Elimu ya bure Kuhusu umeme wa jua

Elimu ya bure Kuhusu umeme wa jua

huku nikiunga betri zaid ya 1 inveter inaungua hapa inakuwaje
Inverter zinakuwa rated kwa DC voltage na Power output. Sasa kama inverter ni 12V, ukiunganisha battery mbili za 12V halafu ukaziunganisha katika mfumo wa series basi DC voltage itakuwa 24V hivyo utaunguza inverter. Hapa ntakushauri uunge battery zako katika mfumo wa parallel ili ubakiwe na 12V

kingine kinaweza kusababisha ni kuchanganya polarity (+/-). umeme wa DC ni muhimu kuzingatia polarity kwani ukichanganya polarity utaunguza kifaa husika. Japo maendeleo ya technology yanasaidia siku hizi baadhi ya vifaa vinakuja vikiwa na protection endapo utachanganya polarity.
 
Back
Top Bottom