

1Watt 5pcs...vyumbani na chooni
2Watt 6pcs...sebureni, corridor na store
3Watt 9pc...nje

Hizi zinauzwa pale Quality Centre moja 5000/ na zina mwanga wa kutosha kama nilivyoeleza hazitumii umeme mwingi tofauti na zamani kipindi nanunua niliuziwa taa zenye watt 10 mpaka 20 ziko kama tube light hizi za sasa ni bulb ambazo kimsingi ilikuwa hata TV kuangalia ni anasa maana taa tu hazikeshi usiku kucha.

(Nilizibadilisha kwa kununua kwanza chache ili nitest mwanga nikakuta zipo poa kabisa) so ikanilazimu nibadilishe zote.
Zinasambazwa na Step Entertaiment hawa jamaa wa Bongo movie.

Na kwa hakika hapa kwenye taa ndo wengi wetu tunaumia maana taa zinakuwa ni A kizamani wakati tech ime advance sana.

Nina Flat Tv 32"
Nina Laptop

Ambapo nimekuja kugundua laptop inakula umeme mwingi sana kuliko flat tv maana unaweza kuangalia tv siku nzima na ukawa safi tu kuliko tofauti na ukitumia laptop. Hapa siongelei TV zile za zamani zenye shape kama kisogo maana ninayo lakini nilishindwa kuitumia kwenye solar.

FAIDA

Haitatokea hata siku moja vifaa vyako kuungua
Pia gharama yake ni mwanzo tu wakati unanunua vifaa.

HASARA

Umeme wake hautoshi mahitaji yote mf pasi, jiko, fridge japo siku hiz zipo water pump, pasi, fridge na freezer za solar ila sijajua utendaji kazi wake.

Cha zaidi nashauri Panel yako iwe upande ambao jua ndo linaonekana kwa asilimia kubwa japo panel zingine zinahitaji mwanga tu then unatosha kuchaji betri yako.

Na fundi aifunge panel sambamba na bati ili kuisaidia uchafu ama vumbi kuwa linatoka lenyewe na hii itasaidia ufanisi wake pia, kuliko kuifunga horizontal maana itasababisha uchafu na vumbi vigande juu yake.

ANGALIZO

Vitu muhimu vya kuangalia wakati wa manunuzi ni Panel, Betri na Inveter ila kama utahitaji kuwa una chaji simu au radio au tv na kama ni taa tu hauhitaji inverter.

Wataalam munaweza kuongezea hapo.

Pamoja
alfred.kohi@kcd.co.tz
Solar yako kwa siku max ni watts 1200 plus or minus 30w umefunga battery ya jumla ya watts 6000 sasa itajaaje hiyo battery ,,
 
Msaada wa kiufundi, nina solar Panel 150w bettry N100. Matumizi yangu kwa ujumla hayazidi Watt 120. Nimepata Inverter ya 750W. Je inafaa kwa matumizi hayo., je inveter haiongezi matumizi ya Betry?
 
Haina athari kwenye kumaliza umeme ambao umetunzwa kwenye betry? ukizingatia ukubwa wa Inverter dhidi ya matumizi yangu?
Haina athari kwenye kumaliza umeme ambao umetunzwa kwenye betry? ukizingatia ukubwa wa Inverter dhidi ya matumizi yangu?
Matumizi makubwa yawe mchana, usiku yawe matumizi madogo tu
Haina athari kwenye kumaliza umeme ambao umetunzwa kwenye betry? ukizingatia ukubwa wa Inverter dhidi ya matumizi yangu?
 
Kwa panel za zaman za 50watts zilikuwa na uwezo wa kujaza battery ya 100Ah au N100 kutokana na uwezo wa haraka wa kuabsorb jua kwa haraka na pia ikiwa na current kubwa. Kwa hesabu ya:
50w = 100Ah
160w = 300Ah.

Sasa hii panel ya 160w kwa 500Ah na inajaa full atakuwa amepata panel nzur sana.
Battery ya 100Ah kwa 12v ni sawa na watts 1200 solar ya 50w masaa 8 ndo unapata watts 400 ...sasa mahesabu gani mmepiga hapo ..how come panel za sahizi hizo zijaze such a battery
 
Back
Top Bottom