Elimu ya Bajeti kwenye Familia.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,884
ELIMU YA BAJETI KWENYE FAMILIA!

Anaandika, Robert Heriel.

Picha linaanza nikaambiwa kwenye maisha hakuna pesa ndogo, sijafika mbali naambiwa nisiidharau pesa yoyote ipitayo mikononi mwangu. Picha linaendelea naambiwa usidharau kazi yoyote Ile ambayo iko mbele yako, siku zote fanya kilichombele yako ilimradi kiwe halali.

Picha linaishia kwenye mapato na matumizi, hapo ndipo kitu kinachoitwa Bajeti hutokea.

Mtu mwenye malengo lazima awe na Mipango, na kwenye mipango hapatakosekana Bajeti. Ni kusema Bajeti ni sehemu ya mpango mkakati WA kutimiza Malengo.

Bajeti lazima iangalie lengo la maisha, na nini kinatufanya tuendelee kuishi,
Lengo la maisha ni kuishi, na ili tuishi na tuendelee kuwepo lazima Tule chakula,
Tunakula ili tuishi, tunaishi ili tuweze kuendeleza maisha ya Dunia Kwa kushirikiana na viumbe wengine, iwe viumbe hai ya laa.

Bajeti Namba moja ni yachakula, hii ndio Jambo la Kwanza kulizingatia kwenye maisha,
Chakula ni dawa, chakula hufukuza magonjwa, chakula kinatufanya tuwe na Afya njema,

Ili akili itulie ni lazima ijue chakula chauhakika,
Mtu anayeweza Kula pekee hawezi kuwa na akili ya kuwaza mambo mengine, kuwaza chakula Kwa uhaba wake ni kuifanya akili iwe na njaa.

Namna ya kuweka Bajeti
1. Nunua vyakula vya kutosha Kwa jumla ukiweza vya wiki au mwezi au miezi mingi zaidi. Usinunue rejareja

2. Usipende kupikapika kila mara ikiwa uchumi wako haupo thabiti, ukiweza upike vyakula vya moja Kwa moja, yaani unachokula mchana na usiku, au utakachokula usiku na kesho yake mchana.
Mfano Wali maharage, Makande, Ndizi, n.k.

Kupika chakula cha moja Kwa moja, kitakusaidia kupunguza gharama za Mafuta, chumvi, Gesi au mkaa au umeme, matumizi ya Sabuni, pamoja na muda.
Usipike pike hovyo,

3. Usiache Redio au Luninga vikiwa vinaongea wakati huvitumii.
Yaani upo nje unafua alafu ndani umeacha Luninga au TV ipo ON

4. Usiwe na Safari zisizo zalisha hata Kama unapanda Daladala,

5. Nunua bando Kwa kiasi na liwe linazalisha, Kama ni la starehe basi usitumia zaidi ya elfu moja Kwa siku.

6. Usitoe pesa Kwa Mwanamke ambaye sio mke wako au ambaye hana mtoto wako.
Na Kama utatoa uwe unafanya biashara, elfu kumi akupe Huduma inayoendana na pesa hiyo.

7. Usifue fue hovyo ikiwa umevaa nguo mara moja. Pia usivae nguo muda mrefu mpaka zikachafuka Sana. Kwani utatumia sabuni nyingi kuzitakatisha.

8. Usiogeoge hovyo, angalau Kwa siku mara moja. Utapunguza bajeti ya maji, Mafuta, na sabuni ya kuogea.

9. Safisha Meno mara mbili Kwa siku, kwani hayo ndio yanakusaidia kumeng'enya chakula katika hatua za awali.

10. Usiende kanisani na usitoe Sadaka au michango isiyo na umuhimu wowote. Mfano Kama kipato chako ni Tsh 300,000/= utatoa Kwa mwezi elfu 30,000 Kama Ada ya mambo yote ya kiroho, ikiwemo Sadaka na mambo ya Ibada Kwa mwezi, hii ni kusema kila wiki ukienda kanisani utoe elfu 5 Kama Sadaka, alafu elfu mbili Kama michango ya Kanisa. Kwa mwezi itakuwa 28,000/=
Hiyo ni Kwa kipato hicho.

Ukienda Kanisani au Kwa mganga ili upate mafanikio wakakutaka pesa, waambie ufanikiwe Kwanza ndio uwape pesa na sio uwape pesa ndio ufanikiwe.
Kama wamekupa utajiri tafsiri yake wanauwezo wa kukunyang'anya ikiwa hutowalipa pesa Yao.
Na utoe Kama unaona Huko kanisani unapata faida za wazi

11. Starehe, kunywa pombe au vitu uvipendavyo Kwa kuweka 5% katika kila senti uipatayo iwe Kwa siku au Kwa mwezi.

12. Zingatia mlo kamili, na kunywa maji mengi, kisha jichunge na Mazingira hatarishi ya kukuletea magonjwa, kuepuka kuugua ugua, kama utaweza kata Bima ya Afya, Kama huwezi basi zingatia mlo kamili wa haja na maji walau Lita tatu Kwa siku.

13. Usiwe na familia kubwa ambayo itakuwa na wanyonyaji wengi, wategemezi.
Kama utakaa na ndugu basi hakikisha wanazalisha iwe unawapa kazi za kuuza vitu vidogo, kufuga, kupika maandazi n.k.
Usikae na mtu asiyezalisha labda awe mtoto mdogo chini ya miaka 10.
Na ukae Naye Kama Wazazi wake wamefariki.

Mifano ya watu waliokaa Kwa watu ni Kama Yakobo alikaa Kwa Mjomba wake Labani, hakukaa bure Bali alikuwa anachunga mifugo,
Musa aliishi ukweni midiani hakukaa bure alipewa kazi ya kuzalisha Kwa kuchunga mifugo

Kila mtu akiwa mzalishaji ndani ya familia automatically umasikini utakimbia.

Watoto wanaokuja Likizo wapewe kazi nyepesi za uzalishaji ili siku ya kuondoka wapate zawadi na nahitaji Yao ya shule Kama Sare, madaftari, viatu n.k.
Asikae mtu Bure ili bajeti isiathirike.

14. Vifurushi vya Chaneli viwekwe kulingana na mahitaji ya wanafamilia wote na sio mtu mmoja ili kuondoa Ubinafsi.
Kama uwezo mdogo muwe na Kisimbuzi kimoja tuu kinatosha.

15. Kila mtoto ndani ya familia awe na kimradi chake kidogo kumjengea uwezo wa kusimamia biashara, mfano Mtoto wa kiume unaweza mnunulia kuku wawili yeye akija jioni kutoka shule kazi yake ni kuwasimamia, mpe mtoto ukaribu na nature hasa wanyama hii itamfanya kuwa na tafakuri .
Baadhi ya vitu vya mtoto vinunue kutokana na mapato ya Mradi wake labda kuuza mayai ununue kalamu au Daftari. Hakikisha umwambie na Ajue pesa hiyo inatokana na jasho lake, msifie na mpe moyo

16. Vitu vya watoto vinunuliwe Kwa jumla, na mtoto aambiwe na kupewa Muongozo wa namna wa kutumia vitu vyake vikiwemo vya shule.

17. Matumizi ya Mke yahusishwe Kwa mwezi. Angalau msuko na mtindo ya nywele muchague inayokaa angalau mwezi mmoja.
Kama ni nafuu basi walau mara mbili kila mwezi. Hakikisha mkeo anapendeza hata Kama kipato ni kidogo.
Urembo ni mahesabu.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
 
Sasa mimi muislamu huko kanisani nitaendaje? Ondoa hiyo namba 10 na 11. Mambo mengi yamekaa vizuri Sana
 
59588790-3.jpg

Ngoja nitafakari jambo.
 
Imara sana
 
mfano Mtoto wa kiume unaweza mnunulia kuku wawili yeye akija jioni kutoka shule kazi yake ni kuwasimamia, mpe mtoto ukaribu na nature hasa wanyama hii itamfanya kuwa na tafakuri .
Hii ni point ya msingi sana hasa katika kuwakuza watoto wetu juu ya ufahamu wa mambo na kukuza ubongo
 
Mada tamu sana hii.

Nimependa hii ya kila mtu azalishe, Kama njia mojawapo ya kupambana na umaskini.
 
Back
Top Bottom