Elimu ya bure Kuhusu umeme wa jua

Elimu ya bure Kuhusu umeme wa jua

By Professional mie ni electronics engineer. Ninaishi dar ninaweza kumsaidia yeyote kuhusu hii system bila malipo yoyote, nitakushauri kabla ya kunua na kufunga..online

Nimefunga Solar System nyumbani 2008 baada ya serekali kubadili mfumo na kuleta LUKU service Charge
Nina 2 Panels 90Watts @ = (180Watts)
Batery 7 sealed za 150Ah@ = 1050Ah

Matumizi
Nina Desktop Computer 1
Nina Laptop 1
Nina Solar Frige kubwa 290Lrs
Nina 500Watts Power invetor
Nina 32 Inch TV flat screen
Nina taa 3watts 11 ndani
nina taa 5watts 7 nje
Nina Brender 400Watts
Nina Music system 2000Watts PMPO ikipiga just kama uko disco
Mafundi wanakujaga na machine zao za kukata chuma na mbao wanatumia bila shida yoyote.

Sijutii kufunga solar system sio kwamba niko sehemu ambayo Tanesco hawajapita hapana nguzo ya umeme iko 1 meter kutoka nyumba yangu ila utumwa sitaki, kila siku bei ya umeme inapanda utasiki watu wanalia na kulalamika. 2008 elfu kumi nilikuwa napata 112 units sasa hivi 10,000 hata 38 units hupati
Mabadiliko ya kweli hutokea kwenye fikra na unayoyaona kwa nje ni matokeo tu...

Watanzania Tubadili jinsi tunavyo fikiria life is good
Panel zako ni ndogo kujaza hizo battery
 
Habari mkuu. Nimeufatilia mjadala huu wa solar power kwa umakini sana.

Sasa mimi swali langu ni hili
Mimi solar yangu ni watt 120

Nina tv ya watt 55
King'amuzi watt 10
Taa8 za watt 3
Taa 8 za watt 5

Je hapa naweza angali tv usiku na mchana bila tatizo lolote?
Inveter ya sola yako ni watts ngap? Battery yake? Controller na panel zake?
 
Ni hivyo mkuuView attachment 896730
20181013_155043.jpeg
20181013_155016.jpeg
20181013_155733.jpeg
 
Wadau naomba nijulishwe, Nina betri N100,na Sola Watt 150,nimetumia muda wa mwaka mmoja, lakini kwa sasa solar haichaji betri tena, nimejaribu kutoa kwenye system ya connection ili nichaji betri peke yake lakini naona bado haichaji,Natumia taa 3 na kuchaji CM.
 
Kwenye mfumo wako wa solar kuna kidhibiti chaji? Kama betri yako ni ya kuweka maji fanya uangalie maji.
 
Betri ni dry, ila nikienda kuchaji kwenye sola nyingine ina chaji, yaani ni kwamba moto ni mdogo sana unaotoksa Katika sola,
 
Charger control ipo? Ugonjwa Mkubwa wa mfumo wa umeme jua ni betri kwa sababu ya kuto kuweka kidhibiti chaji au pannel kubwa kuzidi betri au kinyume chake, matumizi makubwa kuzidi uwezo wa betri.
 
Angalia pannel kama kuna kivuli ktk mwelekeo wa pannel zako kwa muda wote kuanzia saa 09:00 mpaka saa 15:00 kama kuna kimvuli, au kinyesi cha ndege
 
Charger control ipo,na taa ya kuonesha panel imeungwa inaonesha na taa ya kuonesha kuwa betri inaingiza chaji inawaka lakini haioneshi kujaa hata ifike jioni,na jua ni kutosha maana nipo katika ukanda wa nusu jangwa
 
Angalia pannel kama kuna kivuli ktk mwelekeo wa pannel zako kwa muda wote kuanzia saa 09:00 mpaka saa 15:00 kama kuna kimvuli, au kinyesi cha ndege
Sehemu nilipo ni nusi jangwa na jua ni kianzia asubuhi mpaka jioni
 
Fanya utafute fundi kupima volt kutoka kwenye pannel na short cct current mpaka kwenye betri yawezekana charger control imeharibika na hivyo kuto kupeleka umeme kwenye betri
 
Kwanza kabisa naomba nitahadhalishe kuwa mimi sio expert wa hii kitu ila nahakika walau mtapata mawili au matatu lakini pia naamini wataalam zaidi watakuja kufafanua na pengine kujibu maswali.

Ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi wana uelewa wa hii nguvu lakini pia nahakika kuwa kwa namna moja ama nyingine elimu ni bahari.

Kwangu nimefunga

1. Panel ya 160w (made in ujerumani).

2. Dry battery ya 500N (made in Ujerumani)

3. Inverter ya Victron/Phoenix) 12v, 350va (made in Philipine) ambayo ni auto na haina kelele

4. Dash board 15A/ solar power controller aina ya Steca/Solarix PRS 1515 ya (made in zhing zong)

Na vifaa tajwa hapo juu vinategemeana na matumizi yako ila mimi nina run

TAA

1Watt 5pcs...vyumbani na chooni
2Watt 6pcs...sebureni, corridor na store
3Watt 9pc...nje

Hizi zinauzwa pale Quality Centre moja 5000/ na zina mwanga wa kutosha kama nilivyoeleza hazitumii umeme mwingi tofauti na zamani kipindi nanunua niliuziwa taa zenye watt 10 mpaka 20 ziko kama tube light hizi za sasa ni bulb ambazo kimsingi ilikuwa hata TV kuangalia ni anasa maana taa tu hazikeshi usiku kucha.

(Nilizibadilisha kwa kununua kwanza chache ili nitest mwanga nikakuta zipo poa kabisa) so ikanilazimu nibadilishe zote.
Zinasambazwa na Step Entertaiment hawa jamaa wa Bongo movie.

Na kwa hakika hapa kwenye taa ndo wengi wetu tunaumia maana taa zinakuwa ni A kizamani wakati tech ime advance sana.

Nina Flat Tv 32"
Nina Laptop

Ambapo nimekuja kugundua laptop inakula umeme mwingi sana kuliko flat tv maana unaweza kuangalia tv siku nzima na ukawa safi tu kuliko tofauti na ukitumia laptop. Hapa siongelei TV zile za zamani zenye shape kama kisogo maana ninayo lakini nilishindwa kuitumia kwenye solar.

FAIDA

Haitatokea hata siku moja vifaa vyako kuungua
Pia gharama yake ni mwanzo tu wakati unanunua vifaa.

HASARA

Umeme wake hautoshi mahitaji yote mf pasi, jiko, fridge japo siku hiz zipo water pump, pasi, fridge na freezer za solar ila sijajua utendaji kazi wake.

Cha zaidi nashauri Panel yako iwe upande ambao jua ndo linaonekana kwa asilimia kubwa japo panel zingine zinahitaji mwanga tu then unatosha kuchaji betri yako.

Na fundi aifunge panel sambamba na bati ili kuisaidia uchafu ama vumbi kuwa linatoka lenyewe na hii itasaidia ufanisi wake pia, kuliko kuifunga horizontal maana itasababisha uchafu na vumbi vigande juu yake.

ANGALIZO

Vitu muhimu vya kuangalia wakati wa manunuzi ni Panel, Betri na Inveter ila kama utahitaji kuwa una chaji simu au radio au tv na kama ni taa tu hauhitaji inverter.

Wataalam munaweza kuongezea hapo.

Pamoja
alfred.kohi@kcd.co.tz
Mfano nikitaka nitumie vifaa vyote vya solar (mf TV,redio,pass n.k) kuna haja ya kuwa na inveter ? mana umeme wa solar ni DC na vifaa vyake pia ni DC
 
Mkuu vitu muhimu ni:
1. Solar panel

2. Charge controller

3. Battery.

Ila km una vifaa vinavyotumia umeme mkondo geu(Alternating Current AC) ni muhimu kuwa na inverter ili kubadili kiwango cha voltage kutoka umeme mkondo mnyoofu(Direct Current DC) au umeme wa battery kuwa km umeme wa Tanesco.
Nina battery limeandikwa 12V 18Ah, hapo power ni kiasi gani mtaalam ? Nakuwa confused kidogo ktk hili
 
Kwanza kabisa naomba nitahadhalishe kuwa mimi sio expert wa hii kitu ila nahakika walau mtapata mawili au matatu lakini pia naamini wataalam zaidi watakuja kufafanua na pengine kujibu maswali.

Ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi wana uelewa wa hii nguvu lakini pia nahakika kuwa kwa namna moja ama nyingine elimu ni bahari.

Kwangu nimefunga

1. Panel ya 160w (made in ujerumani).

2. Dry battery ya 500N (made in Ujerumani)

3. Inverter ya Victron/Phoenix) 12v, 350va (made in Philipine) ambayo ni auto na haina kelele

4. Dash board 15A/ solar power controller aina ya Steca/Solarix PRS 1515 ya (made in zhing zong)

Na vifaa tajwa hapo juu vinategemeana na matumizi yako ila mimi nina run

TAA

1Watt 5pcs...vyumbani na chooni
2Watt 6pcs...sebureni, corridor na store
3Watt 9pc...nje

Hizi zinauzwa pale Quality Centre moja 5000/ na zina mwanga wa kutosha kama nilivyoeleza hazitumii umeme mwingi tofauti na zamani kipindi nanunua niliuziwa taa zenye watt 10 mpaka 20 ziko kama tube light hizi za sasa ni bulb ambazo kimsingi ilikuwa hata TV kuangalia ni anasa maana taa tu hazikeshi usiku kucha.

(Nilizibadilisha kwa kununua kwanza chache ili nitest mwanga nikakuta zipo poa kabisa) so ikanilazimu nibadilishe zote.
Zinasambazwa na Step Entertaiment hawa jamaa wa Bongo movie.

Na kwa hakika hapa kwenye taa ndo wengi wetu tunaumia maana taa zinakuwa ni A kizamani wakati tech ime advance sana.

Nina Flat Tv 32"
Nina Laptop

Ambapo nimekuja kugundua laptop inakula umeme mwingi sana kuliko flat tv maana unaweza kuangalia tv siku nzima na ukawa safi tu kuliko tofauti na ukitumia laptop. Hapa siongelei TV zile za zamani zenye shape kama kisogo maana ninayo lakini nilishindwa kuitumia kwenye solar.

FAIDA

Haitatokea hata siku moja vifaa vyako kuungua
Pia gharama yake ni mwanzo tu wakati unanunua vifaa.

HASARA

Umeme wake hautoshi mahitaji yote mf pasi, jiko, fridge japo siku hiz zipo water pump, pasi, fridge na freezer za solar ila sijajua utendaji kazi wake.

Cha zaidi nashauri Panel yako iwe upande ambao jua ndo linaonekana kwa asilimia kubwa japo panel zingine zinahitaji mwanga tu then unatosha kuchaji betri yako.

Na fundi aifunge panel sambamba na bati ili kuisaidia uchafu ama vumbi kuwa linatoka lenyewe na hii itasaidia ufanisi wake pia, kuliko kuifunga horizontal maana itasababisha uchafu na vumbi vigande juu yake.

ANGALIZO

Vitu muhimu vya kuangalia wakati wa manunuzi ni Panel, Betri na Inveter ila kama utahitaji kuwa una chaji simu au radio au tv na kama ni taa tu hauhitaji inverter.

Wataalam munaweza kuongezea hapo.

Pamoja
alfred.kohi@kcd.co.tz
Ungetumia vifaa vya solar ungeenjoy zaidi, kuna solar TV 20W, redio 15W, fan 15W yani ukichaji once, unaweza ukatumia hata siku tatu na kuendelea bila kuchaji tena
 
Nashukuru sana kwa msaada wako mkuu, ninacho fikiria ni kutafuta fundi wa kupima volt kutoka kwenye panel maana naona control charge haina tatizo.Maana nimeazima sola nyingine watt 100 ina charge vizuri kabisa.
Fanya utafute fundi kupima volt kutoka kwenye pannel na short cct current mpaka kwenye betri yawezekana charger control imeharibika na hivyo kuto kupeleka umeme kwenye betri
 
Mbona hunijibu
Jumla matumizi yako ni watts 129 kwa (economic view huu utakua mtambo wa watts 200 ).... hapa utahitaji battery atleast ya N150 panel watts 100×2 controlla 20A(unaweza pata ata 10A sio mbaya na invetor watts 500......usiku hutowasha tv full time mpaka saa 4 then unaacha taa zenyewe zitapiga mpaka asubuhi .....ukitaka kuongeza muda wa kuangalia tv usiku unaweza kwenda na mtambo wa watts300 .......hu unakua na panel 2 za watts 150 kila moja ...controla 20A invetor watts 750 na batter mbili za N100
 
Back
Top Bottom