Nafikiri tunajaribu kutafuta majawabu rahisi kwa maswali magumu. Hakuna dhamira ya dhati ya kutaka kuboresha elimu ya taifa letu. Watu tunashindwa kujiuliza kwa nini waliosoma zamani walikuwa bora zaidi. Watu waliomaliza darasa la nne walikuwa na bado ni bora kuliko wanaomaliza shule za msingi sasa. Waliomaliza darasa la nane walikuwa na ni bora kuliko wanaomaliza kidato cha sita sasa. Waliomaliza darasa la kumi waliweza kwenda Chuo kikuu moja kwa moja. Walikuwa wazuri si kwa lugha (Kiingereza na Kiswahili) lakini hata kwa hisabati na sayansi kwa ujumla(linganisha waandishi wa vitabu vya Kiswahili na Kiingereza wa zamani na sasa). Tusione aibu kugeuka nyuma. Tuchunguze ni nini kilikuwa kikifanyika huko nyuma kupata mafanikio na tunafanya nini sasa kwa mafanikio mabovu tunayo yapata sasa. Ukiangalia waheshimiwa wetu wanaoshabikia Kiswahili wao wenyewe utakuta hawawezi kuongea Kiswahili kwa ufasaha (huchanganya Kiswahili na Kiingereza) sijuwi ni kwa maksudi au ni kujifanya wao ni zaidi!! Tofauti na jirani zetu wakiamua kuongea Kiswahili wanaongea Kiswahili kizuri mpaka unapenda!! Achana na lafudhi maana hata hapa kwetu Kiswahili kina lafudhi tofauti kutegemea na lugha mama ya mzungumzaji. Ni vema tuboreshe ufundishaji wa Kiingereza na hisabati kuanzia chechea ili watoto wapende na waijue lugha hiyo na hisabati, hatutakuwa na shida huko mbeleni kufundisha masomo mengine kwa kimombo!!